Nimezisoma sheria za urithi katika Uislam, nikiri kwamba zipo kwa haki

Nimezisoma sheria za urithi katika Uislam, nikiri kwamba zipo kwa haki

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Kwa mujibu wa Sheria ya Kiislam mgawanyo wa urithi uko kama ifuatavyo:

Wajane

hurithi 1/8, Wengi huendelea kutunzwa na watoto wao na nimeona kwa huu mgao unalinda wasiwe na tamaa za kutaka mwanaume afe ilinwapate mali, k

Wazazi

- Wazazi hupewa 1/6 ya salio baada ya kuondoa fungu la mjane/wajane.

Watoto

Mali iliyosalia hugawanywa katika mafungu matatu. Watoto wa kiume hupata mafungu mawili na watoto wa kike hupata fungu moja. Watoto wa kiume hupewa mara mbili ya watoto wa kike. (Tukiachana na sheria za sasa za binadamu ukweli haufutiki kwamba Mungu alimuumba Mwanamke kuwa msaidizi kwa mwanaume, hana kwake ana kwao, hata mila zetu nyingi mwanamke akishaolewa tu huyo ni wa ukoo wa huko alikoolewa, watoto ataozaa watakuwa ni uoande wa mme wake, Pia mwanamke akiachika anarudi kwa kaka zake) ama hakuna watoto wa kiume atatafutwa mjukuu wake wa kiume, baba yake, babu yake, n.k.

Mjane Mwanaume

- Mgane (Mjane mwanaume) hupewa 1/4 ya mali ya marehemu mke wake kama kuna watoto au 1/2 kama hakuna watoto.

Watoto nje ya ndoa

Watoto nje ya ndoa hawawarithi chochote kama hawakuhalalishwa wakati marehemu akiwa hai au kuwepo wosia unaowapa urithi. (nadhani Mungu aliona mbali siku hizi mbegu zinaweza kuchomolewa bila kujijua zikaenda kupandikizwa kwa mwanamke)

Mali za kurithisha kwa wosia

si zaidi ya 1/3 isipokuwa kama kuna makubaliano ya warithi wote baada ya kifo cha mweka wosia
 
Mbona hujaongelea kwa wake waliozidi wanne? Vp Kama marehemu Hana watoto wakiume? BTW logic ya kuwapunja watoto wa kike urithi wao kisa wataolewa, Haina mashimo, maana sio wote watapenda kuolewa/ kuishi na waume zao mpaka mwisho.
 
Sheria ya kiislam inaruhusu wake si zaidi ya wanne

Kama hakuna watoto wa kiume atatafutwa mjukui wake wa kiume, baba yake, babu yake, kaka yake n.k
 
Wanawake wa kiislamu wanaungulia kimyakimya moyoni ndio maana wao hufikia kuuwa waume zao na kuwasambaratisha kabisa watoto ili mwisho wao mali zote ziwe mikononi mwao
 
Mtoa mada kumbuka pia Kabla ya mirathi, wakati wa ndoa dini inaruhusu Kila mtu kumiliki Mali kivyake, mkiachana Kila mtu afe na chake.....sio mke mama wa nyumbani halafu mkifumaniana mgawane jasho la mume aliyekuwa anahangaika usiku na mchana, au mke pia anafanya kazi halafu Mali zote zinahesabiwa za mume, ukiuliza alitoa mahari🤣🤣🤣

Na hiyo 1/8 ya urithi wa mke, ni anarithi lile jasho pure la mume, kama mke alichangia chochote katika kuchuma Mali, basi alichochangia kwanza kinatolewa anarudishiwa, Kisha Ile sehemu ya mume inayobaki ndio atarithi hiyo 1/8, nyingine ndiyo watarithi watoto na wazazi kama wapo.
 
Kama nafsi imesuuzika basi kheri
 
Huu ni mfumo na sheria kamila ila tabu kwa watekelezaji hata hao Bakwata ni chenga ,Ndo maana hii inahitaji elimu sana na sio urasimu kitu kama mirathi ni rahisi kuamua ila utasikia watu wanazungushana karibia miezi 6.

Elimu ni muhimu hata anayeenda kudai lazima awe anajua kila kitu ili asipigwe chenga ...Bahati mbaya elimu kama hizi ni ngumu sana kwa mtu mmoja mmoja kujua katika mitaala mingi ya madrasa hii wanafundishwa watu walioko ngazi ya juu Nina maana vijana wengi hwajui.

Elimu na mambo kama haya ambayo watu wengi tunakutana nayo mda wowote yaani kama wazazi wetu wanaweza kufa mda wowote basi ni muhimu...ukiachana na mirathi hata jinsi ya kuzika na kumkafini marehemu ni muhimu.

Hayo mambo Mimi kusoma kwangu madarasa hatukuwahi kusoma bahati nzuri tukiwa fomu Three ndo tulisoma kupitia kipind cha dini plus mambo ya mazishi.
 
Mbona hujaongelea kwa wake waliozidi wanne? Vp Kama marehemu Hana watoto wakiume? BTW logic ya kuwapunja watoto wa kike urithi wao kisa wataolewa, Haina mashimo, maana sio wote watapenda kuolewa/ kuishi na waume zao mpaka mwisho.

Kiislam kuolewa ni amri sio hiyari,
Sio ishu ya kupenda.
 
Mtoa mada kumbuka pia Kabla ya mirathi, wakati wa ndoa dini inaruhusu Kila mtu kumiliki Mali kivyake, mkiachana Kila mtu afe na chake.....sio mke mama wa nyumbani halafu mkifumaniana mgawane jasho la mume aliyekuwa anahangaika usiku na mchana, au mke pia anafanya kazi halafu Mali zote zinahesabiwa za mume, ukiuliza alitoa mahari🤣🤣🤣
Sasa bibie si uwe unasoma Kisha ukaelewa. Kwenye Uislamu Mwanaume ndiyo anatakiwa kumuhudumia Mwanamke.
 
Kiislam kuolewa ni amri sio hiyari,
Sio ishu ya kupenda.
Uwe unaandika mambo ukiwa na Elimu nayo. Sharti la ndoa katika Uislamu ni kuridhiana baina ya wenzi hao wawili. Hakuna ndoa ya kulazimishana katika Uislamu.

Hivi kijana kwani ni lazima uandike kila unachoona kiona. Kila siku unakosea unapoongelea Uislamu, unatakiwa ujifinze usilete ujuaji.
 
Back
Top Bottom