Nimsaidiaje huyu best yangu anayefilisiwa na Forex?

Nimsaidiaje huyu best yangu anayefilisiwa na Forex?

Kwangu forex ndio inaniweka mjini..nimepaga Nyumba kwa sababu ya forex na ninaishi kwa sababu ya forex..huyo kuna kosa analofanya..na ni la kawaida nalo ni kwamba hana business plan ya daily au malengo..na hasa anawaza utajili wa haraka kupitia forex kitu ambacho sio ukweli...
Lakini huenda anategemea signals za kwenye magroup hayo anayolipia kitu ambacho ni kosa kubwa sana kwenye forex
Zaidi atafute mwalimu wa karibu Ili amfundishe hakika atafanikiwa
Huyo jamaa ni lot tembo mtaji sungura ndo tatizo, alafu anaamini pesa ni za bure tu na utajiri wa haraka. Akili itamkaa sawa
 
For telegram user

Anayehitaji kujifunza
*forex basic
*advanced course,candlestic pattern and pysology behind its formation
*Supply and demand strategy

ajoin telegram chanel

👇🏽
Forex lesson tanzania (swahili)
 
Jana amenunua latest books kwa LORDFX sijui ni broker wa wapi, katumia ela zote now ashaanza kunililia shida.
Wale walokole please muwekeni jamaa kwenye maombi na maombezi kila mpigapo goti kwa muumba.

Mbona unajua sana hiyo Forex as if wewe mwenyewe ndiye unayecheza
 
For telegram user

Anayehitaji kujifunza
*forex basic
*advanced course,candlestic pattern and pysiology behind its formation
*Supply and demand strategy

ajoin telegram chanel

👇🏽
Forex lesson tanzania (swahili)
 
Atamimi rafiki yngu mkubwa amefilisika na kurudu kwao moshi huu mchezo sitaki ata kufahamu n Atari kma ukoma

Nami rafiki yangu kakimbia Dar kisa Forex.Kwa nini utake pesa bila kuwajibika,na hesabu kupata pesa bila kuwajibika ni dhambi sana
 
Yale yale,kwenye forex kuna watu wanaokula na kuna watu wanaoliwa... He is in the later group
 
Usimkatishe tamaa.
Mimi nimeacha kazi nilikuwa meneja mauzo Vodacom kanda ya kaskazini nikaaacha kazi.
Nimejenga sasa nina usafiri nimeoa....
Ninaishi maisha yangu ninayotaka.
Huyo anakosea mahali anichek nimtumie vitabu 9 tu akimaliza kusoma atafaidi.
Tatizo letu hatutaki kusoma...tunapenda kutumia maarifa ya waliosoma huko kwenye magrup.
Na mm naomba unitumie ivyo vitabu mkuu
 
Hivi unaijua FOREX vizuri??? Inshort hiyo ni miradi ya watu uko Ulaya, Ingekuwa rahisi kila mtu angekimbilia huko.
Jamaa amechoka mbaya ungemuona ungemhurumia
Smart money sio kwa ajili ya kila mtu...Shaffii Dauda anapiga pesa ndefu kwa betting tu
 
Usimkatishe tamaa.
Mimi nimeacha kazi nilikuwa meneja mauzo Vodacom kanda ya kaskazini nikaaacha kazi.
Nimejenga sasa nina usafiri nimeoa....
Ninaishi maisha yangu ninayotaka.
Huyo anakosea mahali anichek nimtumie vitabu 9 tu akimaliza kusoma atafaidi.
Tatizo letu hatutaki kusoma...tunapenda kutumia maarifa ya waliosoma huko kwenye magrup.
Story za kutunga kama hizi ndio zinawafelisha vijana.
 
Mm nilikuwa nafundisha private school napigwa kama 6k,
Ila natrade forex now naitafuta iyo 6k within one week and half.naweza piga 2M per month nakazi nimeacha nafanya forex ila nimejiajir.
Ushaur wa bure.hakuna mwalimu wa forex na hata tokea but hii nakwambia kama mwl achana na utapeli wa mitandao tafuta vitabu soma.tutorial you tube.achana na magroup ya telegram .Forex is mind game.depend how smart you are?
 
IMG_0019.JPG
 
Wakuu wa JF hope mko poa sana na maisha yanaenda fresh pande zenu.

Ninaandika uzi huu kwa uchungu sana kuhusu rafiki yangu wa kufa na kuzikana (he Is like a brother to me), huyu jamaa alijitumbukiza kwenye FOREX yapata mwaka sasa na hakuna kitu amefaidika nacho zaidi ya kupoteza pesa. Jamaa ni student nimekua nikimshauri sana aachane na hiyo miradi ya wazungu huko Ulaya kwani hakuna anachopata zaidi ya kuunguza account every now and then.

Jamaa ana hali mbaya sana kwa sasa ameuza kila kitu hana hata nguo ya kuvaa/kiatu lakini pesa yote ya boom + anayotumiwa kwa matumizi mengine anatumbukiza FOREX. Jana nimeongea nae aachane na hii mishe naona kama ameanza kunichukia flani, daily yupo YOUTUBE anafatilia videos about FOREX, ana groups za Telegram & Whatsapp zaidi ya 50 za mambo hayo ya FOREX na nyingi analipia. Kila nikimpa ushauri ananiona kama mimi ni kikwazo cha maisha yake, he keeps on saying anzia January nakua tajiri namwambia kirahisi hivo anasema we tulia hizi hela ni za bure lazima nizipate.

Then he keeps on saying HELA za FOREX zipo tuu na ni zabure kabisa eti mimi ndio mshamba sizitaki hizo ela za bure. FOREX complications ni nyingi sana, daily ananitajia watu wa uko SOUTH AFRICA waliofanikiwa, namjibu waliofanikiwa ni mmoja kwa milioni Ila haelewi. Bado sijajua aliemdanganya aingie kwenye hiyo mishe ni nani.
Ukimwambia FOREX ni mchezo kama UPATU anamind sana eti nisidharau biashara za watu.

Wakuu nimpe ushauri gani huyu best yangu maana anaangamia mbele ya macho yangu and sitaki kuona hilo linatokea.

Best regards,
Mbao Ya Chuma.
achana nae mkuu kunywa [emoji481]
 
Back
Top Bottom