Nimsaidiaje huyu best yangu anayefilisiwa na Forex?

Nimsaidiaje huyu best yangu anayefilisiwa na Forex?

Mm nilikuwa nafundisha private school napigwa kama 6k,
Ila natrade forex now naitafuta iyo 6k within one week and half.naweza piga 2M per month nakazi nimeacha nafanya forex ila nimejiajir.
Ushaur wa bure.hakuna mwalimu wa forex na hata tokea but hii nakwambia kama mwl achana na utapeli wa mitandao tafuta vitabu soma.tutorial you tube.achana na magroup ya telegram .Forex is mind game.depend how smart you are?
Appreciate
 
Wakuu wa JF hope mko poa sana na maisha yanaenda fresh pande zenu.

Ninaandika uzi huu kwa uchungu sana kuhusu rafiki yangu wa kufa na kuzikana (he Is like a brother to me), huyu jamaa alijitumbukiza kwenye FOREX yapata mwaka sasa na hakuna kitu amefaidika nacho zaidi ya kupoteza pesa. Jamaa ni student nimekua nikimshauri sana aachane na hiyo miradi ya wazungu huko Ulaya kwani hakuna anachopata zaidi ya kuunguza account every now and then.

Jamaa ana hali mbaya sana kwa sasa ameuza kila kitu hana hata nguo ya kuvaa/kiatu lakini pesa yote ya boom + anayotumiwa kwa matumizi mengine anatumbukiza FOREX. Jana nimeongea nae aachane na hii mishe naona kama ameanza kunichukia flani, daily yupo YOUTUBE anafatilia videos about FOREX, ana groups za Telegram & Whatsapp zaidi ya 50 za mambo hayo ya FOREX na nyingi analipia. Kila nikimpa ushauri ananiona kama mimi ni kikwazo cha maisha yake, he keeps on saying anzia January nakua tajiri namwambia kirahisi hivo anasema we tulia hizi hela ni za bure lazima nizipate.

Then he keeps on saying HELA za FOREX zipo tuu na ni zabure kabisa eti mimi ndio mshamba sizitaki hizo ela za bure. FOREX complications ni nyingi sana, daily ananitajia watu wa uko SOUTH AFRICA waliofanikiwa, namjibu waliofanikiwa ni mmoja kwa milioni Ila haelewi. Bado sijajua aliemdanganya aingie kwenye hiyo mishe ni nani.
Ukimwambia FOREX ni mchezo kama UPATU anamind sana eti nisidharau biashara za watu.

Wakuu nimpe ushauri gani huyu best yangu maana anaangamia mbele ya macho yangu and sitaki kuona hilo linatokea.

Best regards,
Mbao Ya Chuma.
Mzabue booonge la kofi la Usoni, akili ikae sawa
 
Smart money sio kwa ajili ya kila mtu...Shaffii Dauda anapiga pesa ndefu kwa betting tu
Ashawahi kukuonesha akaunti zake za betting

Au unazungumzia kuwatangazia makampuni ya betting

Baada ya nyie akina kajamba nani kuchaniwa mikeka yenu
 
kama sijakosea na wewe ni mwanafunzi wa Ontario.
Forex ni wizi, ukisha deposit pesa yako, ukianza kutrade tu mapicha picha ya red yanaanza ukija kushtuka pesa imeshateketea kwenye account, hii ni kamari ya matajiri kwa walalahoi wa nchi masikini kama tanzania ni kujiongezea umasikini tu
 
Huwa simshawishi mtu yeyote aingie kwenye hii biashara

Maana huwa sipendi malalamiko kama yanayoletwa humu .

Mtu akiona hii kitu inamfaa na kaifanyia utafiti akaifanye mwenyewe kwa bidii na juhudi zake

Akipoteza atakuwa Hana wa kumlaumu

Binafsi naifanya niseme tu Kuna faida na hasara pia kama zilivyo biashara zingine .

