Nina maswali kadhaa kuhusu mwenge

Mwenge ni jadi, mila na desturi ya taifa hili, kamwe haitatokea tukaacha kukimbiza mwenge. Jiulize wewe kwanini usirudi tumboni kwa mama yako na uachane na shida na raha za Duniani 🤣🤣
Faida yake ndio hiyo tu katika kudumisha hivyo?
 
Mwenge ni kiini macho cha Serikali kwa raia wapumbav
 
Humu wamejaa wale jamaa wenye suit nyeusi na miwani mkuu
Sitaki kung'olewa meno na kucha! Ni bora niishi kwa amani niendelee na biashara yangu ya kuuza majeneza ndani na nje ya Dodoma
😂😂 Unawaogopa wazee wa kutambaa
 
Na wewe ukakubali kwa maana kwamba kabla ya uwepo wake huo mwenge hayo majanga yalikuwepo?
 
Mwenge ni jadi, mila na desturi ya taifa hili, kamwe haitatokea tukaacha kukimbiza mwenge. Jiulize wewe kwanini usirudi tumboni kwa mama yako na uachane na shida na raha za Duniani [emoji1787][emoji1787]

Kipi kilitangulia kuwepo? Mwenge ama Tanganyika / Tanzania? Watu waliishije kabla ya Mwenge kuwepo na walipata faida gani ya ziada baada ya Mwenge kuwepo?


(Husiniambie kuhusu uzinduzi wa miradi)





Mfano uliotoa hauendani.
 
Kun Historia ikonjyuma ya Pazia kuhusu Mwenge. Inasemekana yalikuwa ni maagizo ya zindikiko. Lilifanywa na Wazee baada ya Uhuru hukooo Bagamoyo!
Kuna Mwamba anaitwa Forojo Ganze ndiye aliyemwambia Nyerere aanzishe Mwenge ...na alitamka Yale maneno...Sisi tunataka kuwasha Mwenge...
Like ni zindiko kubwa sana ,Ndio maana VIONGOZI huwa wanaapa na luoazimika.kuushika Mwenge!
Huwa Kuna utani kuwa ukishika tu huo Mwenge lazima uwe ja tabia za kivhawachawa!
Kwa maelezo zaidi google Stori za Forojo Ganze!
 
Ni kama miungu ile Mungu aliyowakataza wana wa Israel kuabudu.
 
Hua nashangaa Sana serikali inavyo teketeza mabilioni ya fedha kuzungusha ule moto,

na wakati huo bado zahanati na wataalamu wa afya hawatoshelezi mahitaji, bado maji ni tatizo lisilo na ufumbuzi, umeme pia bado hautoshi, shule na vifaa vya kufundishia ni mgogoro usio na mwisho na mengine mengi ambayo hiyo fedha wanayo iharibu kwenye kuzungusha moto ingetosha kufanya, alafu fedha zenyewe bado wanakopa Kila mwaka na kuja kuziharibu,

Kwa nini ule moto usiwekwe makumbusho tuu atakae kuuona aufate makumbusho akautazame, mbona uingereza walio itawala hii nchi Wana mwenge lakini hawa potezi fedha na muda kwa kuukimbiza 🤔🤔 serikali iache kuchezea pesa na wakati zina mahitaji mengi Sana ya msingi
 
Mimi nauliza hivi huo Mwenge hua unazimwa aje?

Coz ule sio mshumaa utauzima kwa kuupuliza.
 
1. Faida: Kukagua miradi mbalimbali iliyojengwa kwa fedha za umma na ile iliyotokana na michango ya Wananchi. Lengo kuwakumbusha watendaji kutolala kwani Mwenge utawaunguza. Pesa zinazohudumia Mwenge wa Uhuru zinatokana na michango ya hiari kutoka kwa Watanzania Wazalendo. Serikali inatoa bajeti ndogo sana ya Mwenge.

2. Baada ya kuzimwa, Mwenge wa Uhuru unahifadhiwa kwenye Makumbusho ya Taifa.

3. Ni jukumu la Rais wa JMT kumchagua Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru akishirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambao nao huchagua Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wengine kufanya wawe Sita Kitaifa.

4. Literary, hauzimwi, lakini linapokuja suala la kuongeza mafuta na kuufanyia services ndogo ndogo, unazimwa ila kwenye sehemu maalum.

5. Kufa ni kwa binadamu yeyote, anayekimbiza na hata ambaye hajawahi kuuona licha ya kuukimbiza wanakufa. Wapo ambao waliwahi kufa, lakini wapo wengine wapo hai hadi Sasa. Mfano, Kamanda Jordan Rugimbana na Mzee Sukwa Said Sukwa kutaja wachache.

6. Wanaouzunguka mara nyingi ni askari (FFU), Skauti au Vijana Shupavu kutoka UVCCM, ila LAZIMA wawe wameandaliwa kwa kazi hiyo. Lengo ni kuukinga na upepo usizimike.

7.Kila mwaka unatengenezwa mpya kwa ajili kuukimbiza kwa mwaka husika. Mwl. Nyerere alikuwa na vifimbo zaidi ya mia, lakini watu waliamini ni kamoja tu! Ahahahahaha!!!

8. Ulianza rasmi mwaka 1961 pale Ndugu Nyirenda alipouweka juu ya Mlima Kilimanjaro. Asili yake ni kutokana kauli ya hekima kutoka kwa Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliposema, " Sasa tunakwenda kuwasha Mwenge Ili umurike ndani na nje ya mipaka yetu.....!" Hakuna Imani za kishirikina wala nini ingawa huwezi kuzuia waja kunena!

Naamini kwa majibu yangu hayo umepata uelewa kidogo kuhusu Mwenge wa Uhuru. Karibu kwa maswali mengine!
 
Mbio za mwenge kwenye hii karne ya 21 ni 🚮 tu na uchezeaji wa pesa za walipa kodi kwenye mambo ya kipuuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…