Nimewasambaratisha majambazi, usiku, kwa Jina la Yesu!

Nimewasambaratisha majambazi, usiku, kwa Jina la Yesu!

Ninunulie bible
Biblia zinapatikana bure app store au play store
Biblia.jpg
 
Ungetaja tena kwa nguvu "Allah ". Hiyo naona kama chai. Siku hizi jina Yesu linatumiwa kwa biashara.
Jina la Yesu tu ndilo lenye uwezo wa kumfukuza shetani na wasaidizi wake(wachawi, wezi, majambazi...)
Flp 2:9-11
Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.
 
Ndugu zangu, hii ni habari ya kweli kabisa; sio chai! Uongo mimi nauchukia kama ukoma!

Ilikuwa around saa saba usiku, nilikuwa safarini nikiendesha gari langu, kuelekea nyumbani. Barabara ilikuwa tulivu, ila haikuwa na taa za barabarani, hivyo giza lilitanda kila upande wa barabara. Sikujua katika eneo hilo kuna majambazi, hivyo niliendesha tu gari comfortably.

Nilipokaribia kona fulani, kundi la majambazi wapatao watano walijitokeza mbele yangu kwa kushtukiza, wakanifanyia ishara ya kunisimamisha. Ni dhahiri walikuwa na nia ya kufanya uhalifu.

Mita chache kabla ya kuwafikia, kwa sauti ndogo tu, ila ya ujasiri, nilitamka: "Kwa Jina la Yesu, mmeshindwa!"

Loo, aibu yao! Nguvu ya Jina la Yesu iliwagusa hao majambazi, wakatawanyika wote kwa haraka na kunipisha nipite! Si ajabu waliona moto kutoka mbinguni ukiwaijia! Nikapita salama, nikiwa nimejaa shukrani na sifa kwa Mungu aliyenilinda na kunifikisha nyumbani salama. Haleluya!
Mwamposa amewaharibu mmekuwa wajinga.
 
Jf imevamiwa na vichaa
 
Walokole muukoeni huyu mwenzenu, akiwahishwa atapona....
 
Unasemaje bure wakati ili uwe na biblia uwe na simu na bundle
Simu na bando unalotumia kuchangia mada hapa linatosha kudownload app ya Biblia.
 
Mleta mada ulifanya je mpaka ukanunua gari, si wengine tunaamka kabla ya mapambazuko na kulala usiku mwingi lakini hatuna hata baiskeli!
 
Jf imevamiwa na vichaa
Asante kwa kunipandisha cheo. Kumbe na mimi nimefikia level ya Yesu ya kuitwa nimerukwa na akili? Wow! This is great news!
Marko 3:20-30 SRUV
Mkutano wakakusanyika tena, hata wao wenyewe wasiweze hata kula mkate. Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili.
 
Mleta mada ulifanya je mpaka ukanunua gari, si wengine tunaamka kabla ya mapambazuko na kulala usiku mwingi lakini hatuna hata baiskeli!
Nilimuomba Mungu.
Mathayo 7:7
Ombeni, nanyi mtapewa
 
Nimeongeza na mhogo wa kuchoma., naila hapa na inateremka kwa jina la chai.

Aisee hawa mafundi mchundo🙌🏾
🐼🐒🔥
 
Nimeongeza na mhogo wa kuchoma
Umekumbuka kumshukuru Mungu kabla hujaanza kula huo mhogo
1 Wathesalonike 5:18
Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu
 
Back
Top Bottom