Nina maswali kadhaa kuhusu mwenge

Nina maswali kadhaa kuhusu mwenge

Mtafute omary mnyeshani ameuelezea kwa kina sana na jinsi unavyofanya kazi kichawi akiwa mshiriki wa kuitambikia nchi mkoa wa Lindi na eneo analijua
 
Hakuna faida y maana ni ujinga ujinga tu, tunapoteza pesa kodi zetu kwa ujinga ujinga tu.
 
JPM alifuta hadi sherehe za Uhuru lakini hakuthubutu kufuta Mwenge

ni bora Muungano uvunjike kuliko kufuta Mwenge

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
 
Uchawi wa kuzindika nchi ulianza mapangoni bagamoyo baada ya wazee kumuomba shetani awasaidie kuwafukuza wakoloni.
Shetani akawaambia wakoloni wataondoka lakini mtakuwa masikini.,wazee wakaona sawa bora wananchi wawe masikini lakini wakoloni waondoke.
Wakapewa mwenge baada ya kukubali masharti ili kuwapumbaza watu
Hahaha
 
1. Faida: Kukagua miradi mbalimbali iliyojengwa kwa fedha za umma na ile iliyotokana na michango ya Wananchi. Lengo kuwakumbusha watendaji kutolala kwani Mwenge utawaunguza. Pesa zinazohudumia Mwenge wa Uhuru zinatokana na michango ya hiari kutoka kwa Watanzania Wazalendo. Serikali inatoa bajeti ndogo sana ya Mwenge.

2. Baada ya kuzimwa, Mwenge wa Uhuru unahifadhiwa kwenye Makumbusho ya Taifa.

3. Ni jukumu la Rais wa JMT kumchagua Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru akishirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambao nao huchagua Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wengine kufanya wawe Sita Kitaifa.

4. Literary, hauzimwi, lakini linapokuja suala la kuongeza mafuta na kuufanyia services ndogo ndogo, unazimwa ila kwenye sehemu maalum.

5. Kufa ni kwa binadamu yeyote, anayekimbiza na hata ambaye hajawahi kuuona licha ya kuukimbiza wanakufa. Wapo ambao waliwahi kufa, lakini wapo wengine wapo hai hadi Sasa. Mfano, Kamanda Jordan Rugimbana na Mzee Sukwa Said Sukwa kutaja wachache.

6. Wanaouzunguka mara nyingi ni askari (FFU), Skauti au Vijana Shupavu kutoka UVCCM, ila LAZIMA wawe wameandaliwa kwa kazi hiyo. Lengo ni kuukinga na upepo usizimike.

7.Kila mwaka unatengenezwa mpya kwa ajili kuukimbiza kwa mwaka husika. Mwl. Nyerere alikuwa na vifimbo zaidi ya mia, lakini watu waliamini ni kamoja tu! Ahahahahaha!!!

8. Ulianza rasmi mwaka 1961 pale Ndugu Nyirenda alipouweka juu ya Mlima Kilimanjaro. Asili yake ni kutokana kauli ya hekima kutoka kwa Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliposema, " Sasa tunakwenda kuwasha Mwenge Ili umurike ndani na nje ya mipaka yetu.....!" Hakuna Imani za kishirikina wala nini ingawa huwezi kuzuia waja kunena!

Naamini kwa majibu yangu hayo umepata uelewa kidogo kuhusu Mwenge wa Uhuru. Karibu kwa maswali mengine!
-kama Mwenge unakagua miradi mbalimbali ya Maendeleo, Nini kazi ya Controller and Auditor General? , Nini kazi ya TAKUKURU?
  • Kuhusu michango mnawachangisha Watumishi wa Umma kwa Lazima,
  • Mwenge unamulikaje nje na ndani ya mipaka ya nchi yetu? huoni hapo ni Uongo tu
 
Mwenge ni tambiko kuu la taifa hili, na mpaka mwenge huo unawaka watu wengi walipoteza maisha.
Ulikuwa mpango ulioshirikisha watu maalum nchi nzima, kuna wengine (hao maalumu) walikubali kufa Ili mwenge uwake, haikuwa kazi rahisi kuwasha mwenge.

