Nimfanyeje mke wangu aipende na kuifurahia harufu ya sigara isimkere, Ndoa bado Changa

Nimekuwa nikivuta sigara mwaka wa 9 huu..hapo nyuma kidogo nimekutana na binti alinipenda hv hv na mifegi yangu,na tukaishi vzr kabisa ila nature iliamua siko nae sasa nimepata mwingine nae anavumilia japo najitahidi sana kiwa smart na mwenye kunukia kila wakati,napiga mswaki mara kwa mara,natumia hydrogen peroxide mouth wash inauzwa buku tu inatoa harufu mbaya kinywani.
Ila nina mpango wa kuacha sasa
 
Kipindi naacha sigara zile wiki 2 za mwanzo aisee nilipata shida sana yaani mdomoni mate yanakauka kauuu ukivuta fegi mate yanarudi kama kawaida ikawa mwendo wa maji tuu mate yakikauka mi napiga maji tuu mpaka hali ikarudi kawaida..hapo chagua uache mke au sigara japo najua huwezi acha sigara kwasabu ya vitu vya kijinga😇😇😇
 
USiache aisee kuna jamaa hapa aliacha sigara baada ya siku 3 akafa kwa ajari we unadhani chanzo ninini kama sio laana ya kuacha fegi
 
Tafuta sigara za Grade A cuban cigar kwa mfano achana na hizo sigara nyota hazijawahi kuwa na harufu ya kuvutia
 
Wewe ukipewa nasaha kwa njia ya kupakwa mafuta kwa mgongo wachupa hautasaidika.

Njia nzuri na njema pekee ya kuchukua wewe hapo ni kuacha sigara na si kumzoesha harufu mkeo.

Ukiwa kijana hauwezi kuona dhiki zitokanazo na uvutaji, lakini kama Mungu hajakuua mapema hadi ukazeeka, vifo vitokanavyo na tumbaku huwa ni vya 'kujiona' namna kinavyokuchukua na kwa njia ya mateso sana.

Natumaini hili ulikuwa haujaelezwa na mtu.

Anza mazoezi na kujenga dhamira ya kuacha, utafanikiwa.

Ninajua uraibu utokanao na sigara, ni ngumu kuacha.

Lakini ukidhamiria kutoka moyoni, sigara utaiacha bila shida.

Hapa ushauri wangu nimezingatia afya yako tu, sijaangalia mambo ya mapenzi wala nini.

Mimi ni shuhuda wa madhara ya sigara, nimezika ndugu zangu wanne wavutaji.
 
Mshawishi na yeye avute
 
Anza taratibu Kila kitu kilianza kidogo kidogo Kisha kitu kamili ukiwa unakula fegi unaweza kushika pesa mkono mmoja unampa pesa ya nyama au ya kwake akatumie tenga kias flani hivi kutokana na hazi zenu
 
Sawa
 
Kwanini umfiche mwenza wako wa maisha jambo kama Hilo?
Dunia hii kuna kila tabia za watu
Kuna mpaka wauwaji ila hawatasema maisha yao
Wapo wanaoficha mengi na tunashuhudia wakisema sikutegemea kama ni mlevi au mvutaji nk
Wengine wanadanganya ili wafanikishe mambo yao
Ila ni vizuri kuwa mkweli na kuainisha yote mazuri na mapungufu pia

Mkiendana ni vizuri zaidi
 
Hiyo haiwezekani,jitahidi kuacha kuvuta
 
Acha sigara! Mungu amemleta kwako ili akusaidie na kuacha sigara! Sigara siyo nzuri kwa afya yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…