Nina mawazo mazuri kuisaidia nchi ila sijui nimfikishie nani

Nina mawazo mazuri kuisaidia nchi ila sijui nimfikishie nani

Andika hapa ndugu, wote wanapita hapa na hakika yatafika kwa wanaostahili.
JamiiForum ndio sehemu pekee ambapo mawazo mbalimbali mema na mabaya kuchukuliwa na kufanyiwa kazi.
Amen amen Haleluyaaa,,,,,na mimi ndio sehemu pekee ya kutolea stress.....bila shaka ndio naongoza kwa lugha chwaafuu
 
Hawawezi kukusikiliza kwavile wanaongoza kupitia vipaji kimojawapo ni cha upumbavu, upumbavu ni tabia ya mtu anayelijua vizuri jambo, (mbobezi), lakini hufanya tofauti a.k.a kujizima data

Na ndiyo maana hatuna: 'National economic system, (structure)
 
Hakuna atakaekusikiliza sababu viongozi wengi wapo kwa ajili ya kuikwamisha tanzania na sio kuiongoza kwenye maendeleo, wao kila uchwao wanawaza namna ya kuliibia tu taifa.

Kama wazo lako kuna namna watafaidika wanaweza lifanyia kazi.. Kama hakuna maslahi nao, hawata thubutu kutenda chochote.
 
Kabisa hata mimi nina mawazo kama yako ya kulisaidia Taifa,,,,,,,,kwa kufuga bata kando kando ya mto Wami na Ruvu na Ruaha na maeneo ya Rufiji pia Pangani mpaka mto Lumbegea hukoo Likuyu bila kusahau Paramawe na Miangalua mto Themii si mbaya tutafuga sababu itakuwa ni kivutio manake ni mto uatizao ktk jiji kwa pale Mkuju tutacheki noma pale Malagarasi tutawezesha vijana ambao wako tayari then tutawapelekea huduma zote eeeh naaa hapa wapi hapaaa YAA Kagera pale tumetenga kw aajili ya mabinti tu kwa upande wa mto mara tutafuga bata wale wakubwa wakubwa na kuanzisha viwanda vidogo vya Chang'aa mto Ruvuma kwa wamama watu wazima walio tayari 🙂 nao tutawapelekea huduma za kijamii.
Kama wewe ni mwana siasa wa chama pinzani utashangaa maji kwenye mabwawa hakuna hata hao samaki hawapo
 
Niletee siku hizi kuna mashindano ya mawazo mazuri unaweza pata hata $600,000 zikutoe.. Maana viongozi lazima wavae SUTI na Kununua VX kukaa nayo sio Dili..

Maana kila mtu ana maisha yake

OK , nitakutafuta Mkuu private niwasilishe .
 
Nimekuelewa hasa na Mimi hilo ndo lengo sijalenga kupata hela maana sifikirii Kama hela hata wakinipa zinaweza kuwa sawa na thamani ya mawazo yangu.
Siyo taifa la kukuza vipaji hata vya mpira havifanikiwi ndiyo maana namba 9 hatuna
 
Sasa kama unajiona ni great thinker si ungegombea kabisa uongozi kuliko kutaka ulipwe hela ili kuyatoa hayo mawazo?

Au mnasemaje ndugu zangu.
He is an Opportunity seeker
Mtafuta fursa ,kumbukeni fursa huwa hazitufuwati
 
Najua 90% ya wale great thinkers wa serikali huwa wanakuja JF kuchukua madini na kwenda kuyatumia .

Hivyo ningependa kutoa Mawazo yangu haya Kwa njia yenye kuleta maana na sio bila Mpangilio.

Mawazo yamejikita Katika kuinua Uchumi wa serikali kuanzia juu hadi katika grassroots.

Najua viongozi mnapitia hapa mtaniambia njia gani bora ya kuwasilisha mawazo yangu.
Hayo mawazo bora ukae nayo! Maana kama njia huijui inamaana hata unakoenda hukujui! Unaweza kuchangia kuinua uchumi wa nchi yako kwa kufanyakazi na kulipa kodi hapohapo ulipo alafu mchango wako ukishaonekana serikali itakutafuta yenyewe!
 
Najua 90% ya wale great thinkers wa serikali huwa wanakuja JF kuchukua madini na kwenda kuyatumia .

Hivyo ningependa kutoa Mawazo yangu haya Kwa njia yenye kuleta maana na sio bila Mpangilio.

Mawazo yamejikita Katika kuinua Uchumi wa serikali kuanzia juu hadi katika grassroots.

Najua viongozi mnapitia hapa mtaniambia njia gani bora ya kuwasilisha mawazo yangu.
Tangu lini chura kiziwi akasikia!?
 
Back
Top Bottom