Nikikumbuka maisha niliyowahi kuyaishi siwezi kuja kumuombea hata adui umasikini, Ni hali inayoaibisha, kukunyanyasa, kushusha heshima, kukutesa, n.k.
- Nimevaa sana mitumba ya kurusha, kiatu unaenda kutafuta lisaa zima uone chenye nafuu
- Simu imepasuka kioo miaka miwili sina pesa ya kubadili kioo
- Kuna muda unatembea ili ubane nauli
- Ombea usiumwe, shughuli inaanza unafika hospitalini huna Bima na mifuko imetoboka, ndio hapo unaanza kutafuta mizizi na mitishamba maporini
- Mapenzi ya kudumu yalikuwa kitendawili, Mwanamke unakuta anakupenda ila hata kumpa pesa ya vizawadi au matunzo huna, sizungumzii zile level za kuhonga / vizinga bali kutimiza wajibu as a man, hata mahari ya laki 4 huna.