Nimeumia sana hii mechi yetu na Morocco, nimeumia sana na timu yetu ya taifa

Nimeumia sana hii mechi yetu na Morocco, nimeumia sana na timu yetu ya taifa

Yaani mimi niumie sisiem star kufungwa ebo
 
Kifupi Refa alikuwa upande wa Morroco, mechi nimeifuatilia kwa karibu sana
Refa alikuwa anawabeba sana Morroco
N.B; Mimi sio shabiki wa Soka ila huwa napenda kufuatilia inapocheza timu ya Taifa au zinapokutana Simba na Yanga ila kiuhalisia sina timu
 
Tena mim nafikiri tatu chache ilitakiwa watu wagongwe week na siku mbili.
 
Ndugu iliwauma. Mimi sijaongelea uchambuzi miminimeumia matamanio. Why not a win.haswa kwa sisis wenye mapenzi. Sijaongelea historia hapa
Basi Matamanio yako yako juu sana. Morocco kwa viwango ipo juu sana kulinganisha na Tanzania. Tushukuru hawakutupiga tano!
 
ni mgonjwa tu wa akili ( maniac ) pekee ndiyo alikuwa akidhani na akiwa na uhakika wa 100%. kuwa taifa stars ccm samia serikali fc leo ingeshinda na kuwafunga wenye akili, mipango, uwezo na malengo morocco
Nakazia ni mgonjwa wa akili tu ndie angeweza kuamini taifa stars wangeshinda. Wale morocco hata wangekuwa 9 uwanjani bado tusingeweza kuwafunga.
 
Kila nikilalaa naamka na ndoto za kufungwa, nimelala usingizi mubaya muno.
 
Kama kuna mtu alitegemea tutashinda hii mechi bc hana akili huyo mtu, na tutafungwa mechi zote mbili zilizobakia
 
Hamna mechi katika maisha yangu imeniuma kama hii Tanzania na Morocco.

Kweli Tanzania sisi wakupigwa goli Tatu. Kwamba sisi tuko level ya chini hivi. Sawa timu huwa zinafungwa. Kweli vijana wetu wameenda kutuwakilisha mechi ya kwanza wanapigwa tatu.

Mbona walituadaa mioyo yetu vizuri. Sisi kweli wakulalamika muda huu. Serious. Kauli za kocha ziliniumiza sana kabla ya mechi.

Je, kweli hiki ndicho tunapewa zawadi sisi au mimi mtanzania. Why?

Kweli tumepigwa hii mechi. Nimeumia sana. Hivi brazil ikienda kucheza huwa si inawaza nchini kwake wabrazil wenzao, au pale germany, au london uingereza si huwa wanajua wameenda wakilishwa. Serious Timu ya taifa ya kutuumiza kila siku😪😪😪😪.

I am very disappointed, sijui ni mm tu nimeumia hvi. Aaanh
Aah ndugu, Kuumia, kukasirika, kustuka nk ni zao la tukio usilotegemea au moyo wako haukujitayarisha kabisa kupokea hilo; sasa kipigo cha Stars kutoka kwa Morocco hukukitegemea? Hivi tuwe serious tujiulize kupitia mfano huu: Mbwa kumuuma binadamu na binadamu kumuuma mbwa, hapo habari itakayokimbiliwa na watu ni ipi? Sasa tuje ya kwetu: Stars kumfunga Morocco na Moroco kumfunga Stars ipi ingekuwa habari ya kustua? Ndugu, nakuhurumia, usije ukajisababishia BP, Stress, Depression na kukosa raha bila sababu yoyote ya msingi! Sisi tuendelee kukifunza kwa wenzetu ktk uwekezaji na kuacha siasa na upendeleo kwenye ligi zetu huku kwetu!
Kuumia, kustuka, kukasirika
 
Kucheza AFCON ni mafanikio tosha , ilipaswa kushukuru hapo huku(kucheza AFCON )wala hatutoboi , kufika huku tu ni mafanikio kwetu

Ukilielewa hilo hutaumia, sisi bado wachanga huwezi kuzaliwa na ukaanza kutembea hapo hapo
 
Unaumia nini. Kwani ulikuwa unatgemea matokeo tofauti ya staz Kizimkazi na haya? Staz kushinda mechi huko Afcon labda tume ya taifa ya uchaguzi ikaibe magoli badala ya kura
 
Tumetaabikaa tumesulubikaaa jamani sisi tumepigikaaa aaa sisi tumepigikaaa

Tatu bila tatu bilaaa by j nature

Pole mkuu
[emoji23][emoji23]

Wew si mzalendo kwakwel

Mwamba kahuzunika unamshushia na ngoma kuongeza maumivu kweli!

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Ile redcard ya Miroshi ndo ilitumaliza... vijana walikuwa wameanza ku recover na kuzoea mchezo....
 
Back
Top Bottom