Nimetelekezwa na ujauzito, natafuta kazi

Nimetelekezwa na ujauzito, natafuta kazi

Watu wa Mungu mpoo?

Mimi ni member wa JF tangu miaka ilopita nimekuja na ID tofauti ili nieleze yaliyonikuta iwe funzo na ushuhuda kwa wengine.

Niliweka post hapa mika ilopita na kwa bahati tu sijui niseme nzuri au mbaya ila Mungu ndio anajua, nikapata mwanaume ambaye tulianza mahusiano ambayo yalikuwa siriazi kidogo.

Baada ya muda tukapanga mipango ya kuanza mikakati ya kufunga ndoa. Na wakati huo huo ujauzito ukawa umeingia kwangu. Sasa tangu nilipomwambia yule mwanaume kuwa nina ujauzito aliniblock simu na namba zote mawasiliano hakuna. Hadi leo amenitelekezea ujauzito. Alichoniambia mara ya mwisho kabla hajanikimbia ni "wewe ulivyobeba ujauzito si ulijua unabeba ujauzito na sina pesa za kukutunza" kwa maana hiyo nipambane na hali yangu mwenyewe.

Kiukweli maisha kwangu yamekuwa magumu maana ujauzito umefikisha miezi saba na siwezi kufanya kazi nilokuwa nafanya hapo mwanzo. Daktari alinisahuri niachane nayo maana ni kazi ya kusimama zaidi ya masaa saba endapo nitapata wateja mfululizo.

Me nimeleta hili janga lilonipata ili tuendelee kuwa makini humu. Tusikurupukie watu sio wote ni wazuri kama tunavyodhani

Pia nimekuja kuomba kwa yeyote anayeweza kuniajiri kwa kazi yoyote ambayo sio ya kusimama muda mrefu kwa muda wa miezi hii mitatu ya mwishoni nina uhitaji wa kazi ili walao nipate pesa kwa ajili ya kujifungua maana sina msaada wowote wa kifedha wala vifaa vya kujifungulia. Sina matatizo yoyote ya afya hadi sasa yatakayonifanya nishindwe kuhuduria kwenye kazi hiyo nitakayoipata.

Kwa vigezo mimi ni mhitimu wa elimu ya kidato cha sita najua lugha ya kiswahili na kiingereza pia ninajua kutumia komputa vizuri. Naahidi kwamba atakaeniajiri hatajuta licha ya kuwa mimi ni mjamzito.

Mungu awabariki sana.
Umefika chuo?
 
Sina cha ku comment kwa kweli

Ila nyie wanawake nawapa ushauri wa bure:

Most of us men huku JF ni dont care humu, na wengi hatupo serious tunapenda chini tu tukimwaga wazungu ndo biashara imeishia hapo....

Punguzeni kujirahisisha na maneno yetu matamu matamu maana tutazidi kuwaumiza, to some of us.

Pia hizo PM zenu ni bora mngefunga tu.

I mean no malice....

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 SEMA HIKI KISA NAONA NI KAMA CHAI HIVI. SIJUI KWANN

YOU CAN'T BE THIS DUMB. AU NI MIMI SIJAELEWA
 
Kufuatia uandishi wako...!

1.Wewe ni mtu mzima mwenye umri kati ya 35-40
2.Uliingia kwenye mahusiano na mume wa mtu
3.Ulikuwa una tafuta mume Kwa mhemuko wa kuzaa
4.Hakuna mimba ya bahati mbaya kwenye umri wako ,ulikuwa unajua unacho kufanya
5.Mwanaume alikuwa ana stress zake na hustling zake za maisha hakuwa serious
💯💯
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣😆😆😆😆

Sijui kwann nacheka kaa fala 😅😅😅😅

Asee vidume tumekuwa mbwa kweli.

Tunataka kimasihara tu, walai kuweni makini nyie watu fungeni pm hizo.

Msije mkanasishwa vibaya.
Mtu aliefikisha miak 18 kuliwa anaamua mwenyew Kwa hiyar yake na mapenz tele 😀😀ila kuchukua tahadhari ndio muhimu sana
 
Ukute ni chai
Aisee mi siamini kuna mwanamke anaweza kuwa mjinga kiasi hiki duuuh. Hapana bana

Yaani umkubalie kumzalia kapuku kweli asiye na direction na maisha...

Au alilogwa sio akili zake hizi, mi nakataa kwa kweli..

Yaani vitu vingine ni kutumia akili ndogo tu lakini hii nakataa asee,

Chai ya moto kabisa
 
Back
Top Bottom