Nina Mgogoro kwenye ndoa, kila pesa anayopata Mke wangu anaenda kujenga kwao. Naomba msaada

Mimi sijui Nina hormone za kiume,nimpeleke 10 home wakati nakaa nyumba ya kupanga?thubutuuu....wangeambulia 1M warekebishe kitu wanachoona kina kipaumbele
 
Mkopo ukiisha, nachukua mwingine na NITAJENGA KWETU ili siku tukiachana niende kwetu kwa raha! Wanaume mna matatizo sana ACHA MKEO AJENGE KWAO, wewe Jenga KWAKO.

Unampango wa kuachika?!
 
The last phrase says it all !!
Wanawake wengi wanapenda. Rough bad boys ukimfanyia wema wanarespond kwa kukurudishia ubaya.
 
Ndo mbaya anaweza kuingia kweny mgogoro na ndugu zake mwenyewe kweny ishu ya mirathi bora ajijenge tu mwenyewe.
 
Haya maisha unayoongelea yapo first world ambapo mume na mke wanakutana kwa kujitoa kwa ajili ya ndoa tu hakuna attachment yoyote .
Dada zetu ndoa ni daraja la kukuunganishia matatizo yake na ukoo wake , na wazazi wanasomesha watoto wa kike wakiwa wana matumaini ya kunufaika naye !
Vijana wa kataa ndoa wana hoja !
 
Kumbe kuzaa ni kujitolea ila si wajibu wa Ke tokana na kauli za Mungu kwamba "Ke azae kwa uchungu na Me ale kwa jasho"?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Kama hiyo nyumba aliyotia 47 mil ni yake halafu wala haitumii na anakatwa kwenye mshahara ! Huo ni zaidi ya ujuha!
 
Kama hiyo nyumba aliyotia 47 mil ni yake halafu wala haitumii na anakatwa kwenye mshahara ! Huo ni zaidi ya ujuha!
Mfano kwa mkopo wa million 47 mpaka aje kumaliza mkopo sio leo😅😅..

Asikwambie mtu raha ya maendeleo ya kifamilia yafanyike mapema ndani ya miaka 5 au chini mna nyumba tayari ,watoto washakuwa angalau.
 
[emoji120] The decent Woman.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Acha roho mbaya mkuu, yani unajisikia vibaya mtu akimsaidia mama yake? Vipi wewe ungejisikiaje kama ulikuwa unamjengea mama yako halafu yeye akakataa? Huyo ni mama yake na wewe umesema ni mzee sasa uanataka mzee wake akaishi wapi?
Ushasema mwenyewe kuwa katika ndugu zake yeye ndiye mwenye uwezo sasa asipomsaidia mam yake atamsaidia nani?

Nyie wanaume wa hivi ndio mana wanawake wanaficha vipato vyao, hapo ilitakiwa huyo mama asikwambie kama kapata mkopo kazini kwao kwa hivyo usingejua nani kamalizia..ndio mana wanawake wanakuwa wasiri kwa vipato vyao..

Unakasirika kwa sababu tu kamsaidia mama yake na kakushirikisha hakufanya siri; je angemhonga mchepuko ungefanyaje? wewe ndio haustahiki kuwa na huyo mwanamke na wewe ndio una matatizo..

halafu acha kumsimanga dada wa watu eti umemsomesha, unamsimanga kwa sababu kamjengea mama yake? angemjengea mama yako ungemsimanga? angekuchit je ingekuwaje..
 
Ila nyie wanaume hamueleweki, wakati ule nikipata kale ka mshahara ka miaka ile nilikuwa naweka mezani hela inapangiwa bajeti,

Kuja kushtuka mtaa wa tatu keshazaa watoto wawili.

Sometimes mnaboa
 
Duu umewachoka haswa wanawake
* Ever ndiye Kigeugeu bustanini Eden.

* Delila ndiye Kigeugeu kwa Samsoni.

* Mke wa Ruthu ndiye Kigeugeu alipogeuka nyuma kuangalia Sodoma na Ghomora akikaidi agizo la Mungu na kuwa nguzo ya chumvi.

* Mke wa Ayubu ndiye aliye Kigeugeu kwa Mumewe hadi alimtaka Ayubu amkufuru Mungu.

* Mke wa Mfalme Potifa ndiye Kigeugeu alipomtamani Yusufu azini naye kisha alimsingizia Yusufu alitaka kumbaka baada ya Yusufu kumkatalia.

Mifano mingi mno, mingine utaongezea Mama.

Me tumwombe sana Mungu atujalie hekima ili tuishi na Ke kwa akili.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Upumbavu wako ulianzia hapo. Huyo mkeo alishasoma ujinga wako mapema sana. Biblia imeandika mke ataambatana na mkewe na watakuwa mwili mmoja. Au hiyo biblia yako imesema mke ataambatana na kaka zake? Kutumia 47m ya familia kujenga kwao ni uhuni mkubwa kwa karne ya 21. Huyo mkeo ni mbinafsi mwenye tuzo ya Nobel kwenye ubinafsi. Ni shetani katika sura ya binadamu. Haya mambo yapo sana kwa watoto wa kike. Binafsi ilibidi nimwambie mdogo wangu wa kike aache kiherehere kujifanya anasaidia nyumbani bali awe bize na mumewe. Aliacha na sasa hivi wana maendeleo. Pole sana mkuu ila mwamuzi wa mwisho ni wewe kwenye hilo jambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…