round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 345
- 1,145
Nikikumbuka maisha niliyowahi kuyaishi siwezi kuja kumuombea hata adui umasikini, Ni hali inayoaibisha, kukunyanyasa, kushusha heshima, kukutesa, n.k.
- Nimevaa sana mitumba ya kurusha, kiatu unaenda kutafuta lisaa zima uone chenye nafuu
- Simu imepasuka kioo miaka miwili sina pesa ya kubadili kioo
- Kuna muda unatembea ili ubane nauli
- Ombea usiumwe, shughuli inaanza unafika hospitalini huna Bima na mifuko imetoboka, ndio hapo unaanza kutafuta mizizi na mitishamba maporini
- Nilipokuwaga mdogo nilikuwa nashangaa mtu anafikaje 30 hana nyumba wala gari, Nilitubu !!
- Mapenzi ya kudumu yalikuwa kitendawili, ukiwaza wajibu wako kama mwanaume utamlishaje na utamtunzaje nguvu zinakuisha, commitment inapungua.