Nimeuziwa gari la urithi bila kuelewa, najinasuaje huu msala

Kwa kadi ambayo haina jina langu?

Hana cha kusema yeye anadai maza wake alimpa lote lote ndo maana hata kadi alikuwa nayo so anashangaa maza imekuwaje anakua hivi, ila saa hizi huyo dogo hapatikani kabisa.
Wewe neenda police ufungue kesi kwamba maza kafisha mtuhumiwa alio ni tapeli, wa uzie kesi hiyo, maza atamtafuta mwanae au yeye awekwe ndani kuficha muhalifu......hiyo issue inaisha asubhi tu.
 
AISEE POLE SANA ILA MIMI NAKUSHAURI UTAFUTE WAKILI NA KAMA SLIP ZA MANUNNUZI UNAZO BADO ZITAKUSAIDIA ILA SIKU NYINGINE USINUNUE GARI YA MKONONI BILA KUJIRIDHISHA NAKALA MUHIMI ZA GARI HUSIKA NI BORA UAGIZE GARI JAPAN KULIKO KUNUNUA MKONONI
 
Mkuu umenikunbusha mwaka 2015 nilitaka kununua gari kwa dada moja. Nilifika na fundi wangu dada akatupa gari tulitest na kweli tulizunguka nalo kwenye barabara mbovu zote za mkoa husika gari ilikuwa mpya balaaa. Tukakubaliana bei hapohapo nikamuuliza swali kadi ya gari ina jina lako? Akasema kadi ya gari haina jina Lake bali ina jina la rafiki yake (mwanaume) aliyemnunulia kama zawadi siku ya harusi yake. Nikamwambia kwa kuwa tumekubaliana bei sasa mwite mwenye jina Lake tufanye mauziano mbele ya mwanasheria. Dada akasema yeye hawezi kufanya kazi hiyo kama nataka gari nitoe hela nipewe na kadi hivohivo. Tulitoka nduki fasta na fundi wangu.
 
Hapo mkuu kama una kadi og na mkataba wa mauziano japo swala linakuja aliyekuuzia sio mmiliki ya hiyo gari...
Ongea na maza busara itumike
Akifuata ushauri huu unaweza kumsaidia,binafsi sioni cha kumsaidia zaidi ya busara na kujishusha kwa huyo mazeri
 
Nenda polisi fungua jalada la uchunguzi kuhusu wizi wa kuaminiwa.

Hao wamekuibia wala hakuna mirathi hapo
 
Kuna maswala fulani nimeyaona. 1. Kwamba ulinunua gari bila kuchukua kadi.
2. Uliuziwa na mtu asiye mmiliki wa gari.
3. Hukuwahi kubadili umili wa gari kwa kubadili kadi kuwa jina lako.
Majibu yangu ni kuwa.
1. Bado huna uhalali wa hilo gari ingawa sio mwizi. Maadamu kuna ule mkataba wa mauziano hakuna wizi. Ila kuna utapeli. Wewe umetapeliwa.
2. Kisheria gari ni kadi. Kwa hiyo kitendo cha kutochukua kadi ulifanya kosa binafsi kubwa tu. Kwa matiki hiyo pamoja na kutoa hela na wewe kuwa nalo bado sio mmiliki wa gari hilo.
3. Namba 2 inaendana kuwa kuendesha gari na kuwa nalo kwa maana ya kulinunua bila kubadili umiliki ni kosa kisheria. TRA.
4. Kitakachofanyika watakuja kukunyanganya gari ili wewe umdai hela zako aliyekuuzia gari.
5. Kitakachokuokoa ni pale uliposema aliyekuuzia ni mtoto wa mwenye gari na mama akawa shahidi. Hapo patakuokoa.
 
Kwa lugha nyepesi nimpe mama gari lake afu nifungue kesi sio?
 
Kwa lugha nyepesi nimpe mama gari lake afu nifungue kesi sio?
Hapana. Lazima ujitetee. Usijiue waziwazi. Polisi aliyekushauri anaona suala kijinai jina.
Umesema mtoto alikuuzia, mama akawa shahidi kama sikosei. Halafu mama huyo huyo anadai gari. Huo ni utapeli.
Ningekuwa mimi. Ningemwambia mama aniandikie maandishi kulitaka hilo gari. Baada ya kuyapokea ningetengeneza affidavit na kuwafungulia kesi kudai kadi ya gari, pia ningesema wakati nadai kadi ndio nageukwa na watu wale wale walioniuzia kuwa gari ni ya urithi kitu ambacho hukujua. Ninheweka na blaa blaa kuwa hukujua kama mmiliki alishafariki.
 
Soma tena mtoto aliniuzia ila mama hakuwepo, mama alikua shahidi wakati mume wake(ambaye ni marehemu) ananunua gari, mama aliidhinishwa kama msimamizi wa mirathi ikiwemo gari na dogo aliachiwa tu alitumie na sio kuliuza.
 
Soma tena mtoto aliniuzia ila mama hakuwepo, mama alikua shahidi wakati mume wake(ambaye ni marehemu) ananunua gari, mama aliidhinishwa kama msimamizi wa mirathi ikiwemo gari na dogo aliachiwa tu alitumie na sio kuliuza.
Kwa vyovyote itakavyokuwa, hii case kuna uwezekano mkubwa wa fedha kukutoka. Hata kama haki iko upande wako, lakini utahitajika kutumia fedha ili polisi ''wakuelewe''. Kosa ulilofanya ni kukubali kuuziwa gari bila kadi halisi. Mtafute dogo aliyekuuzia, tumia fedha, awekwe ndani kwa kesi ya utapeli, uone mama yake ata-react namna gani.
 
We ndo umeongea point
 
Mambo mengine yanashangaza yaani shahidi amegeuka nakudai ndio msimamizi wa miradhi baada ya mauzo, hapo mi naona hao wote ni matapeli tu, hapo mdake huyo dogo na huyo maza wakurudishie pesa yako au wapeke polisi , hao watakuwa wamezulumiana huko hivyo maza ameamua kuharibu mpango , inawezekana dogo amemzidi kete maza,
 
Nafikiri option ya pili ni nzuri, wewe nenda kafungue kesi ya utapeli ili upewe RB ya kumtafuta huyo tapeli (mtoto wa huyo mama). Kama ni mwanae wa kumzaa kabisa basi mtalimaliza tu, vinginevyo mwanae atazeekea jela+fine.
 
Mi nahisi aliyekuuzia na mpiga simu,wote lao moja
 
Kwa kadi ambayo haina jina langu?

Hana cha kusema yeye anadai maza wake alimpa lote lote ndo maana hata kadi alikuwa nayo so anashangaa maza imekuwaje anakua hivi, ila saa hizi huyo dogo hapatikani kabisa.
Mkataba wa mauziano unao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…