#COVID19 NIMR: Tunafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania kama zinatibu Covid 19, chanjo za Magharibi bado hazijathibitika kukinga

#COVID19 NIMR: Tunafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania kama zinatibu Covid 19, chanjo za Magharibi bado hazijathibitika kukinga

Mkurugenzi mtendaji wa NIMR Prof Yunus Mgaya amesema taasisi yake inafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania zikiwemo 4 za kufukiza kama zinatibu Covid 19....
Huyu Profesa kila siku anazidi kuwa na hekima inayoendana kabisa na umri wake, majukumu yake, elimu yake na hadhi yake. Amenifurahisha sana jana, Yaani unaona kabisa kuwa huyu mtu yuko katika kiwango kile anachotakiwa kuwa na amesoma na akaelimika. Huyu mtu ameelimika, tuseme tu ule ukweli
 
Hii si sababu ya kutosha.
Wakati unafanya huo utafiti.
Fikiria:
1: Population ya taifa husika
2: Size ya taifa husika
3: Ugonjwa ulisambaa kiasi gani kabla ya chanjo?
4: Priority amepewa nani kwanza?
Hii si zima moto.
Suala hapa sio "population" , tatizo ni juu ya ubora na uhakika wa chanjo zenyewe bado hakuna uhakika, ndio maana hata marekani yenyewe hawana uhakika juu ya chanjo gani raia wake watumie, Ujerumani, Ufaransa bado kuna "debate" juu ya chanjo gani ndio ya uhakika zaidi.

Naipongeza sana Nchi yangu ya Tanzania kwa kuchukua tahadhari na umakini juu ya kupokea chanjo kutoka mataifa mengine.
 
Mkurugenzi mtendaji wa NIMR Prof Yunus Mgaya amesema taasisi yake inafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania zikiwemo 4 za kufukiza kama zinatibu Covid 19....
Kikubwa kabisa alichosema Profesa Mgaya jana ni kuwa
  • Hiki kilichopo sasa kinachosemekana kuwa ni chanjo siyo chanjo bali ni utafiti kwa ajili ya kupata chanjo
  • Kawaida, utafiti kwa ajili ya kupata chanjo huwa unalipiwa na wale wanaofanya utafiti huo, wanatkiwa kulipa pesa kwa ajili ya kupata taarifa za utafiti wao
  • Kwa hiyo kama tukikubali Tanzania kuletwa kwa chanjo hiyo ambayo bado ipo kwenye utafiti, sisi ndiyo tunatakiwa kulipwa na watafiti hao
  • Yule anayeleta chanjo hiyo ya utafiti inabidi atupe chanjo hiyo bure na pia atulipe, na siyo sisi kununua chanjo hiyo
Baada ya utafiti huo, chanjo hiyo ikishapatikana ndiyo hapo sasa sisi tutatakiwa kutoa pesa kununua chanjo hiyo, iwapo tu bado tutakuwa tunaihitaji
 
sisi watanzania hatutaki chanzo ambazo ni za kulazimishwa! hivi hao wanao tushinikiza kutumia hiyo chanjo ndio wana thamini zaidi uhai wetu kuliko sisi wenyewe?! tafakari kwa makini.
Ongelea nafsi yako..usiongelee sisi.. inawezekana kuna mbumbumbu wengine kama wewe ila usitumie kauli za sisi watanzania, kuna wengine tunajielewa!
 
Mkurugenzi mtendaji wa NIMR Prof Yunus Mgaya amesema taasisi yake inafanyia utafiti dawa 7 za Kitanzania zikiwemo 4 za kufukiza kama zinatibu Covid 19.

Utafiti wa dawa hizo za asili ambazo zimetumika toka enzi za mababu zetu zinafanyiwa utafiti na wanasayansi wetu kupitia baadhi ya hospitali zetu, amesema.

Prof Mgaya amesema chanjo za magharibi zinazotumika sasa huko duniani hazijathibitisha kukinga covid 19 kwahiyo nazo ziko kwenye utafiti ila zikileta madhara hakuna taasisi itakayolipa fidia.

Prof Mgaya amewataka wananchi watakaofanikiwa kuona kichupa cha chanjo za ulaya wasome kwa makini maandishi yote wataona namna wawekezaji wanavyokana kulipa fidia endapo tatizo lolote litatokea.

Prof Yunus Mgaya alikuwa skiwakilisha mada chuo kikuu cha Dar es salaam katika kongamano linaloongozwa na Dr Rioba na kurushwa mubashara na TBC.

Maendeleo hayana vyama!
Hata kile kichupa cha dawa ya Bupiji inayopigiwa debe na rais na Muhimbili ina maandishi madogo sana ambayo no vigumu kusoma kwa macho ya kawaida

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
Vipi ile ya Madagascar ina ubora?

Mlisema mnaenda kuifanyia utafiti maabara je majibu yalikuwaje??
Yaani hawa viongozi wetu wanatuonaga na sie (wananchi) wote pia ni hamnazo kama wao...hawajui tunawachora tu kwakuwa uwezo wa kuwafanya hatuna!.
 
Hivi mkuu, tokea vifo vifululize hapa inapita wiki kama tatu sasa na, Ni lini tena Chadema wazee wa kuripoti habari za misiba wamefanya hivyo??

Kaa kimya tuionyeshe Dunia namna Bora ya kushughurikia milipuko ya magonjwa
Acha kubetua makalio juu kwa jambo usilolijua, kitaalam (sayansi) magonjwa yote yenye tabia za mlipuko kama korona, kipindupindu nk yana nyakati huwa maambukizi na madhara huwa ni makubwa zaidi, so sio nyakati zote madhara huwa juu...kutegemeana na mazingira ya nyakati hizo.

