#COVID19 NIMR: Tunafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania kama zinatibu Covid 19, chanjo za Magharibi bado hazijathibitika kukinga

#COVID19 NIMR: Tunafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania kama zinatibu Covid 19, chanjo za Magharibi bado hazijathibitika kukinga

Mkuu kama ndio hivyo ni kwa nini tumekua tukitumia mabilioni kila mwaka kuagiza madawa ya mafua, upumuaji, athma na magonjwa ya mfumo wa hewa badala ya kutumia tangawizi na limao?

Kwa nini serikali imekua ikitumia hela zote hizo huku dawa ya hayo magonjwa inajulikana miaka mingi?
Kwa sababu tumeacha vya kwetu tunashadadia vya wazungu.hapa kwetu Africa tuna miti mingi inayotibu magonjwa mengi lakini hatutaki kuifanyia utafiti. For example, I have 100% confidence kuna dawa ya kinyeji inaongeza uchungu kwa kinamama wajawazito.
 
Pro. Mbaya, kabla ya kuikana chanjo ya Korona ni vizuri ungeanzia na mile ambacho wewe umeifanyia dunia. Wengine tumeaanza kukusikia humu JF ukiwa na maandiko yako ya upande mmoja kama huu wa leo, upande wa kuunga mkono juhudi.

Ili tukuamini ukisemacho weka hapa kumbukumbu yako hapa kuwa uliwahi kuishi duniani, mfano dawa ya kutibu jeraha la kuumwa na mende.

Kama hauna chochote basi jikite kwenye maswala ya CCM dhidi ya Chadema na ushindi mnono wa wizi wa kura, haya ya tiba yaache yapite kwani huu si uganga wenu wa kienyeji.
 
Kwa sababu tumeacha vya kwetu tunashadadia vya wazungu.hapa kwetu Africa tuna miti mingi inayotibu magonjwa mengi lakini hatutaki kuifanyia utafiti.for example, I have 100% confidence kuna dawa ya kinyeji inaongeza uchungu kwa kinamama wajawazito.
Tatizo wataalamu wetu hawafanyii tafiti. wakishapata phd wanakimbilia siasa. trust me siasa ndio inaua academics hapa nchini.
 
Kwa sababu tumeacha vya kwetu tunashadadia vya wazungu.hapa kwetu Africa tuna miti mingi inayotibu magonjwa mengi lakini hatutaki kuifanyia utafiti.for example, I have 100% confidence kuna dawa ya kinyeji inaongeza uchungu kwa kinamama wajawazito.
Hizo zinatuhuma za kuleta matatizo kwenye mfuko wa uzazi

R.I.P shemeji yangu...tusichezee mfumo wamama wengi wamepoteza maisha wakati wa kujifungua.

Shida ya dawa zetu hakuna dosage per weight, au age.

Everyday is Saturday........... 😎
 
Hizi spices nyingi asilia yake ni Asia watu huko wamekufa huku wakiwa na glasi za tangawizi mikononi na sasa wanalilia chanjo sasa nyinyi maprofesa uchwara na makada wa CCM mtatuua mpaka lini
Mkuu, Asia, si ndo Bala la jangwa 87%
 
Mkurugenzi mtendaji wa NIMR Prof Yunus Mgaya amesema taasisi yake inafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania zikiwemo 4 za kufukiza kama zinatibu Covid 19.

Utafiti wa dawa hizo za asili ambazo zimetumika toka enzi za mababu zetu zinafanyiwa utafiti na wanasayansi wetu kupitia baadhi ya hospitali zetu, amesema.

Prof Mgaya amesema chanjo za magharibi zinazotumika sasa huko duniani hazijathibitisha kukinga covid 19 kwahiyo nazo ziko kwenye utafiti ila zikileta madhara hakuna taasisi itakayolipa fidia.

