Nimeuziwa mbwa maeneo ya Victoria, nilipomfikisha nyumbani mume wangu akasema eti sio mbwa ni fisi

Nimecheka mpk basi,huyo jamaa sio mpenzi wa mbwa,anawaza arudi kapiga masanga puppy akaondoka na mbupu zake.
 
Jana jioni nilipokuwa nikitoka kazini, nikafika Victoria, nikakuta kuna jamaa ana mbwa watatu, wawili wakubwa na puppy mmoja.

Nikavutiwa na puppy nikaenda naye nyumbani. Mume wangu alirudi akiwa amechoka na amepiga mambo yake, lakini nilimjulisha kuwa nimenunua mbwa.

Asubuhi ya leo akaenda kumwangalia, nilikuwa nimemuweka garage sababu bado hatujapata kibanda chake. Nikashangaa mtu ananiita kwa hasira ananizodoa kuwa sina akili kabisa, nimeletaje fisi nyumbani?

Kwa kweli mimi wakati namnunua nilifurahia umbo lake alivyonona, sikujua fisi kuwa wako kama mbwa. Lakini pia nadhani nilirogwa.
Hayo masikio kama bakuli mbwa hana.
 
Wasiwasi upo kwenye picha uliyotuwekea. Huyo fisi anaonekana akiwa porini na si katika gereji kama unavyotaka tuamini. Rudi kapige picha ukiwa umempakata kwani puppy huwa wapole ndo maana uliweza kwenda naye hadi nyumbani kwako pasipo kupata madhara yeyote. Kule kwetu Usukumani tunawatunza vizuri tu, ila hakikisha una nyama ya kutosha kama chakula chake.
 
Back
Top Bottom