Magonjwa hayo ya milipuko hushambulia sana kuanzia miezi ya novemba hadi machi

So msianze kumpamba huyo mshamba wenu kwa sifa asizostahili, automatically kasi ya korona itapungua sana kuanzia sasa...ila muambieni apunguze ujinga ahimize wananchi wasiache kuchukua tahadhari maana dalili zinaonesha tatizo bado litarudi tena kwa kasi hapo baadae, hasa kutokana na njia alizoamua kuchukua ktk kukabiliana nalo.
 
Kikubwa kabisa alichosema Profesa Mgaya jana ni kuwa
  • Hiki kilichopo sasa kinachosemekana kuwa ni chanjo siyo chanjo bali ni utafiti kwa ajili ya kupata chanjo
  • Kawaida, utafiti kwa ajili ya kupata chanjo huwa unalipiwa na wale wanaofanya utafiti huo, wanatkiwa kulipa pesa kwa ajili ya kupata taarifa za utafiti wao
  • Kwa hiyo kama tukikubali Tanzania kuletwa kwa chanjo hiyo ambayo bado ipo kwenye utafiti, sisi ndiyo tunatakiwa kulipwa na watafiti hao
  • Yule anayeleta chanjo hiyo ya utafiti inabidi atupe chanjo hiyo bure na pia atulipe, na siyo sisi kununua chanjo hiyo
Baada ya utafiti huo, chanjo hiyo ikishapatikana ndiyo hapo sasa sisi tutatakiwa kutoa pesa kununua chanjo hiyo, iwapo tu bado tutakuwa tunaihitaji
Unachokizungumzia kitaaluma tunakiita Clinical trial na inakua na clearance zake unapewa certificate pia na hata kwa wanyama hua tunapata consent ya mmiliki endapo mnyama atakua included kwenye study na ikitokea shida hulipwa pia....

Chanjo ya Covid -19 ishavuka pre -clinical trials sasa tuko post marketing surveillance ajabu watu bado wanaishi zama za mawe kuamini chanjo yaweza kuingia kwenye market bila kufanya clinical trial phase 1-4 na muda huo wanapokea ARV's na na Chanjo lukuki za watoto
 
Prof. Mgaya namheshimu sana. Lakini akubali kuwa tafiti za chanjo zilizofanyika duniani zimefanywa na wataalam kama yeye. Sasa hoja yake ya kuzidharau inaanzia wapi? Teknolojia zinaongezeka kila leo duniani. Tafiti za kuchukua miaka 10 ili kuokoa maisha zimepitwa sana na wakati. NIMR nawapongeza kwa dhati kwa kutupatia products (natural) ambazo zinatufaa katika kipindi kifupi (chini ya miezi 6). Tafiti za Ki-Sayansi zinapingwa kwa tafiti za kisayansi na si vinginevyo. Porojo za Kisiasa uchwara tuziache katika hoja kubwa jamani
Mkuu Prof Mgaya hawezi lingana na watafiti wa huko nje hata kwa chembe.
Kimsingi hana miundombinu ya kufanya tafiti husika na vile vile tafiti za viruses km covid si fani yake hata kidogo.
 
Unachokizungumzia kitaaluma tunakiita Clinical trial na inakua na clearance zake unapewa certificate pia na hata kwa wanyama hua tunapata consent ya mmiliki endapo mnyama atakua included kwenye study na ikitokea shida hulipwa pia....

Chanjo ya Covid -19 ishavuka pre -clinical trials sasa tuko post marketing surveillance ajabu watu bado wanaishi zama za mawe kuamini chanjo yaweza kuingia kwenye market bila kufanya clinical trial phase 1-4 na muda huo wanapokea ARV's na na Chanjo lukuki za watoto
Dokta, how long does it take kwa chanjo kupitia stages zote hizo hadi kuwa confirmed kuwa ni chanjo sahihi kwa ungonjwa husika, ukizingatia kuwa Covid-19 is younger than 1.5 a year? Unachomaanisha wewe hapa ni kwamba chanjo hiyo iko sahahi na imepitia stages zote zinatzotakiwa, si ndiyo?.
 
Kiranja mkuu akisema chanjo inafaa atakuja na utafiti mwingine wa kusema ni salama na inafaa, watu wachanjwe🤣
 
Mzee unashinda kwenye tv kuanzia asubuhi mpk saa sita usiku [emoji23][emoji23][emoji23]

Ova
Huyo ni mwajiriwa wa uvccm au (MATAPA) Make Tanzania Poor Again, kazi yao ni kuwa mitandaoni/kwenye tv kumsifia Jiwe
 
Jamani tushasema sana, kimeo hiki!
 
Dokta, how long does it take kwa chanjo kupitia stages zote hizo hadi kuwa confirmed kuwa ni chanjo sahihi kwa ungonjwa husika, ukizingatia kuwa Covid-19 is younger than 1.5 a year? Unachomaanisha wewe hapa ni kwamba chanjo hiyo iko sahahi na imepitia stages zote zinatzotakiwa, si ndiyo?.
Clinical trial zinachukua miaka 3 hadi 6 ila lengo kuu la clinical trial ni kuestablish uhakika kuhusu usalama wa mtumiaji

Kwa kifupi covid haina hata miaka 2 ila imeua watu sana so hatuwezi kusema tuendelee kukaa miaka mingi bila utafiti ndio maana chanjo imefanyaiwa utafiti wa haraka na gharama( tafiti zina gharama kubwa sana) hadi kufikia hapo phase zote zilifanyika issue inabaki kila mtu kujipigia upatu kwa nchi aliyopo ipi iko vizuri kuliko nyingine lazima kuna moja itakua superior !

Mwisho niseme tu huku niliko nilipata Chanjo ya Moderna nina mwezi sasa na sijaona shida yoyote hadi sasa...
 
Back
Top Bottom