Nimetoa sharti la kupewa laki kila mwezi ....vinginevyo atambae

dada YANGU, KULIPWA LAKI KWA MWEZI YAN UNAONA BONGE LA DAU? HONGERA KWA KUUZA
 
Thamani yako ni sawasawa na Tshs:5000/= kwa siku X 5Dys = Tshs:25,000/= X 4Weeks = Tshs: 100,000/=
 
Umeandika upuuzi kwa kujiamini wakati unajiuza halafu kwa bei chee bwege wewe pandisha bei biashara hiyo
 
Kuna mtanashati ameonesha nia kutaka kunioa. Nami nikaona niwe muwazi kwake mapema isije ikazua balaa siku za usoni.

Nimefunguka kinaga ubaga kuwa mwanamke mazingira, mwanamke matunzo. Nikaenda mbali zaidi kwa kumpa usemi usemao "ukiona mbwa anakonda lawama zinaenda kwa mwenye mbwa". Na mm sitaki kuchakaa nitakapo olewa.

Basi nikamuambia ili kuhakikisha naendelea kupendeza nitataka uwe unanipa pesa kwa ajili ya matumizi yangu ya dharura isiyopungua laki. Hii pesa pamoja na mshahara wangu usiiihesabie kwenye matumizi yoyote ya nyumbani wala usiichukulie kama ndiyo hela ya matunzo yangu. Hii ni kama pocket money tu. Ili mtoto wa watu niendelee kuchanua na nisichake kwa stress.

Ndiyo. Huko ndiyo kuolewa, mwanaume si ni kichwa cha nyumba!??Siyo niolewe halafu bado niendelee kuishi kwa kuiwazia hela ya kula, kodi, kuvaa, kunywa,n.k. Hela ya kuendesha maisha ya familia inatafutwa na mwanaume mm si nimeolewa bhana.!?Mshahara wangu ni kwa ajili ya mambo yangu. Kazi yangu kubwa ni kuzaa tu. Ndiyo maana nchi za kiarabu huko mwanamke akibeba mimba mumewe inabidi alipe hela nyingi sana kama asante kwa mkewe. Na bado wanawake wengi ktk nchi hizo siyo tu kwamba hawaendi maofisini, bali hata sokoni hawaendi.

Nimempa hilo sharti, akiliona analiweza poa, akishindwa basi ajue siyo fungu lake.

ONYO; Wanaume bebeni jukumu la kulea familia, msioe kwa kuangalia mishahara ya wake zenu. Wanawake wanapaswa kutunzwa. Mishahara yao ipo kama ziada kwa matumizi yao binafsi.
Mkikosa wa kuwaoa msilalamike km style zenyewe ndo hizo,na huyo mume asitegemee maendeleo huko ndani labda awe na assumption yuko pekee yake kule ndani.
 
Pasi na unafiki

wewe utakuwa ni mfanyabiashara ya uchi
Wanaume tu wajanja sana atakubali masharti huku ndani akicheka, hata hiyo anaweza kudabo, akimega anakata mazoea..wanawake jishusheni kwa wanaume mle vya uvunguni, ukijifanya mjanja ohooo hatufai tukiamua.
All in all tuna upendo mzito kwa mwanamke mwelewa na sio machangu kama mleta uzi
 
Mmh bado hajaweza kutambaa tuu na maneno yote ayo yaliyokutoka
 
Ukifika 30s hiyo laki utatoa wewe ili uolewe, hata bibi alikuwa binti

Heshima pesa
 
1. Huyu hatakuba
2. Utapunguza dau litafika 50
3. Utapunguza tena tu 20
4. Utafika 10
5. Utaanza kuaidi kutoa 10
Hadi 100000
Ila hutaolewa hata uahidi kumpa mshahara wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko ndani kuna makinikia?ili nimtafutie swahiba watasha wa kununua kabisa.
 
Kuna mtanashati ameonesha nia kutaka kunioa. Nami nikaona niwe muwazi kwake mapema isije ikazua balaa siku za usoni.

Nimefunguka kinaga ubaga kuwa mwanamke mazingira, mwanamke matunzo. Nikaenda mbali zaidi kwa kumpa usemi usemao "ukiona mbwa anakonda lawama zinaenda kwa mwenye mbwa". Na mm sitaki kuchakaa nitakapo olewa.

Basi nikamuambia ili kuhakikisha naendelea kupendeza nitataka uwe unanipa pesa kwa ajili ya matumizi yangu ya dharura isiyopungua laki. Hii pesa pamoja na mshahara wangu usiiihesabie kwenye matumizi yoyote ya nyumbani wala usiichukulie kama ndiyo hela ya matunzo yangu. Hii ni kama pocket money tu. Ili mtoto wa watu niendelee kuchanua na nisichake kwa stress.

Ndiyo. Huko ndiyo kuolewa, mwanaume si ni kichwa cha nyumba!??Siyo niolewe halafu bado niendelee kuishi kwa kuiwazia hela ya kula, kodi, kuvaa, kunywa,n.k. Hela ya kuendesha maisha ya familia inatafutwa na mwanaume mm si nimeolewa bhana.!?Mshahara wangu ni kwa ajili ya mambo yangu. Kazi yangu kubwa ni kuzaa tu. Ndiyo maana nchi za kiarabu huko mwanamke akibeba mimba mumewe inabidi alipe hela nyingi sana kama asante kwa mkewe. Na bado wanawake wengi ktk nchi hizo siyo tu kwamba hawaendi maofisini, bali hata sokoni hawaendi.

Nimempa hilo sharti, akiliona analiweza poa, akishindwa basi ajue siyo fungu lake.

ONYO; Wanaume bebeni jukumu la kulea familia, msioe kwa kuangalia mishahara ya wake zenu. Wanawake wanapaswa kutunzwa. Mishahara yao ipo kama ziada kwa matumizi yao binafsi.

Safi sana
 
nisimpe mchepuko wangu nikugee wee niliyekuweka ndani......karoge tena
 
Back
Top Bottom