Nimetuma Sticker ya Ngono kwenye Group la Kanisa

Nimetuma Sticker ya Ngono kwenye Group la Kanisa

Furaha yangu imezimwa ghafla baada ya kutuma kwa bahati mbaya sticker ya ngono kwenye kundi la kanisa la Whatsapp. Mara baada ya kushtuka nikafuta kwa bahati mbaya sijafuta kwa wote, nilichagua option ya "Delete" badala ya "Delete for All".

Waumini wamenishambulia, nimeona nileft.

Sijui naanzaje kwenda kanisani, naombeni msaada nifanye nini? Heshima yangu jamani...
Heshima gani hapo sasa?wakati ndio mambo yako ya sirini,Mungu ameamua kukufunua maovu yako uyaache husikii

Na utalimia meno mwaka huu 😊🤣🤣🤣
 
Ujue siku yakiwakuta mtajua uzito wake, wengine tuna majukumu tumepewa sasa watu walikuwa wanajua wewe ni kioo halafu wanakutana na picha kama hii lazima wajiulize mara 2.
Kwa hiyo unaogopa watu siyo Mungu.
Yale yale ya Nandy, alinisgangaza video ilipovuja akasema alikuwa anawaza waumini na mchungaji watasemaje.
Nikawaza kumbe dhambi halalu ili mradi wenzako wasjue. Kumbe si kwamba watu wanamwogopa Mungu, bali wanataka waonekane wasaf mbele ya jamii
 
Ujue siku yakiwakuta mtajua uzito wake, wengine tuna majukumu tumepewa sasa watu walikuwa wanajua wewe ni kioo halafu wanakutana na picha kama hii lazima wajiulize mara 2.
Tuma hiyo picha hapa...hata kwa kuificha ficha ili tuone tatizo ukubwa wake
 
Kuna msemo unasema
"Mpe mtu mask akuonyeshe sura yake halisi"
Maana yake watu wengi nyuma ya pazia ni watu wabaya sana Ila kwenye macho ya watu wanajidai wema.

Kwahiyo unafiki wa kuvaa ngozi ya wema ulio nao wewe ndo unafiki huohuo walio nao hao wanaokushambulia usikute simu zao zimejaa video za ngono
 
Back
Top Bottom