Prof Mgaya amewataka wananchi watakaofanikiwa kuona kichupa cha chanjo za ulaya wasome kwa makini maandishi yote wataona namna wawekezaji wanavyokana kulipa fidia endapo tatizo lolote litatokea.

Prof Yunus Mgaya alikuwa skiwakilisha mada chuo kikuu cha Dar es salaam katika kongamano linaloongozwa na Dr Rioba na kurushwa mubashara na TBC.

Maendeleo hayana vyama!
Nilidhani ni taasisi ya kisayansi kumbe ni ya kisiasa
 
Huyu Prof ni kama anacheza na akili za watu kuwalazimisha kinamna kutumia nyungu, kuwaambia watu kinga za ulaya hazijathibitishwa na hawalipi fidia kwa madhara yatakayotokana na matumizi yake ni ujanja ujanja, mbona hajasema kama wao watalipa fidia kwa madhara yatakayosababishwa na nyungu, yaani mgonjwa wa Corona akipiga nyungu au akinywa juice ya malimao na asipopona mumlipe fidia.
Wao bado wanafanya utafiti na hawajatoa ramsi dawa au chanjo ianze kutumika hivyo suala la dhamana sijui side effects au fidia haihusiki kwa sasa.
Wenzetu waliotoa dawa na kuidhinisha matumizi ndio wako responsible
 
Kwa sababu tumeacha vya kwetu tunashadadia vya wazungu.hapa kwetu Africa tuna miti mingi inayotibu magonjwa mengi lakini hatutaki kuifanyia utafiti.for example, I have 100% confidence kuna dawa ya kinyeji inaongeza uchungu kwa kinamama wajawazito.
Corona iliripuka mwaka gani Africa na tukaitibu kwa miti shamba ili tuitafute tena hiyo dawa?
 
huku mtaani watu wanajitibu wenyewe kwa kujifukiza na wanapona! tuache kupinga pinga kila jambo. ... humu ushabiki ni zaidi ya maarifa. ukweli ni kwamba mtaani watu wanagua huo ugonjwa na kupona wenyewe bila kwenda hospital unakuta mtu harufu imekata ,,, anajifukiza baada ya muda anarejea.
 
Ila zingine zina ubora, haki ya Mungu Africa hatuna viongozi bora. Ni bora viongozi, sasa wenyewe wamegundua chanjo yoyote?
 
Pro. Mbaya, kabla ya kuikana chanjo ya Korona ni vizuri ungeanzia na mile ambacho wewe umeifanyia dunia. Wengine tumeaanza kukusikia humu JF ukiwa na maandiko yako ya upande mmoja kama huu wa leo, upande wa kuunga mkono juhudi. Ili tukuamini ukisemacho weka hapa kumbukumbu yako hapa kuwa uliwahi kuishi duniani, mfano dawa ya kutibu jeraha la kuumwa na mende.
Kama hauna chochote basi jikite kwenye maswala ya CCM dhidi ya Chadema na ushindi mnono wa wizi wa kura, haya ya tiba yaache yapite kwani huu si uganga wenu wa kienyeji.
MKUU USIHANGAIKE SANA, PROF AJE HAPA ATUAMBIE KWENYE ENEO LA UTAFITI WA CHANJO KATI YA HAWA WAWILI TUMSIKILIZE YUPI KWA CV HIIZI WALIZO NAZO. MAANA HUYO MAMA CHINI NDIE ALIE SEMA CHANJO YA PFIZER-BIONTECH COVID-19 VACCINE IPO SALAMA KWA ASILIMIA 95.

Prof. Yunus Mgaya
Director-General, NIMR
Prof. Yunus Mgaya is Tanzanian, born in 1957. He studied at the University of Dar es Salaam, the University of British Columbia and the University College Galway in Ireland.

His research has focused mainly on coral reef fisheries, biology and management of invertebrate fisheries as well as aquaculture of different species. He is based at the University of Dar es Salaam, where he started out as a Tutorial Assistant and rose through the ranks to become a full Professor in 2006.

