Maswali yangu ni kama ifuatavyo:
1)Tukiachana na blah blah faida inayopatikana kwa kuukimbiza mwenge ni nini hasa baada ya mabilioni kuteketea kwenye ukimbizaji wa mwenge ni kitu gani kinapatikana.
2)Mwenge huwa unahifadhiwa wapi(Mkoa) na mahali gani(jengo)?
3)Kiongozi wa mbio za mwenge huwa anachaguliwa kutoka wapi?
4)Je mwenge ukianza kuzunguka ni kweli hauzimwi?
5)Kuna uvumi nimekuwa nikiusikia wanaokimbiza mwengi huwa wanadanji uvumi huu unatokana na nini?
6)Mwenge unapokuwa sehemu kuna takribani watu wanne au watano wanatengeneza duara kuuzunguka mwenge kwa karibu kiasi cha kuvuta ule moshi na wanakuwa hapo kwa muda mrefu wakiwa wameunganishana je maana yake ni nini na je ule moshi wanaouvuta kwa muda wote ule hauwezi kuwaletea madhara?
7)Je mwenge ni mmoja huo huo miaka yote au huwa unatengenezwa kila baada ya muda fulani?
8)Nini asili ya mwenge na ulianza rasmi lini na kwa nini unahusishwa na uchawi?
Nadhani maswali haya yanatosha pengine nikipata majibu ya maswali haya kutoka kwenu nitaongeza maswali mengine
Huwa nauona mwenge kama ni kitu ambacho kinaabudiwa kama ambavyo masanamu yanavyoabudiwaga vile watu wanavyoukusanyikia nawaona kama wapo kwenye ibada kwa mungu Tamuzi au baphomet
1. Faida: Kukagua miradi mbalimbali iliyojengwa kwa fedha za umma na ile iliyotokana na michango ya Wananchi. Lengo kuwakumbusha watendaji kutolala kwani Mwenge utawaunguza. Pesa zinazohudumia Mwenge wa Uhuru zinatokana na michango ya hiari kutoka kwa Watanzania Wazalendo. Serikali inatoa bajeti ndogo sana ya Mwenge.
2. Baada ya kuzimwa, Mwenge wa Uhuru unahifadhiwa kwenye Makumbusho ya Taifa.
3. Ni jukumu la Rais wa JMT kumchagua Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru akishirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambao nao huchagua Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wengine kufanya wawe Sita Kitaifa.
4. Literary, hauzimwi, lakini linapokuja suala la kuongeza mafuta na kuufanyia services ndogo ndogo, unazimwa ila kwenye sehemu maalum.
5. Kufa ni kwa binadamu yeyote, anayekimbiza na hata ambaye hajawahi kuuona licha ya kuukimbiza wanakufa. Wapo ambao waliwahi kufa, lakini wapo wengine wapo hai hadi Sasa. Mfano, Kamanda Jordan Rugimbana na Mzee Sukwa Said Sukwa kutaja wachache.
6. Wanaouzunguka mara nyingi ni askari (FFU), Skauti au Vijana Shupavu kutoka UVCCM, ila LAZIMA wawe wameandaliwa kwa kazi hiyo. Lengo ni kuukinga na upepo usizimike.
7.Kila mwaka unatengenezwa mpya kwa ajili kuukimbiza kwa mwaka husika. Mwl. Nyerere alikuwa na vifimbo zaidi ya mia, lakini watu waliamini ni kamoja tu! Ahahahahaha!!!
8. Ulianza rasmi mwaka 1961 pale Ndugu Nyirenda alipouweka juu ya Mlima Kilimanjaro. Asili yake ni kutokana kauli ya hekima kutoka kwa Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliposema, " Sasa tunakwenda kuwasha Mwenge Ili umurike ndani na nje ya mipaka yetu.....!" Hakuna Imani za kishirikina wala nini ingawa huwezi kuzuia waja kunena!
Naamini kwa majibu yangu hayo umepata uelewa kidogo kuhusu Mwenge wa Uhuru. Karibu kwa maswali mengine!