Nimezisoma sheria za urithi katika Uislam, nikiri kwamba zipo kwa haki

Nimezisoma sheria za urithi katika Uislam, nikiri kwamba zipo kwa haki

Yaani wenzio tuna songa mbele katika maisha mambo ya wanaume na wanawake tofauti yao ilisha fyekelewa mbali.
Hivi unajua wanawake wengi sasa hivi duniani ndio wanao fanya kazi na mwanaume anakaa nyumbani kulea watoto?
Dunia ime badilika kwa watu wenye pesa zao.
Sijui labda unakokaa wewe bado kuna mambo ya kumwachi efkumi mkeo ya chukula walahi, uwiiiii
Mwenye Enzi Mungu tuepushe walahi!
Tofauti ya mwanamke na mwanaume haiwezi toweka,ni wapi huko wanawake wengi ndiyo hufanya kazi na wanaume hukaa nyumbani!?
 
Hizo ni sheria kandamizi na zilizopotwa na wakati,mwanamke ana kwao na pia ana kwake,haya ndo masuala ya kumuoza mtoto wa kike huku ukimwambia asirudi labda awe mfu kitu kinachopelekea kuvumilia ndoa za mateso. Siku hizi ni 50/50,nyumba mkijenga wanandoa inakua na majina mawili mume na mke

Mkuu wahindi mwanamke ndo anatoa mahari,anyway usiseme dunia nzima sema baadhi ya nchi za africa maana huko kwa wazungu kuna wanawake wanaoana wao kwa wao
Sahihi
 
Busara imeangaliwa katika mioyo yao dhaifu hali ambayo imgesababisha kuwaua waume zao ili warithi Mali, na ndio maana kesi nyingi ni za wanawake kuua waume zao kwa kutaka Mali, na ukisia mwanaume kaua mkewe ujue ni kwa sababu ya wivu wa kimapenzi na sio mali. Mfano hapo juu Kwa Wamachame, hope utakuwa umeelewa mantiki.
Unatatakwimu sahihi kuhusu unachoandika au umeokoteza maneno ya mitaaani
 
Na mwanamke asipoachika? Hiyo ziada inaenda wap? Kama urith hakuna akiachika hapokelewi kwasababu huo urithi haupo?
Itabakia kwa kaka mtu, kwani UNAPOCHANGIA BIMA YA AFYA, USIPOUMWA ubarudishiwa kile kiasi? Hiyo inawekwa kwa maana matukio ni mengi, Dada yako anaweza kufiwa na mumewe nk nk nk. Shida yako unaweza in a negative way hivyo huwezi kutuhusi ubongo kuelewa hoja hiyo.
 
Maandishi ya dini utaona kama mwanamke ana raha sana. Utekelezaji wake sasa, ndo kasheshe. Achika uone kama utahudumiwa na hao kaka.
 
Ulivyo andika kule umekosea, inaoneka kuolewa katika uislamu ni amri, amri kivipi hujaandika ndiyo maana tulikukataa.

Ile kwamba mbingu yako iko chini ya mumewe.

Kuolewa ni nusra.

Hizo condition ni inafanya ndoa iwe lazima.
 
Thibitisha
( إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّهِ الْإِسْلَامُ ۗ وَمَا اخْتَلَفَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِآيَاتِ اللَّهِ فَإِنَّ اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ )

آل عمران (19) Aal-Imran

Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Kiislam mgawanyo wa urithi uko kama ifuatavyo:

Wajane

hurithi 1/8, Wengi huendelea kutunzwa na watoto wao na nimeona kwa huu mgao unalinda wasiwe na tamaa za kutaka mwanaume afe ilinwapate mali, k

Wazazi

- Wazazi hupewa 1/6 ya salio baada ya kuondoa fungu la mjane/wajane.

Watoto

Mali iliyosalia hugawanywa katika mafungu matatu. Watoto wa kiume hupata mafungu mawili na watoto wa kike hupata fungu moja. Watoto wa kiume hupewa mara mbili ya watoto wa kike. (Tukiachana na sheria za sasa za binadamu ukweli haufutiki kwamba Mungu alimuumba Mwanamke kuwa msaidizi kwa mwanaume, hana kwake ana kwao, hata mila zetu nyingi mwanamke akishaolewa tu huyo ni wa ukoo wa huko alikoolewa, watoto ataozaa watakuwa ni uoande wa mme wake, Pia mwanamke akiachika anarudi kwa kaka zake) ama hakuna watoto wa kiume atatafutwa mjukuu wake wa kiume, baba yake, babu yake, n.k.

Mjane Mwanaume

- Mgane (Mjane mwanaume) hupewa 1/4 ya mali ya marehemu mke wake kama kuna watoto au 1/2 kama hakuna watoto.

Watoto nje ya ndoa

Watoto nje ya ndoa hawawarithi chochote kama hawakuhalalishwa wakati marehemu akiwa hai au kuwepo wosia unaowapa urithi. (nadhani Mungu aliona mbali siku hizi mbegu zinaweza kuchomolewa bila kujijua zikaenda kupandikizwa kwa mwanamke)



Mali za kurithisha kwa wosia

si zaidi ya 1/3 isipokuwa kama kuna makubaliano ya warithi wote baada ya kifo cha mweka wosia
Ziko poa sana, realistic
 
Back
Top Bottom