Nimetengeneza milioni 30 faida ya kilimo ndani ya miaka 3

Nimetengeneza milioni 30 faida ya kilimo ndani ya miaka 3

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,917
Reaction score
11,801
Nimeanza kulima serious toka mwaka 2019, nikilima mahindi na viazi vitamu ndani ya misimu mitatu yaani toka 2022 mpaka sasa nimeweza kutengeneza faida ya 30M kupitia kilimo cha mahindi, viazi vitamu, na maharage.
Kwa hakika kilimo ni biashara tamu.

Nawashauri vijana wenzangu mchangamkie fursa.
 
Kwanza kabisa 30M sio hela nyingi za kukufanya uje utupe testimony ukitegemea utatu inspire. Secondly, ume invest how much kuja kupata hio 30M kwa miaka mitatu..? Tudadavulie mahesabu yalivyo mpaka faida ya 30M ipatikane. Thirdly, jaribu kutizama agribusiness pia, ina hela kuliko kulimo. Uki invest vizuri kwenye agribusiness za horticulture, 30M ni hela ya miezi miwili hadi mitatu unaipata.
 
Tuwekee hapa gharama na faida kwa kuzingatia ukubwa wa mashamba na aina ya mazao
Inaweza kuwa hamasa kwa wengine
 
Kwanza kabisa 30M sio hela nyingi za kukufanya uje utupe testimony ukitegemea utatu inspire. Secondly, ume invest how much kuja kupata hio 30M kwa miaka mitatu..? Tudadavulie mahesabu yalivyo mpaka faida ya 30M ipatikane. Thirdly, jaribu kutizama agribusiness pia, ina hela kuliko kulimo. Uki invest vizuri kwenye agribusiness za horticulture, 30M ni hela ya miezi miwili hadi mitatu unaipata.
Hata hivyo sijaleta uzi kuwa inspire nyie matajiri wakubwa, uzi wangu unawalenga vijana ambao hawana mitaji wanaoweza kujiajiri kupitia kilimo.
 
Kwanza nikupongeze sana mkuu. Ila Kimahesabu M30 kwa miaka mitatu yakutoka jasho na damu M30 ni pesa ndogo ila kwakuwa mtaji umepanda hii itakuwa njia yako ya kudouble hiyo M30 na kufika mbali.
Milioni 30 ni pesa ndogo kwa nyie matajiri lakini kwa vijana wanaotafuta maisha ni pesa nyingi sana.
 
Hata hivyo sijaleta uzi kuwa inspire nyie matajiri wakubwa, uzi wangu unawalenga vijana ambao hawana mitaji wanaoweza kujiajiri kupitia kilimo.

Matajiri wepi Molembe!? Matajiri ambao efu10 wanaiona ndogo lakini means ya kuipata bila wizi na ujanjaujanja hawana🙄

Hebu tuwekee tumaelezo zaidi tujifunze hata kama faida ni milioni 10 sio haba
 
30,000,000 / 36 (miezi) = 833,333 >> 850,000 (kwa mwezi)

Uzi wako Maana yake ni kwamba au kichwa chake kinasema

Nimetengeneza 850,000 faida ya kilimo kwa mwezi mmoja.

Sisemi 850,000 ni pesa ndogo ila binafsi naamini umetumia nguvu nyingi

pesa nyingi,akili nyingi kutafuta faida ndogo ambayo bila hata nguvu ulizotumia ungeweza ipata.
 
Back
Top Bottom