Nina mashaka huyu mtoto si wangu, ushauri wako wa muhimu mwana MMU!

Nina mashaka huyu mtoto si wangu, ushauri wako wa muhimu mwana MMU!

Usichokijua kuhusu wanawake ni kuwa "wanawake hawapendi kuonewa huruma"
1. Mtu ameenda kijijini ana mimba, hajakutafuta
2. Amejifungua, sidhani km ulimpa mtoto jina. Hajakutafuta
3. Ameolewa Kenya. Hajakutafuta
4. Amerudi mtaa uliopo. Hajakutafuta
5. Wewe ndiyo umelazimisha, narudia tena umelazimisha, narudia tena umelazimisha kumuona mtoto na alikubali kwa shingo upande.
Huyo mwanamke hana mapenzi na 100%. Wewe ndiyo unajipendekeza
Agreed
 
Kimbia kaka tena kimbia sana huyo dada atakuharibia maisha

Tafuta laki 2 mpe yule mama then mwombe akufanyie uchunguzi na upelelezi atakupa majibu ya kweli
 
Mwambie unataka kufanya DNA test then omba ifanywe na Lancet vipimo wanatuma Nairobi majibu yatakuja ya ukweli
Na uhakika ukitaja kupima binti atakimbia
 
Kasheshe uliianzisha mwenyewe kwa kufanyakosa la kiufundi hapo eti inawezekana"Hii mimba ni ya kwangu" Kusex na mwanamke hakukupi assurance ya kua baba wa mtoto hata kama ni mkeo. Ili mwanamke umpe mimba labda awe mjinga au aamue yeye nwenyewe ila huyo binti seeems alikua mjanja.

So wewe ulishoboka-ea ujauzito usiokuhusu kisa ulilala nae binti akaona atambae na biti ili siku zisonge, Pole kwa machungu na siku nyingine usirudie kosa hilo. Baba wa Mtoto anayemjua ni mama na sio wewe ujipe Authority ya kusema hii mimba yako Unless there's strong Controversy-ies
Noma sana!
 
Kanishangaza sana [emoji28]
Kosa kubwa nililofanya ni hili, mimi mwenyewe nilijiona mpuuzi sana, lkn kwa mazingira yake alihitaji huruma, miaka chini ya 20, kwanza tuu nilikua nawaza vipi anaweza himili vyote, kumbe nae anavyake.

Laana za wanawake nani anazitaka!! sema ndo hivyo ishakuwa somo!! ila shukran kwa mliochangia uzi huu kwani nimempata mpaka daktari wa Kenya atakaenisaidia kwa umakini, na ushauri wa kutosha!
 
Sijaelewa hapo kumwambia huyo maza kua mimba ni yako!! Uliwaza nini mpaka ukajitosa namna hiyo au ulimkuta bikra ndgu yangu?

Hilo ulijitakia mkuu, na nahisi mtoto hakua wako ndio maana hakukutafuta tena. Pole sana mkuu, ila kapike dna ukishindwa basi usiishi na huyo kiumbe we hudumia mtoto tu.
 
So sisi sio huyo dada pole .
Kingine mshauri kimaungo nitakuoa ml 5 ukiwa mkweli mtoto ni wangu??
Hata ml 10 sema tu nitakopa .
Akikataa kusema mpige mkwara naenda polisi atasema.
Kitu kingine mwambie naenda kwa mganga kucheki hakuna dna tosha kama hiyo
 
Sio mtoto wako kama ulikuwa na uwezo wa kumpa M3 mtafute huyu mtoto mchukue hata unywele ama nguo zake kampime. Hapo kimbia tu. Mwanamke anatakiwa awe wa kwanza kumtafuta mzazi wa mtoto wake.
 
Mimba ulijipa mwenyewe, hukupewa yaan ulishoboka so unavuna ulichopanda japo kwa kusoma andiko lako unaonekana una roho nzuri na ka huruma flani, hayo mengine pambana nayo kiume au laah uatakua Social father nayo sio mbaya
 
Mpeleke mtoto maabara jifanye unaenda kucheki afya ya mtoto na huyo mama wa mtoto....mkifika muombe mhudumu afanye( blood grouping) ya kwako mama na mtoto...group la damu lazima lifanane na la baba vinginevyo umepigwa....huo ni mwanzo tu
Shule uliosoma itaje ili tujue ukilaza ni wako wa kuzaliwa au ni walimu wako, hii ya kufanana blood group ulisomea wapi? Usiabishe ukoo
 
Assalam mwana MMU, pole na majukumu ya kimaisha.

