Kunywa maji kwanza upunguze presha maana maneno yanakutoka hata kilichoandikwa hujaelewa.
1. Acha kukariri mimi wala sio mwanaume ni mama tena mwenye watoto wengi wa kiume na wa kike.
2. Baba ni nguzo ya kiuchumi ya familia among other things, lakini mfumo wa maisha umebadilika baba huyo huyo alipe ada, anunue chakula, ajenge nyumba, awekeze kwaajili ya watoto, akupe mama hela ya mahitaji ya kike, bado hamjatoka out wazazi na muda mwingine kama familia.... bado majukumu ya kijamii ya hapa na pale.
Muda huo mama upo tu MY MONEY IS MY MONEY huyo baba si atatembea anaongea njiani?
Na atajikuta anaishia kubangaiza, ila penye ushirikiano na mgawanyo wa majukumu hata kufikia uhuru wa kifedha ni rahisi, watoto wenu hawatokua na haja ya kusaidiana majukumu na wake zao maana familia imeshatoka huko.
3. Mtoto ni zao la starehe siku hizi vijana hawaoi kwa sababu mbalimbali lakini sababu moja wapo ni ndoa kuwa kama mzigo majukumu ni mengi so bora mtu apige mechi za hapa na pale mimba ikitokea anakula kona au anatoa tu matunzo
Nawahurumia vijana wanaojitafuta na wanatoka familia za kawaida, kuoa itawachukua muda sana maana nayo imekua ni uwanja wa vita na kujiongezea majukumu