Hakuna siku mwenge huo utazimwa, labda Dunia ifike mwisho na iwapo siku itatokea utazimwa tu! shughuli ya nchi nzima itakuwa imeishia hapo.( in mzee wa jambia's voice)
 
• Kila mtu ana kazi yake. CAG ana kazi zake na mipaka yake. Hali kadhalika na Mwenge wa Uhuru pamoja na TAKUKURU ni hivyo hivyo. Hakuna anayemuingilia mwenzake na ndio maana hujawahi kusikia upande wowote ukimlalamikia mwenzake.

• Bajeti ya kuukimbiza Mwenge wa Uhuru niishaizungumzia inapatikanaje. Sio suala langu kwa wewe kuwa na mtazamo tofauti.

• Nimekariri kauli ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Kama ni uongo hayo ni maoni yako, kwani maoni ni "relative".
 
mwenge wanaabudu mizimu na sheitani ndio asili yake na inapumbaza akili
kila atakae uona au kuusogelea ataksahau mungu kabisa
 
Watu wengi huwa wanakuja mjini kwa mbio za mwenge

Ova
 
Mwenge ni mmoja
Wakimbiza mwenge huwa hawafi
Mkuu mwenge upo zaidi ya mmoja ila ni kwa siri sana picha linaanza katika kila mbio huwa kuna mienge miwili kwa maana mmoja ukileta shida mwengina unachukua jukumu haraka hii nimeipata kwa mwanajeshi mmoja mstaafu maeneo ya mwananyamala aliwahi kuwa mshiriki mmoja wapo mwaka 2002
 
Mwenge ni tambiko kuu la taifa hili, na mpaka mwenge huo unawaka watu wengi walipoteza maisha.
Ulikuwa mpango ulioshirikisha watu maalum nchi nzima, kuna wengine (hao maalumu) walikubali kufa Ili mwenge uwake, haikuwa kazi rahisi kuwasha mwenge.

Hakuna siku mwenge huo utazimwa, labda Dunia ifike mwisho na iwapo siku itatokea utazimwa tu! shughuli ya nchi nzima itakuwa imeishia hapo.( in mzee wa jambia's voice)
[emoji2960]
 
Sijui hujanielewa nataka kujua unapoanza kuzungushwa kuna wakati unazimwa na kuwashwa au ukiwashwa hauzimwi mpaka umalize kuzunguka nchi nzima
Huwezi kuupandisha ule moto wa kishirikina ndani ya ndege, lazima uzimwe.
 
Maswali yangu ni kama ifuatavyo:
1)Tukiachana na blah blah faida inayopatikana kwa kuukimbiza mwenge ni nini hasa baada ya mabilioni kuteketea kwenye ukimbizaji wa mwenge ni kitu gani kinapatikana.

2)Mwenge huwa unahifadhiwa wapi(Mkoa) na mahali gani(jengo)?

3)Kiongozi wa mbio za mwenge huwa anachaguliwa kutoka wapi?

4)Je mwenge ukianza kuzunguka ni kweli hauzimwi?

5)Kuna uvumi nimekuwa nikiusikia wanaokimbiza mwengi huwa wanadanji uvumi huu unatokana na nini?

6)Mwenge unapokuwa sehemu kuna takribani watu wanne au watano wanatengeneza duara kuuzunguka mwenge kwa karibu kiasi cha kuvuta ule moshi na wanakuwa hapo kwa muda mrefu wakiwa wameunganishana je maana yake ni nini na je ule moshi wanaouvuta kwa muda wote ule hauwezi kuwaletea madhara?

7)Je mwenge ni mmoja huo huo miaka yote au huwa unatengenezwa kila baada ya muda fulani?

8)Nini asili ya mwenge na ulianza rasmi lini na kwa nini unahusishwa na uchawi?

