Nimevunja kibubu muda huu, siamini nilichokikuta ndani

Nimevunja kibubu muda huu, siamini nilichokikuta ndani

Masharti ya kumiliki kibubu
1. Unapaswa kukiloweka kwenye maji ya chumvi walau kwa masaa 24 kabla ya kukitumia ( hii itasaidia sana kuua uchawi wote uliofanyika

2. Usichanganye sarafu na noti kwa muda mrefu (hiyo ni gateaway nzuri sana kuibiwa kichawi)

3. Kwa kila noti utakayoweka hakikisha unaondoa kishungi cha pembe moja( wachawi hawachukui kitu chenye kasoro)

4. Kila sarafu utakayoweka hakikisha unaijeruhi kwa kuigonga na nyundo ukingoni kwenye mviringo

5. Kibubu hakiwekwi kwenye pembe (huo ni mlango wa wachawi na wanga

6. Si kila pesa ni ya kuweka kwenye kibubu.. Hasa ile iliyotoka direct mfukoni mwa mtu mfano chenchi ya boda boda, konda au tax driver na wauza magenge nknk ( hawa ni chumaulete wakubwa lakini nao pesa zao wanezifanyia featuring ili kuzilinda)

7. Kibubu hakiwekwi mahali kikagusana moja kwa moja na sakafu ama ardhi.. Ardhi zimebeba mengi

Pesa unayoweka kwenye kibubu ni mabaki toka mikono tofauti, hayo ni maroho unayaweka pamoja...lazima zipigwe na mshindwa akimbie.. Na kuna pesa sio zako wewe ni mpagazi tuu, hata ukiiweka kwenye kibubu lazima itembee
Ulimwengu wa utunzaji pesa ni deep ni mgumu na una mengi ndani yake.. Ni lazima kwa namna yoyote ile uhusishe nguvu za kiroho hasi au chabya ndio maana kwenye nyumba za ibada zile zaka huombewa
 
Nimejikuta natamani niwe na chuma ulete pia, nitaipata wapi?
Masharti ya kumiliki kibubu
1. Unapaswa kukiloweka kwenye maji ya chumvi walau kwa masaa 24 kabla ya kukitumia ( hii itasaidia sana kuua uchawi wote uliofanyika

2. Usichanganye sarafu na noti kwa muda mrefu (hiyo ni gateaway nzuri sana kuibiwa kichawi)

3. Kwa kila noti utakayoweka hakikisha unaondoa kishungi cha pembe moja( wachawi hawachukui kitu chenye kasoro)

4. Kila sarafu utakayoweka hakikisha ua nyundo ukingoni kwenye mviringo

5. Kibubu hakiwekwi kwenye pembe (huo ni mlango wa wachawi na wanga

6. Si kila pesa ni ya kuweka kwenye kibubu.. Hasa ile iliyotoka direct mfukoni mwa mtu mfano chenchi ya boda boda, konda au tax driver na wauza magenge nknk ( hawa ni chumaulete wakubwa lakini nao pesa zao wanezifanyia featuring ili kuzilinda)

7. Kibubu hakiwekwi mahali kikagusana moja kwa moja na sakafu ama ardhi.. Ardhi zimebeba mengi

Pesa unayoweka kwenye kibubu ni mabaki to
 
Daah,wife yeye alinunua kibubu cha chuma kabisa Yaani..rkn alichokikuta baada ya kukivunja aliishia kutoa machozi Yaani hana hamu na vibubu.
Mimi nashukuru nimekivunja mapema hata sijaumia kiasi hicho!
 
Dah, yaani hapa wakuu natamani kucheka wakati ni jambo la hovyo limetokea
Siku ya tarehe 3 mwezi huu, ni juzi tu hapo niliamua kununua kibubu na nikaanza kuweka visenti vyangu ninavyopata kazini, kazini nalipwa kwa kila siku, nikaona hela nayolipwa kwa siku ni nyingi na nikajiapiza kuwa nitakuwa nakula walau robo ya kipato na nyingine nitadumbukiza kwenye kibubu.

Kwakuwa ilikuwa tayari ni usiku na nimeshatumia hela niliyolipwa siku hiyo, nikaamua kukizindua kibubu changu kwa kuweka vijisenti vilivyobaki kwenye matumizi, nikaweka 3,400/=
Tarehe 4. 7,000/=
Tarehe 5. 12,000/=
Tarehe 6. 10,000/=
Tarehe 7 nikaweka chenchi chenchi kama za elfu 3.
Tarehe 8 nikaweka 20,000/=
Sasa kwakuwa huwa nasikia stori nyingi kuhusu vibubu, ikabidi nifanye ziara ya kushtukiza kwenye kibubu changu, nikivunje kibubu nione hesabu zangu kama ziko sawa au vipi,


Haha! kama mchezo wa kuigiza tu wakuu, yaani Hapa nimekuta 23,000 mpaka siamini nachokiona.
Chenchi zote zipo, kasoro zile noti tu.

Mlaaniwe wauza vibubu
Wewe ni muongo simple like that....
 
Wakuu kama kuna mtu haamini hii kitu, anunue kibubu (huenda vibubu vingine havina chuma ulete, sielewi katika hili) aweke hata buku kila siku (kwa walau siku kumi)
And then avunje aje atupe mrejesho!
Mimi naweka vibubu huu mwaka wa tatu na hamna shida kabisa
 
Mkuu mimi naishi peke yangu, na hapa hakuna mtu yeyote ambaye ana mazoea hata ya kuja kunitembelea,
isitoshe kibubu chenyewe nimekinunua juzi hapo tarehe 3 mwezi huu.
Kwahiyo kusema eti kuna mtu amekuja na kuzichukua ni uongo na kwakweli haiwezekani'
Vibubu vinakuwa Equipped toka manufactured date
 
Hivyo vibubu mara nyingi vimewashwa Bluetooth,ukiweka tu salio limekwenda,niliwahi shuhudia ndoa ya jirani yangu ikivunjika kwa sababu ya kibubu,mke kila siku anaweka 5000 kwnyw kibubu akitarajia baada miezi mitatu atakuwa na pesa ya kutosha ila mwisho wa siku akakukuta kibubu kina elfu30, fikiria mziki wake.
 
Nimejaribu njia nyingi hazikunipa uwezo wa kuhifadhi fedha nyingi maana ilikuwa rahisi kuzitumia nikipatwa na jambo. Lakini baada ya kununua hisa za UTT AMIS. Nimeweza kuweka fedha ya kutosha. Nikianza na asilimia kumi ya kila malipo ninayopata. Na fedha yoyote ninayoipata iliyo nje ya bajeti ya mwezi. Mwanzoni ni ngumu lakini ukizoea unaweza.
 
Back
Top Bottom