Labda pia nichangie japo kiduchu japokuwa somo la mirath hili ni pana sana ni maktaba nzima kabisa sio la kumsomesha mtu kwa siku moja wala wiki moja.....
Kama alivyoongea bwana
Accumen Mo sheria zetu ni nzuri sana ila sometimes zile ambazo is out of our favor huwa hatuzifati na ukitaka kuamini kwamba ninaloliongea ni kweli jiulize tu katika mtaa wako, ukoo wako au campaign yako ambayo ni waislam, lini umetokea msiba then wakam consult sheikh/ulamaa wa mambo ya mirath ili awasaidie kugawanyia kulingana na sheria ya kiislam????
Why nasema kum consult sheikh??? Kwasababu no elimu nadraa kumkuta mtu sio sheikh au hana elimu kubwa kumkuta ana elimu ya mirath Bali wapo hata masheihk wakubwa ila hawayajui kwa sehemu kubwa masiala ya mirath maana ni mapana sana nje na tunavyoyazania...si rahisi kwa hizi madrasa kusomesha haya mambo labda kwenye ma markza na mavyuo makubwa
Nimemskia duktur mbarak Awes wa Kenya akisema kwenye mirath maulamaa wameafikiana kuna masiala tariban 30k kulingana na scenarios tofauti tofauti you can imagine how bigger it is!
Kuna conditions pia kama tatu baina ya muarith na waarith(analisiwa na mwenye kurith)
i. Daraja ya ukaribu
Iwe itakavyokuwa mwenye nasaba ya karibu na marehemu atapata parefu
ii. Umri
Wewe mtoto wa marehemu mwenye miaka 30 sheria inakutazama ina uhitaji zaidi Na Mali kuliko mzazi wa marehemu mwenye miaka 80
iii. Majukumu
Hapa pia ni miongoni mwa sababu pia kwanini mwanamme apate Mara mbili ya mwanamke kwa sababu kwenye uislam jukumu la kutunza familia na kuhudumia ni la mwanamme vinginevyo kuna dharula mume hana maisha haha
Pia kuna condition zikijitokeza mtoto wa kike anarithi sawa na mwanamme na kuna condition zikijitokeza mwanamke ana rithi zaidi ya mwanamme! Ndio maana nikaanza kusema wansema maulamaa kuna masiala(dalili)(conditions) nyingi sana karibia maelfu haswa! Hivyo haya mambo ni ya wanachuoni ni ngumu upo madrasa na miaka yako 13 usomeshewe elimu kama hii and that's why kuna mailamaa haswa kabisa wabobezi wa mambo haya