Ninachoweza kusema ni hiki hapa.
Nimekuwa shabiki wa mpira wa miguu kwa miaka 45 sasa. Ni mshabiki wa Simba toka nimezaliwa.
Kama mshabiki wa mpira wa miguu, kuna kipindi cha mazao (kuchukua ubingwa) na kipindi cha ukame (kukosa ubingwa). Hii haikuanza miaka ya hivi karibuni.
Kuna kipindi cha miaka ya 80, Simba alichukua ubingwa mara moja tu (kama kumbukumbu yangu iko sawa). Lakini miaka ya 90, alichukua ubingwa mara tatu mfululizo. Young Africans naye kuna kipindi alikuwa na ukame wa ubingwa lakini kuna kipindi akachukua ubingwa mfululizo.
Ninachotaka kusema ni hichi. Kwa miaka ya karibuni, Simba alichukua ubingwa mara nne mfululizo. Nakumbuka Young Africans alikuwa anahangaika na usajili wa wachezaji wengi lakini mwisho wa msimu, Simba anachukua ubingwa. Kila timu inapitia kipindi kigumu. Nakumbuka wapenzi wa Simba tukawa tunawatania sana wapenzi wa Young Africans (maneno ya jengeni timu acheni kulalamika, etc). Ni sehemu ya mchezo. Huwezi kuchukua ubingwa kila msimu (with the exception of Mamelodi Sundowns in South Africa lol!!!).
Nakumbuka zamani nilikuwa naumizwa sana na hili. Lakini kadri ninavyozeeka, ninaangalia katika mtizamo tofauti. Kuna kupanda na kushuka. Kuna wakati una kazi nzuri sana inakupatia kipato mnono na kuna wakati unajiuliza nitapata wapi pesa ya kula. Ni sehemu ya maisha.
Nafikiri ukijiandaa kuangalia katika mtizamo huu (haijali wewe ni mshabiki wa Simba au Yanga), utaweza kuchukulia vitu (whether unapata ubingwa au hapana) vizuri zaidi.
My 2 cents.