Nimetelekezwa na ujauzito, natafuta kazi

Asante sana kwa ushauri. Nimeshapata kazi ya kujishikiza kwa wakati huu rafiki yangu yani nina furaha sana kiukweli. Huku jf kuna wakatisha tamaa na watu wazuri pia wapo. Kikubwa nitapambana hadi tone langu la mwisho la damu ili huyu kiumbe aje duniani. Mungu ni mwema
 
Mkuu
Umeeleweka Sana JF Ina Watu Tele Utapata Msaada Sahihi
 
Kuna vivulana huu uzi kazi kucheka cheka tu na kukebehi..lakini deep inside walilelewa na mama tu ..shame !.huyu dada atakuja toa iushuhuda Mungu atakavyomwinua
Kabisa. Na ninachoamini ni kwamba ukiona mwanamke yeyote amebeba ujauzito na kupitia shida na kukataliwa ujue kwamba kinachopigwa vita ni kiumbe kilichoko tumboni kinakua kimebeba hatma kubwa ya maisha ndio maana anakataliwa asizaliwe. Kwa hiyo siwezi kumlaumu mtu hapa sio wao ni shetani anataka kukatisha hatma ya kiumbe kinachotarajiwa kuzaliwa... kikubwa tuombeane tu wana jf hii dunia ina mengi na hapa tunapita tu sio kwetu tukumbuke na tujifunze kuneneana na kutamkiana mema.... J2 njema niwatakie
 
Ujumbe mzito sana ...! Ongea na mwanao akiwa tumboni mwambie unampenda na kumthamini
 
Aiseee pole sana [emoji119]
 
Pole sana,aliyekutelekeza kazingua sana,alitakiwa ashirikiane nawewe hadi mtoto azaliwe.Makosa yameshatokea,lakini kukata mawasiliano mazima,kwakweli siyo vizuri.Mtoto tarajali,amekosewa pia.Pole,pambana,nina uhakika unapata msaada stahki.
 
double click.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…