Nimevaa sana mitumba ya kurusha, kutumia simu kioo kimepasuka miaka miwili, kutembea kubana nauli, niliyaogopa mapenzi, n.k, Umasikini ulaaniwe

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145
Nikikumbuka maisha niliyowahi kuyaishi siwezi kuja kumuombea hata adui umasikini, Ni hali inayoaibisha, kukunyanyasa, kushusha heshima, kukutesa, n.k.

  • Nimevaa sana mitumba ya kurusha, kiatu unaenda kutafuta lisaa zima uone chenye nafuu
  • Simu imepasuka kioo miaka miwili sina pesa ya kubadili kioo
  • Kuna muda unatembea ili ubane nauli
  • Ombea usiumwe, shughuli inaanza unafika hospitalini huna Bima na mifuko imetoboka, ndio hapo unaanza kutafuta mizizi na mitishamba maporini
  • Nilipokuwaga mdogo nilikuwa nashangaa mtu anafikaje 30 hana nyumba wala gari, Nilitubu !!
  • Mapenzi ya kudumu yalikuwa kitendawili, ukiwaza wajibu wako kama mwanaume utamlishaje na utamtunzaje nguvu zinakuisha, commitment inapungua.
 
Dogo,
Tumia pesa ikuzoee iwe inakutembelea
 
mleta mada wala usiwe na wasiwasi maana wengi wetu ni sawa na wewe, tena ogopa sana sisi tukio kwenye mitandao ya kijamii, wengi wetu miguuni mwetu tume vaa yebo yebo , wengine hata hazujui tutakula nini jioni ya leo.


kwa kweli umaskini ni mbaya mno, vita yake kuishinda ni ngumu mno. kama ni laana basi moja ya laana mbaya kuwepo duniani ni umaskini.
 
Umaskini ni laana na fedheha
 

kiongozi tulia kwanza ueleze kwa utuo imekuwaje uko? umepatwa na nini? maana naona unatoa siri za kambi. kwanza unataka kwenda wapi au umeshinda bet?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…