Nimetumiwa mzigo kutoka Uingereza kuja Afrika Mashariki

Joined
Jan 26, 2019
Posts
87
Reaction score
113
Habari za wakati huu wapendwa,

Wana Jukwaa, naomba ufafanuzi. Kuna mtu amekutumia zawadi ya iPhone, laptop, na pesa taslimu $1500. Naomba msaada kwa wale wazoefu, maana mzigo ulitumwa jana usiku na umefika Kenya katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi.

Naomba msaada kutoka kwa wale wenye uzoefu, ni kweli au ni uwongo? Sijui kama ni matapeli au la. Mzigo umewasili asubuhi ya leo na wameniambia niulete Tabora, lakini wameniambia kuna gharama ya kusafirisha ya Tsh 70,000 kuja Tanzania.

 
Eeh watu wanatumia akili kweli kupata pesa kwa kutapeli watu kuliko kutumia akili kujiongezea thamani..
 
Wafungue wagawe hizo dola wajilipe.
 
Hii kitu ni kweli kabisa tuma pesa chap upate mzigo wako. Then ulete mrejesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…