Nina milioni 25, naweza kuwekeza kwenye nini ili nipate pesa nzuri kwa muda mfupi?

Nina milioni 25, naweza wekeza kwenye nini ili nipate pesa nzuri kwa muda mfupi?

Wadau mawazo yenu Tafadhali.

Mchango wa mdau


Pia soma: Biashara gani zinazoingiza mamilioni kwa muda mfupi?
Weka bank. Fahamu kuwa wazo la biashara linaanza na wewe na kuboreshwa na wengine. Kama huna idea weka hela yako bank usijewalaumu wanadamu. Bank ndio sehemu salama ya kuhifadhi hela kwa watu wasiojua nini cha kufanya nayo kazi.
 
yaani hapa ni unanunua na kuuza.
Ndio. mtu anaweza kununua gari la 2.5m na kuliboresha kidogo (ila sio lazima kama lipo salama) na kuirudisha mtaani na kuulizia 3.5m hadi 6m saa zingine. ni swala la kujua tu wapi kuangalia na kuwa makini kwani kuna walengaji na wanunuzi.

Bei nzuri ni mnunuzi na bei ya chini ni mlengaji. la wewe ndio wakuangalia profit yako. sio biashara ya kuparamia ila mtu ukiwa mtulivu na ikawa na adabu ya pesa, ni kitu kizuri sana. ingawa siku hizi hii shughuli imevamiwa sana. so mzunguko unachukua muda kidogo ila inalipa.
 
Kwenye magari kuna ma oligach wengii angeanza na za pikipiki meaning kufanya services za pikipiki na bajaj zitamtoa taratibu 2M kwa kuanzia, kisha kaingizaa pesa tena katika magahawa wa kisasa 2M kwa kuanzia sio mbaya, tena akaingiza pesa katika usafiri meaning bajaji zake kadhaa labda 2 tu hapa sijajua sinacost bei gani, lastly akimaliza katika hayo anakuja kumwaga hela katika bar na nyama choma.

Hapo jamaa ametawanya pesa katika kila kitu muhimuu yani kiufupi hakwepeki ,yan usipo mpa hela kwenye bajaj utampa kwenye,pkpk ,usipompa hela kwenye pikipiki utampa kwenye chakula au pombe na nyamachomaaaa easy tuuuuuu.....

Sio mbaya akitumbukiza hela chache zitakuwa easy kumanage na easy kufollw up so kile kinachobakia kinaweza kuwa kinaboost biashara na kutatua changamoto mbalimbali.................
 
Sawa sawa maana kuna jamaa mwaka huu huu huku chuga aliitupa crown yake kwa 6mil na alinunua 12mil ndani ya mwezi sababu alitaka pesa ya haraka akauza 6mil dah ila r.i.p kwake jamaa aliyeuza maana alifariki kwa mawazo.
 
Twin hujapata heart attack??...mi nashinda polisi daily[emoji848]

Mimi mpaka sasa kubet ndo kunanipa faida, nadhani upepo umenielekeza huko
Hapana Mungu ni mwema ipo poa sana, hapa naafuta hela niongeze mtaji
 
Location ndo kisanga
 
Muda mfupi ni upi?......wekeza kwa ajili ya vizazi vyako mkuu.
 
Fanya biashara bubu ya kukopesha ila wateja wawe waaminifu .
 
Hela nzuri alafu muda mfupi!? Ila wabongo ndivyo tulivyo.. [emoji3][emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…