Niende moja kwa moja kwenye mada, mwaka 2015 baada ya kuhitimu elimu nilanza harakati zangu kitaa, nilitoka mkoa niliokulia na kuja kanda ya ziwa Mwanza.

Maisha ya kuwa mwenyewe, sijaoa, nikajikuta nakula kwa mama mmoja alikua na sehemu ya kuuzia chakula jirani na napoishi.

Miezi kadhaa baada ya kuzoeleka pale alikuja binti pale mfanyakazi, alikua mchangamfu sana, akawa ndie mtoa huduma kwetu.

Kitabia mimi si mtu wa kufahamiana na watu haraka sana, lakini kwa ule uchangamfu nikakuta nishazoeana nae. Hakuwa binti mkubwa sana kiumri, hata 20 kipindi hicho alikua hajafikisha bado.

Kuna kipindi nilianza kuwa nabanwa sana na majukumu, narudi nyumbani usiku sana, nikapunguza kwenda pale kula, siku moja nikakutana na yule mama, akanishauri kama nimebanana sana wale mabinti watakuwa wanakuletea chakula nyumbani, niliafikiana nae na chakula kikawa kweli kinaletwa nyumbani.

Tatizo lilianzia hapa, kwani mazoea ya yule binti yalizidi sana, japo nikiri sikuwahi kumtamkia swala lolote la kuwa mpenzi, kuna siku nilikua sijatoka nafanya usafi nyumbani, mida ya jioni, ghafla binti akaja na chakula, ilikua mapema sana, alivyofika utani ukaanza mambo mengi, nikajikuta tayari nimesex pasipo kupanga, na ukizingatia ni muda mrefu nimetoka nyumbani ilikua rahisi sana kushawishika (wanaume wanajua).

Wiki kadhaa kupita yule binti aliombwa na yule mama ahame aende kwa mwanae akamsaidie kazi za nyumbani, alivyofika kule akagundulika ni mjamzito!

Kasheshe ilianzia hapa, binti alikataa kata kata kusema, lakini nafsi ilinisuta, ikabidi nimwambie yule mama ukweli, nikamvuta pembeni, nikamweleza, "mama, inawezekana pengine huu ujauzito ni wa kwangu, maana nimewahi sex na huyu binti" mama aliniuliza sasa tunafanyaje? nikamwambia asiutoe nitaulea, kazi ikaanza!

Yule binti kumbe alikuwa mwanafunzi ametoroka kwao, na ameacha shule, kazi nyingine ikawa hapo! japo yule mama alisema tupambane tuu tuone itakapoishia, akampiga mikwara yule binti nae akae kimya asiseme kwa mtu!

Nikawa na hudumia, sasa mabadiliko ya ujauzito, binti akawa anafanya vituko, kuna siku halali nyumbani anasingizia alikua kwangu, kuna kipindi akapoteza vyombo vya watu masufuria makubwa aliyaacha nje usiku yakabebwa ikabidi nilipe, mambo yalienda mpka yule mama akatuchoka ikabidi anishauri nimrudishe kwao!

Basi nikaongea nae uzuri alikubali, nikampa fedha za kutosha nikamsindikiza akaondoka, alivyofika nyumbani tuu, akawa hapatikani tena hewani (anadai alipoteza simu).

Muda ulienda, nimefuatilia sana toka 2016 mpaka nikakata tamaa mwezi huu wa sita 2022 yule mama akanipigia usiku akaniambia yule binti amekuja yupo kitaa, nilijawa na shauku na furaha sana.

Nikamtafuta hatimae tukaonana, tulikaa sehemu, akanihadithia vingi, ikiwepo kupoteza simu, na jinsi alivyojifungua, akaenda Kenya akaolewa, huko akampata mtoto mwingine, wakaachana na huyo mume na sasa ndo amekuja huku Mwanza kunitafuta.

Nilimpa pole nyingi, na nikamuuliza anataka nini kutoka kwangu, akadai anataka TUISHI WOTE, nikamwambia sahivi nina mchumba, na nishamtambulisha nyumbani, nitafanyaje? akatulia, nikamwambia nimtafutie 3milion afungue biashara zake, lakini mtoto anipe akaanze shule.

