Kilichotokea Libya
Kilichotokea Misri
Kilichotokea Tunisia
Kilichotokea Sudan
Ilikuwa ni watu kutoka Magharibi kuja kupandikiza watu wao ili itokee insurgency na wao wapate nafasi ya kuingia kwenye Hilo Taifa wakisema wanaenda kutoa humanitarian aid kumbe wakamwaga siraha na kubadilisha regime hii ndio inaitwa false flag siku hizi
Kwa nini Misri baada ya Arab spring na kiongozi wakamchagua kwa demokrasia wa Muslim brotherhood akatofautiano kimawazo na wamagharibi wakafanya mpango akapinduliwa na Jeshi na General Al sis.
kuingia uliona kama Mataifa ya Magharibi yalikemea kuhusiana na undemocratic nature iliyotokea ila walizidi kuipa msaada Misri kwa sababu kwao inaserve strategic mission zao na intereste. funguka macho mtu mweusi jua mizania isiyo sawa watumiayo mabeberu.
Mnafamu nini kilichoendelea Sudan, Kilichoendelea Lebanon
Baada ya hapo Mashiriki ya kijasusi duniani yakajua Kilichoendelea hivyo
walivyotaka kuingia Syria kwa kutumia mbinu zile zile wakazuiliwa na mrusi
Tena hapa Syria wakasema hadi civilian s wamepigwa na chemical weapons kumbe walifanya wao kupitia WHITE HELMETS.
Wakaenda Hong Kong kwa pre text ya uhuru wa habari na kujieleza
Uliona jinsi wachina walivyolishughurikia.
Wakadai Hong Kong haipo huru juu ya sheria mpya ya Ulinzi sijui Usalama ya mtu kupelekwa Mainland ukikosea kumbe Wamagharibi walipatumia Hong Kong kama sehemu ya kufanya na kuendeleza covert operation dhidi ya china.
Wakaenda Belarus wakidai Kuna rigged election results uliona walivyohandle
Wakaenda Kazakhstan hii juzi juzi tu uliona CSTO ikiongozwa na Mrusi walivyodhibiti Yale machafuko kupitia nguvu yaani aim to kill,
Wamagharibi walivyoona mbinu Yao imeshindikana wakaanza kusema Urusi wamevamia Kazakhstan na Warusi waliingia hawatoki lakini walivyomaliza walitoka kwa amani
Lazima ujue hawa jamaa Wana mbinu nyingi na Wana operate kutumia hizi NG'Os to impose their idea na Kuna watu wanalipwa fedha nyingi kuinstigate hayo mambo.
Kwa hiyo usiseme mhemko jamaa ana hoja.
Naomba kuwasilisha.
Unaona unavyoweweseka na kupachika pachika matukio yasiyohusiana ilikupata mutililiko wa hoja zako zisizo.
unaposema baada ya Arab spring wamisri walichaguo kiongozi kutoka Muslimbrotherhood unakuwa unamaanisha nini?.
kuna tofauti gani na mtu kusema:, baada ya Serikali ya Samia kumfunga mwenyekiti wa chadema {Mbowe} wanachedema wakachagua kiongozi mwingine toka chedama,hii ina sound logic kweli?.
Muslim brotherhood ni chama chenye nguvu Misri kule hakuna Christian brotherhood, hindu brotherhood, ama athest brotherhood hata useme WESTERNERS walitaka kuweka kiongozi toka kwenye hivyo vyama ilikufanikisha ajenda zao.
arab spring haina uhusino na unachokieleza hapa.
Chief, elewa kuwa propaganda zinatumika kila upande.
mfano ni hapa hapa bongo kuna watu wana amini kuwa Nyerere alitumwa na Kanisa katoliki kwenda kumg'oa Iddy Amini kwasababu alikuwa ni muislam na watu hao uwezi badili mtazamo wao.
sasa wewe Endelea kuamini kuwa kila wananchi wa nchi fulan wakitaka mabadiliko watakuwa wamepandikizwa na Westerners kufanya hivyo.
yaan full ujinga ujinga fulan wa Kulaum wengine. Hong Kong ni kama zanzibar akina Sheikh Farid walikuwa wanapigania zanzibar yao iwe huru, bilashaka hao nao kuna watu wanasema ni pandikizi la Westerners.
Pathetic