Nimeuziwa mbwa maeneo ya Victoria, nilipomfikisha nyumbani mume wangu akasema eti sio mbwa ni fisi

Nimeuziwa mbwa maeneo ya Victoria, nilipomfikisha nyumbani mume wangu akasema eti sio mbwa ni fisi

View attachment 2413649
Jana jioni nilipokuwa nikitoka kazini, nikafika Victoria, nikakuta kuna jamaa ana mbwa watatu, wawili wakubwa na puppy mmoja.

Nikavutiwa na puppy nikaenda naye nyumbani. Mume wangu alirudi akiwa amechoka na amepiga mambo yake, lakini nilimjulisha kuwa nimenunua mbwa.

Asubuhi ya leo akaenda kumwangalia, nilikuwa nimemuweka garage sababu bado hatujapata kibanda chake. Nikashangaa mtu ananiita kwa hasira ananizodoa kuwa sina akili kabisa, nimeletaje fisi nyumbani?

Kwa kweli mimi wakati namnunua nilifurahia umbo lake alivyonona, sikujua fisi kuwa wako kama mbwa. Lakini pia nadhani nilirogwa.

Japo haina kahawa lakini huyo kweli ni fisi....[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tulia nae tu fisi ukimdometicate yuko poa kuliko mbwa ! Just last week nilikuwa na jadili na wife kufuga fisi as a pet akikubali tuta fanya business utamleta zenji akikataa tutafanya swaping wewe na fisi mtakuja zenji wife na paka atakuja kwenu -joke
Heeeee😳
 
Kama sio chai ya strungi basi fuga hiyo makitu itakusaidia mbeleni maana una nyota ya kichawi au umerithi jina la marehemu bibi yako sasa mizimu imeamua kukupa mikoba bila weye kujua.
Fuga hilo dubwasha litakusaidia kuwa linaenda kuiba mifugo kama mbuzi na kuku kwa majirani
Jemima ni Biblical name, she was Job's daughter.
 
View attachment 2414024
Jana jioni nilipokuwa nikitoka kazini, nikafika Victoria, nikakuta kuna jamaa ana mbwa watatu, wawili wakubwa na puppy mmoja.

Nikavutiwa na puppy nikaenda naye nyumbani. Mume wangu alirudi akiwa amechoka na amepiga mambo yake, lakini nilimjulisha kuwa nimenunua mbwa.

Asubuhi ya leo akaenda kumwangalia, nilikuwa nimemuweka garage sababu bado hatujapata kibanda chake. Nikashangaa mtu ananiita kwa hasira ananizodoa kuwa sina akili kabisa, nimeletaje fisi nyumbani?

Kwa kweli mimi wakati namnunua nilifurahia umbo lake alivyonona, sikujua fisi kuwa wako kama mbwa. Lakini pia nadhani nilirogwa.
Simulizi yako hii mtu akisoma lazima acheke sana tu.

Fisi na mbwa ingawa ni familia moja lakini wana tofauti kubwa ya kimaumbile pamoja na sura!

Ndiyo maana mr akakuzodoa kwamba hauna akili.

Na aliyekuuzia naye ni mwamba kweli kweli, kuhodhi fisi na ukamtuliza na kuwaweka pamoja na mbwa wakaelewana si kazi ya kitoto.

Fisi ni kama kwale, kiasili hafugiki, ni viumbe wa porini, wajanja na hawataki mazoea.
 
Nchi ina mijitu ya ovyo iliyotoka usingizini kiasi kwamba ikipewa chai inaamini ni kahawa...
Ungesema fox au wolf sawa ila fisi ni kuchangamsha tu genge.. Hell noh
 
Back
Top Bottom