Ah, nilivyomwambia swala la mtoto kunipa alibadilika, akasema haiwezekani, huyo mtoto ametoka nae mbali, hawezi kunipa alelewe na mama mwingine, kama ninamtaka mtoto tuishi wote yeye na wanae hao wawili sasa!

Muda ulienda nikamwambia aniletee mtoto nimwone kwanza, aligoma, nikamsisitiza sana, mwisho akakubali japo kishingo upande sana, nilianza kupata mashaka hapa!

Mtoto alivyoletwa doh, aisee hata kitu kimoja sijafanana nae, nilijitahid sana kujikaza, nisiulize, akawa kama ameshtuka hivi, akawa anaongea maneno mengi, mara mtoto wako huyu, mnafanana sana nywele sema nimemsuka hutaona, kidogo mwanao huyu ona alivyokuzoea haraka!

Akawa anamwambia mtoto mwite baba, mambo yalikua mengi, nikampiga mtoto picha tukaagana, nilipatwa na hofu sana, nikaona hapa naenda kupigwa, halafu kibaya dogo anafanana sana na kuna jamaa namfahamu!

Dogo hataki kuachiwa na mama yake, hata dakika moja!

Samahani sana kwa urefu wa story, lakini walau nimeamua kutoa matukio ya muhimu, ili niweze kupata ushauri mzuri, nifanyaje??

Natanguliza shukrani!
Kwa maelezo yako haya kuna uwezekano wa asilimia 90 kuwa umepigwa, japo hizo 10 pia zina nguvu ya kubadili hisia zilizopo sasa...

Kuna watakao kwambia ukampime DNA, well and good, Ila kuwa na uhakika ukienda kumpima utajipiga kitanzi cha kudumu hata kama ukweli mtoto sio wako!

Ofisi ya mkemia kwa sasa hata ukipeleka sampuli ya mtoto asiye wako kabisaaa, as long as inahusisha parentage, nakuhakikishia utaambiwa ni wa kwako (hii imefanywa makusudi kunusuru ongezeko la watoto wa mtaani),
Kwa experience, rafiki yangu alisafiri kikazi kwenda Ghana, alikaa huko kwa miezi minne, aliporudi akakuta mkewe ana ujauzito, na kwa maelezo yake alipokuwa anasafiri mkewe alikuwa Menstrual Period!

Jamaa alivyorudi akakomaa kutaka kujua mimba ni ya nani mke akasema ni kwake, hakubadili msimamo mpaka alipojifungua, jamaa mwezi wa 1, 2022 akaamua kufanya DNA test, majibu yakaja kwamba mtoto ni wa kwake, japo ukiwaona watoto wake wengine na huyo mwingine ni tofauti!

Ukitaka kupoteza muda na pesa zako bure nenda ofisi ya mkemia kapime then utarudi hapa utusimulie!

Hatua na gharama za kupima!
Kila sampuli moja inapimwa kwa sh.100,000/= na lazima uende baba,mama na mtoto (hapo itakuwa 300,000/=)

Kuna gharama za wakili (kama haujapita ustawi wa jamii), hizi zinategemea na mtakavyokubaliana, kuna wanaofanya kwa 200k na wengine zaidi ya hiyo!

N.B regulations zinazoongoza upimaji na utoaji majibu ya vinasaba yameelekeza wazi kwamba mtoa majibu LAZIMA AZINGATIE MASLAHI YA MTOTO!
 
Bro, huhitaji DNA. Mtoto sio wako. Ushauri wangu, kama uwezo unao msomeshe mtoto umpunguzie mzigo mama mtu. Kama huna muahidi kumpa msaada mambo yakikaa vzr. Mfanyie uungwana bila kujiumiza mwenyewe
 
Gharama ya DNA ni sh. ngapi, hakuna taratibu za kufuata?
Tanzania Ukicheki DNA hata kama sio wako utaambiwa wako

So kama uko radhi kuteketeza laki moja yako ni wewe tu wala sio gharama kubwa unapima ofisi ya mkemia mkoa uliopo kwa kibali kutoka mahakamani

Lakini kila kitu kina loophole bado unaweza ukawashinda wasiweze pika majibu
 
kwaza pole sana! Ulipokosea ni uliposema unahisi mtoto ni wako.. Ungesubiri huyo bonti amtaje baba wa mtoto mwenyew
 
Back
Top Bottom