Nimewaza Ujinga: Kwanini magari yasigome kuwaka mpaka dereva atakapochomeka leseni yake na funguo kwa pamoja?

Nimewaza Ujinga: Kwanini magari yasigome kuwaka mpaka dereva atakapochomeka leseni yake na funguo kwa pamoja?

Ajenda ya upinzani ni kupinga maendeleo na kumtukana Rais Magufuli.
 
Mbona kulikuwa na wizi wa fedha hata kabla ya kuja kwa ATMs na sasa zipo lakini watu bado wanabuni njia mpya za wizi?

Wahalifu wasiwe kikwazo cha maendeleo ndio maana kuna taasisi ya Police.
Hilo la uhalifu ni moja ya sababu nyingi nilizotoa. Leseni bado tunaweza kuzidhibiti kwa njia rahisi zaidi. BTW Haya nchi zilizoendelea tatizo la watu kuendesha gari bila leseni au kwa kutumia leseni ya mtu mwingine siyo kubwa kihivyo. Tujaribu kufuatilia na kuiga wanavyofanya badala ya kukimbilia ku-complicate mambo ambayo hatuyawezi.
 
Tujaribu kufuatilia na kuiga wanavyofanya badala ya kukimbilia ku-complicate mambo ambayo hatuyawezi.
Kwanini ukae unaigaiga watu? Wewe hauna confidence ya kuanzisha kitu chako? Unatumiwa na mabeberu nini mkuu? Kila jambo kwako ni lazima lianzie ulaya? Wewe haupo serious...
 
BTW Haya nchi zilizoendelea tatizo la watu kuendesha gari bila leseni au kwa kutumia leseni ya mtu mwingine siyo kubwa kihivyo.
Acha kung'ang'ania nchi zilizoendelea katika kupata justification ya kila jambo. Jiamini kisha be you.
 
Leseni hizi zinazouzwa kama njugu na vishoka?
Hizi ni hoja za vijiweni lakini jamaa analazimishaa. Unapotaka kutatua tatizo inatakiwa uangalie chanzo chake na siyo kufanya maamuzi kama wanavyofanya wanasiasa. Mtu anataka kujenga ghorofa wakati hana hata nyumba ya tembe.
 
Unapotaka kutatua tatizo inatakiwa uangalie chanzo chake na siyo kufanya maamuzi kama wanavyofanya wanasiasa. Mtu anataka kujenga ghorofa wakati hana hata nyumba ya tembe.
Sio lazima kila mada uchangie. Unaweza ukasoma tu kisha ukaondoka zako.
 
Back
Top Bottom