Huwezi ukawa unakula tu kila siku Kuna wakati unakosea analysis na unapaswa kukubali loss .

Kwa mentality za kitanzania aisee ngumu Sana kuielezea FX mtz akauelewa hasa baada ya matukio ya upatu kama deci,forever living ,qnet nakadhalika

Nashauri vijana msikurupukie vitu kwa hearsay za mitaani

FX inataka watu smart, emotionally,mentally ukiwa weak haikufai sababu flaoating na volatility no kuuuubwa Sana hi ni kutokana na transaction zinazofanyika na big players kama banks,hedge funds nakdhalika

Watu wajanja siku hizi hata Forex hawafanyi Sana wako kweny stocks,indices,metals Huko ndio Kuna hela za uhakika na loss za kibabe

QOur slogan :Trading forex is very risk you may loose your capital .

Forex is not for everyone [emoji23]
 
Forex is not for every one jambo la kwanza
Jambo la pili forex is the game of principles
Jambo la tatu forex is a business of discipline + knowledge

*Jamaa yako kupata hasara kwenye forex haimaanishi kwamba forex ni kitu kibaya pia hata biashara zingine za kawaida watu wanapata hasara, naona watu wengi mnaitolea povu kitu ambacho ni dalili za kuwakatisha watu wengine tamaa come on acheni kujikuta mnajua kila kitu

Forex this game is real but very trick, lakini mtu ukiwa na knowledge, discipline, business plan yako na ukaiheshimu una stick nayo lazima ikupe faida
Na kitu cha mwisho hii sio biashara ya kukupa utajiri ndani ya siku mbili au siku moja forex ni long term investment inahitaji muda wako, heshima na nidhamu ya hali ya juu.
 
Usimkatishe tamaa.
Mimi nimeacha kazi nilikuwa meneja mauzo Vodacom kanda ya kaskazini nikaaacha kazi.
Nimejenga sasa nina usafiri nimeoa....
Ninaishi maisha yangu ninayotaka.
Huyo anakosea mahali anichek nimtumie vitabu 9 tu akimaliza kusoma atafaidi.
Tatizo letu hatutaki kusoma...tunapenda kutumia maarifa ya waliosoma huko kwenye magrup.
Kuacha kaz kama hyo si sawa na kujamba ushuz bro,acha uongo,pumbaf,huna jeur hyo labda kama meneja vodacom wa vibanda vya mpesa
 
Akina buffet wanapata hela bila kuwa na kampuni inayozalisha nao ni wenye dhambi

Dini zinawaendesha Sana ndio maana mnabaki maskini

Teknolojia imekupitua kushoto

Ahsante umri wangu miaka 58 nilizaliwa na kukulia uchagani niko kijiji Cha Kapangalamsenga Katavi ,ni kweli ninaweza kusema mimi si maskini hata kidogo.Mimi mjanja hapa wananikubali asilimia mia moja.Karibu kwenye ujasiriamali kwenye sekta ya Kilimo
 
Mbao ya chuma, Kama kweli anaamini katika anachokifanya atafanikiwa, usimkatishe tamaa bado yuko kwenye learning curve ambayo inaweza ikachukua hata miaka mitatu, usimkatishe tamaa!!

Binafsi imenichukua miaka miwili hadi kuanza kuona consistency kwenye game, lakini kabla ya hapa nimechoma sana akaunti zisizo na idadi lakini nilijipromise kuto kukata tamaa na sasa namshukuru Mungu naona matunda ya forex.

Nimedevelope methodology au strategy yangu na nimeipa jina LA MONEY COMETH CODE(MCC) kwakweli naona fedha zikija kupitia hii strategy siyo kwangu tu Bali na kwa wanafunzi wangu wachache waliochagua kuiamini!!!

Unaweza ukamwambia acheki uchambuzi wangu wa soko kabla na baada kupitia page yangu ya Instagram yenye la, (sullam_Fx).

Karibu.
 
Back
Top Bottom