Nina mawazo mazuri kuisaidia nchi ila sijui nimfikishie nani

Andika hapa ndugu, wote wanapita hapa na hakika yatafika kwa wanaostahili.
JamiiForum ndio sehemu pekee ambapo mawazo mbalimbali mema na mabaya kuchukuliwa na kufanyiwa kazi.
Amen amen Haleluyaaa,,,,,na mimi ndio sehemu pekee ya kutolea stress.....bila shaka ndio naongoza kwa lugha chwaafuu
 
Hawawezi kukusikiliza kwavile wanaongoza kupitia vipaji kimojawapo ni cha upumbavu, upumbavu ni tabia ya mtu anayelijua vizuri jambo, (mbobezi), lakini hufanya tofauti a.k.a kujizima data

Na ndiyo maana hatuna: 'National economic system, (structure)
 
Hakuna atakaekusikiliza sababu viongozi wengi wapo kwa ajili ya kuikwamisha tanzania na sio kuiongoza kwenye maendeleo, wao kila uchwao wanawaza namna ya kuliibia tu taifa.

Kama wazo lako kuna namna watafaidika wanaweza lifanyia kazi.. Kama hakuna maslahi nao, hawata thubutu kutenda chochote.
 
Kama wewe ni mwana siasa wa chama pinzani utashangaa maji kwenye mabwawa hakuna hata hao samaki hawapo
 
Niletee siku hizi kuna mashindano ya mawazo mazuri unaweza pata hata $600,000 zikutoe.. Maana viongozi lazima wavae SUTI na Kununua VX kukaa nayo sio Dili..

Maana kila mtu ana maisha yake

OK , nitakutafuta Mkuu private niwasilishe .
 
Nimekuelewa hasa na Mimi hilo ndo lengo sijalenga kupata hela maana sifikirii Kama hela hata wakinipa zinaweza kuwa sawa na thamani ya mawazo yangu.
Siyo taifa la kukuza vipaji hata vya mpira havifanikiwi ndiyo maana namba 9 hatuna
 
Sasa kama unajiona ni great thinker si ungegombea kabisa uongozi kuliko kutaka ulipwe hela ili kuyatoa hayo mawazo?

Au mnasemaje ndugu zangu.
He is an Opportunity seeker
Mtafuta fursa ,kumbukeni fursa huwa hazitufuwati
 
Hayo mawazo bora ukae nayo! Maana kama njia huijui inamaana hata unakoenda hukujui! Unaweza kuchangia kuinua uchumi wa nchi yako kwa kufanyakazi na kulipa kodi hapohapo ulipo alafu mchango wako ukishaonekana serikali itakutafuta yenyewe!
 
Tangu lini chura kiziwi akasikia!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…