Kimsingi mpaka sasa wale makomandoo watatu Khalfani Bwire,Adamoo na Mohamed Ling'wenya ni innocent guys, ni raia wema kwa ushahidi wa Lut Denis Urio ambaye ndiye shahidi muhimu kuliko wote.Amethibitisha kua aliwaita kama Raia wema, aliwaita kwenda kufanya kazi ya Ulinzi, na alisema aliwaomba wakiona kuna dalili za kihalifu wampe taarifa na mpaka wanakamatwa hawakuwahi kumpa taarifa za kihalifu. Hawa makomandoo walipigwa na kuonewa bure waachiwe huru hakuna namna.
Tukirudi upande wa Mhe Mbowe , Denis Urio anakiri kabisa kuwa hakuna ushahidi wowote wa picha, Video wala audio au vifaa vyovyote alivyoona vilikuwa vitumike kufanya ugaidi...isipokuwa kuna sms chache hapo Denis Urio yeye akiomba pesa kwa Mbowe ili awakutanishe wale vijana wanne na ile ya Muamala ambayo ni ya kawaida kabisa.Mbaya zaidi hakuna seme hata moja inayothibitisha Ugaidi popote. Amebaki na maneno ya Ooh alisema titanaenda kulipua vituo vya mafuta na kukata magogo, uthibitisho wa matendo hayo hakuna hata punje. Si angemrekodi Homeboy wake akiongelea hayo matukio ili kuwepo na ushahidi?
Yaani kwa Teknolojia ilivyokua hivi sasa karne ya 21 ofisi kubwa ya DCI inakosa device yeyote ya kumrekodi Mbowe akiongeleo Ugaidi? Basi angemrekodi hayo mazungumzo ya simu. Hii tamthiliya tamu sana 🤣🤣🤣🤣🤣
Haya sasa ugaidi wa Mbowe upo kwenye nini?
Kiongozi mwenye walivyosema anapangiwa njama kuuliwa inasemekana ni Sabaya ana hukumu ya Ujambazi yupo jela. Kamba ingekuwa kweli kwani kumdhuru jambazi ni kosa?