Nimewasambaratisha majambazi, usiku, kwa Jina la Yesu!

Ungetaja tena kwa nguvu "Allah ". Hiyo naona kama chai. Siku hizi jina Yesu linatumiwa kwa biashara.
Jina la Yesu tu ndilo lenye uwezo wa kumfukuza shetani na wasaidizi wake(wachawi, wezi, majambazi...)
Flp 2:9-11
Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.
 
afadhali wewe mwenyewe umejua kuwa unatupa chai na umetoa angalizo.
 
Mwamposa amewaharibu mmekuwa wajinga.
 
Jf imevamiwa na vichaa
 
Walokole muukoeni huyu mwenzenu, akiwahishwa atapona....
 
Unasemaje bure wakati ili uwe na biblia uwe na simu na bundle
Simu na bando unalotumia kuchangia mada hapa linatosha kudownload app ya Biblia.
 
Mi nilijua ni audio ukiwa unazinguana na vibaka hao kumbe ni gospel🤣🤣

Anyway, YESU NI MWEMA
😁😁
Asingepata muda wa kurekodi, alizama kwenye maombi.
 
Mleta mada ulifanya je mpaka ukanunua gari, si wengine tunaamka kabla ya mapambazuko na kulala usiku mwingi lakini hatuna hata baiskeli!
 
Jf imevamiwa na vichaa
Asante kwa kunipandisha cheo. Kumbe na mimi nimefikia level ya Yesu ya kuitwa nimerukwa na akili? Wow! This is great news!
Marko 3:20-30 SRUV
Mkutano wakakusanyika tena, hata wao wenyewe wasiweze hata kula mkate. Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili.
 
Mleta mada ulifanya je mpaka ukanunua gari, si wengine tunaamka kabla ya mapambazuko na kulala usiku mwingi lakini hatuna hata baiskeli!
Nilimuomba Mungu.
Mathayo 7:7
Ombeni, nanyi mtapewa
 
Nimeongeza na mhogo wa kuchoma., naila hapa na inateremka kwa jina la chai.

Aisee hawa mafundi mchundo🙌🏾
🐼🐒🔥
 
Nimeongeza na mhogo wa kuchoma
Umekumbuka kumshukuru Mungu kabla hujaanza kula huo mhogo
1 Wathesalonike 5:18
Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…