Nimevunja kibubu muda huu, siamini nilichokikuta ndani

Masharti ya kumiliki kibubu
1. Unapaswa kukiloweka kwenye maji ya chumvi walau kwa masaa 24 kabla ya kukitumia ( hii itasaidia sana kuua uchawi wote uliofanyika

2. Usichanganye sarafu na noti kwa muda mrefu (hiyo ni gateaway nzuri sana kuibiwa kichawi)

3. Kwa kila noti utakayoweka hakikisha unaondoa kishungi cha pembe moja( wachawi hawachukui kitu chenye kasoro)

4. Kila sarafu utakayoweka hakikisha unaijeruhi kwa kuigonga na nyundo ukingoni kwenye mviringo

5. Kibubu hakiwekwi kwenye pembe (huo ni mlango wa wachawi na wanga

6. Si kila pesa ni ya kuweka kwenye kibubu.. Hasa ile iliyotoka direct mfukoni mwa mtu mfano chenchi ya boda boda, konda au tax driver na wauza magenge nknk ( hawa ni chumaulete wakubwa lakini nao pesa zao wanezifanyia featuring ili kuzilinda)

7. Kibubu hakiwekwi mahali kikagusana moja kwa moja na sakafu ama ardhi.. Ardhi zimebeba mengi

Pesa unayoweka kwenye kibubu ni mabaki toka mikono tofauti, hayo ni maroho unayaweka pamoja...lazima zipigwe na mshindwa akimbie.. Na kuna pesa sio zako wewe ni mpagazi tuu, hata ukiiweka kwenye kibubu lazima itembee
Ulimwengu wa utunzaji pesa ni deep ni mgumu na una mengi ndani yake.. Ni lazima kwa namna yoyote ile uhusishe nguvu za kiroho hasi au chabya ndio maana kwenye nyumba za ibada zile zaka huombewa
 
Nimejikuta natamani niwe na chuma ulete pia, nitaipata wapi?
 
Daah,wife yeye alinunua kibubu cha chuma kabisa Yaani..rkn alichokikuta baada ya kukivunja aliishia kutoa machozi Yaani hana hamu na vibubu.
Mimi nashukuru nimekivunja mapema hata sijaumia kiasi hicho!
 
Wewe ni muongo simple like that....
 
Wakuu kama kuna mtu haamini hii kitu, anunue kibubu (huenda vibubu vingine havina chuma ulete, sielewi katika hili) aweke hata buku kila siku (kwa walau siku kumi)
And then avunje aje atupe mrejesho!
Mimi naweka vibubu huu mwaka wa tatu na hamna shida kabisa
 
Vibubu vinakuwa Equipped toka manufactured date
 
Hivyo vibubu mara nyingi vimewashwa Bluetooth,ukiweka tu salio limekwenda,niliwahi shuhudia ndoa ya jirani yangu ikivunjika kwa sababu ya kibubu,mke kila siku anaweka 5000 kwnyw kibubu akitarajia baada miezi mitatu atakuwa na pesa ya kutosha ila mwisho wa siku akakukuta kibubu kina elfu30, fikiria mziki wake.
 
Nimejaribu njia nyingi hazikunipa uwezo wa kuhifadhi fedha nyingi maana ilikuwa rahisi kuzitumia nikipatwa na jambo. Lakini baada ya kununua hisa za UTT AMIS. Nimeweza kuweka fedha ya kutosha. Nikianza na asilimia kumi ya kila malipo ninayopata. Na fedha yoyote ninayoipata iliyo nje ya bajeti ya mwezi. Mwanzoni ni ngumu lakini ukizoea unaweza.
 
Mimi naweka vibubu huu mwaka wa tatu na hamna shida kabisa
Unaishi sehemu gani mkuu uje nikupeleke niliponunua kibubu na wewe ununue, uweke pesa walau kwa wiki moja na baada ya hapo ukivunje tuone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…