Nadhani maswali haya yanatosha pengine nikipata majibu ya maswali haya kutoka kwenu nitaongeza maswali mengine

Huwa nauona mwenge kama ni kitu ambacho kinaabudiwa kama ambavyo masanamu yanavyoabudiwaga vile watu wanavyoukusanyikia nawaona kama wapo kwenye ibada kwa mungu Tamuzi au baphomet
Nakala kwa Mohamed Said
Kupitia uzi wa mshanar jr!

Mwenge asili yake ni huko kuzimu KWA malaika waliolaaniwa huko yaani mizimu ya nchi na wazee!!

Mwaasisi wa mwenge ni mchawi mmoja aitwaye forojo ganze MIAKA hiyo baada ya tz kupata uhuru!!

Inasemekana eti NYERERE alikua ananusurika sana kupinduliwa akawaomba wazee wa kiswahili mashekh wamsaidie ndipo walipoenda huko KWA kufuata taratibu zao ndio wakauleta mwenge!!

Japo mchakato ulikost umri wa Baba wa taifa kufupishwa KWA mujibu wa uzi ule wa mshanar!!

Unatuliza watu Ili watawaliwe vizuri bila kelele!!

Source jf uzi wa mshanar Jr!
 
Sionagi hata faida yake kitu kinakimbizwa miaka nenda rudi,wauzime tu ishu nyingine ziendelee
 
Maswali yangu ni kama ifuatavyo:
1)Tukiachana na blah blah faida inayopatikana kwa kuukimbiza mwenge ni nini hasa baada ya mabilioni kuteketea kwenye ukimbizaji wa mwenge ni kitu gani kinapatikana.

2)Mwenge huwa unahifadhiwa wapi(Mkoa) na mahali gani(jengo)?

3)Kiongozi wa mbio za mwenge huwa anachaguliwa kutoka wapi?

4)Je mwenge ukianza kuzunguka ni kweli hauzimwi?

5)Kuna uvumi nimekuwa nikiusikia wanaokimbiza mwengi huwa wanadanji uvumi huu unatokana na nini?

6)Mwenge unapokuwa sehemu kuna takribani watu wanne au watano wanatengeneza duara kuuzunguka mwenge kwa karibu kiasi cha kuvuta ule moshi na wanakuwa hapo kwa muda mrefu wakiwa wameunganishana je maana yake ni nini na je ule moshi wanaouvuta kwa muda wote ule hauwezi kuwaletea madhara?

7)Je mwenge ni mmoja huo huo miaka yote au huwa unatengenezwa kila baada ya muda fulani?

8)Nini asili ya mwenge na ulianza rasmi lini na kwa nini unahusishwa na uchawi?

Nadhani maswali haya yanatosha pengine nikipata majibu ya maswali haya kutoka kwenu nitaongeza maswali mengine

Huwa nauona mwenge kama ni kitu ambacho kinaabudiwa kama ambavyo masanamu yanavyoabudiwaga vile watu wanavyoukusanyikia nawaona kama wapo kwenye ibada kwa mungu Tamuzi au baphomet
Nakala kwa Mohamed Said
Mungu kaingiaje hapo, tulielewana hakuna mungu
 
• Kila mtu ana kazi yake. CAG ana kazi zake na mipaka yake. Hali kadhalika na Mwenge wa Uhuru pamoja na TAKUKURU ni hivyo hivyo. Hakuna anayemuingilia mwenzake na ndio maana hujawahi kusikia upande wowote ukimlalamikia mwenzake.

• Bajeti ya kuukimbiza Mwenge wa Uhuru niishaizungumzia inapatikanaje. Sio suala langu kwa wewe kuwa na mtazamo tofauti.

• Nimekariri kauli ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Kama ni uongo hayo ni maoni yako, kwani maoni ni "relative".
- Mwenge wa Uhuru unaendeshwa kwa masharti ya Sheria gani? Takukuru unaendeshwa kwa masharti ya Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa ya 2007, Naot ni Katiba, public audit act nk, Mwenge wa Uhuru je?

-Bajeti ya Mwenge wa Uhuru ni kuchangisha watumishi wa Umma kwa nguvu, na serikali inachangia.
-
 
Back
Top Bottom