Over the years, Prof. Mgaya has gained wide administrative experience at the University and his recent achievements include his appointment as Associate Dean in the Faculty of Sicence (2000-2002), the Dean of Aquatic Sciences and Technology (2003-2006) and the Deputy Vice Chancellor in Charge of Planning, Finance and Administration (DVC-PFA) (2006-2014) and the Executive Secretary of the Tanzania Commission for Universities (TCU) (2014).

KATHRIN U. JANSEN, PH.D.​

Senior Vice President, Head of Vaccine Research and Development
Dr. Jansen received her doctoral degree in microbiology, biochemistry & genetics from Phillips Universitaet, Marburg, Germany. Following completion of her formal training, she continued her postdoctoral training at Cornell University working on the structure and function of the acetylcholine receptor.

She then joined the Glaxo Institute for Molecular Biology in Geneva, Switzerland, where she focused on basic studies of a receptor believed to be a drug target to treat allergies. Dr. Jansen was appointed an Adjunct Professor at the University of Pennsylvania – School of Medicine in 2010.

Before the Wyeth acquisition by Pfizer in 2009, Dr. Jansen served as Senior Vice President at Wyeth Pharmaceuticals and on Wyeth’s Research and Development Executive Committee since 2006 and was responsible for vaccine discovery, early development and clinical testing operations.
 
1: Mtu ambaye ameshindwa kujua kuwa chanjo iko exempted kwenye madhara kwa mchanjwaji kulipwa na kampuni inayotengeneza chanjo na hiyo ni SERA kwa chanjo zote hata hanisumbui. Na huyu ni Profesa na mkurugenzi mkuu wa tasisi ya utafiti.

2: Mkurugenzi mkuu, ambaye hajui kuwa kuna emergency permit provision ya vaccine baada ya watu kukaa na kufanya analysis dhidi ya kusubiri miaka 15-18 ili chanjo iingie sokoni. Na utaratibu huu upo, kitu kama hicho pia kilihusisha chanjo ya Ebola ilipoonyesha ufanisi.

Angekuja na facts kuwa sababu zilizotumika kisayansi hazijitoshelezi au NIMR tumegundua:

A: Kwenye drug discovery/molecules and development kuna hiki kitu kwenye zile chanjo na hazifai.

B: Uwezo wake tulielezwa ni kiasi hiki na sisi kwa uwezo wetu tumegundua uwezo wake ni kiasi hiki, hivyo hazifai.

C: Kuna molecule hii inaleta shida hii, hivyo hazifai.etc.

D: Kwenye clinical trails, chanjo ilionyesha WEAKNESS hii na haikurekebishwa mpaka inaenda sokoni.

Na tukumbuke kadri muda unavyoenda, wakati sisi tunalala sana, wenzetu wanazidi kugundua more sophisticated tools kumaliza kazi zao mapema na kwa ufanisi.

Lakini, wanakuja mbele yetu kama wanasiasa tu. Please, let's invest in science and technology.

Tuache ku-mbwela mbwela tu.
 

Attachments

  • 20210308_085109.png
    20210308_085109.png
    8.7 KB · Views: 1
Waziri mkuu wa Israel, Rais wa Africa Kusini, Rais wa Ghana, Joe Bidden na wengine walio choma chanjo huyu baba anaweza akalinganishwa nao kwa akili, fedha, maisha... kwamba tuseme yeye Mkurugenzi wa NIMR ana akili sana na ujanja mwingi zaidi yao. watu wengine ni bange tu.
 
Watu siku hizi wanaongea kwa kufuata mlengo wa mteuzi wao ili wasitumbuliwe au wapewe cheo kikubwa zaidi. Mambo ya taaluma yaneshatupwa pembeni. Tunarudi enzi zacujima kwa spidi kubwa sana.
 
Back
Top Bottom