Nina milioni 25, naweza kuwekeza kwenye nini ili nipate pesa nzuri kwa muda mfupi?

Nina milioni 25, naweza kuwekeza kwenye nini ili nipate pesa nzuri kwa muda mfupi?

Tatizo humu watu wa nadharia wengi..nenda mgodi wa dhahabu kafanye VAT leanching (kuozesha masalio)mwaka tu una nyumba na Range rover Velar...na mtaji unabaki..
Fafanua hii mkuu
 
Nunua Bajaj 2 milioni 6 tafuta nyumba ya kupanga na fenicha na mtoto mzuri wa kimachame au Siha.

Kila siku Bajaj unaletewa 20k
20,000 x 2 x 365=14,600,000.

Mwaka mzima haiharibiki, no service, dereva hajapata breakdown ..? [emoji23][emoji23][emoji23]
Hakuna hesabu kama hizoooo....
 
Nunua Bajaj 2 milioni 6 tafuta nyumba ya kupanga na fenicha na mtoto mzuri wa kimachame au Siha.

Kila siku Bajaj unaletewa 20k
20,000 x 2 x 365=14,600,000.
Hesabu nyepesi sana ikiwa kwenye maandishi 😃😃😃 nunua hizo bajaji sasa uone! Maana unafikiri itatembea barabarani bila TARURA na TRA kuweka baraka zao! Sijazungumzia kumwaga oil, filter,bush na matairi msee!
 
Chukua milioni tano au kumi, kwa milioni kumi unapata eka 50 kwa kila eka laki mbili mbili.

Kila eka utatumia 30 au 50 kulima.
tafuta mbegu nzuri ya mihogo, uzuri wa kilimo cha mihogo mizizi ikishashika tu basi ata Kama kuna uhaba wa mvua itastahimili.

Kuvuna ukiuzia shambani kila eka haukosi milioni moja na laki tatu, apo unakua umemuuzia dalali shambani, ukiwa na soko lako faida kubwa zaidi.

Ukivuna Mara moja tu ela yako itakua imerudi, na faida kubwa umepata, Shamba ni lako kila mwaka utaendelea kulima.utanishukuru badae
n.b ukiitaji Shamba nicheki 0693786080
Mashamba wapi huko?
 
Jaribu kuagiza, nguo au viatu kwa idadi ndogo kutoka AliExpress ambavyo sio yeboyebo kwa sehemu ulipo. Then vikifika jilipue mtaani au vyuoni kuvinadisha, game likikubali unaweza ukawa unaongeza bidhaa taratibu.

Note, usianze na mzigo wa pesa nyingi, 200k inatosha kabisa kuanzia.
 
We acha tu...hii ni biashara kichaa labda kama hela umeiiba au umeiokota[emoji848]
Hapo sawa na kutakatisha hela, lakini hela ya kuenyeka huwezi kufanya huo ufala, unajenga nyumba ya let say 80m, unapangisha 250k itachukuwa miaka 26 kurudisha hiyo hela.
 
We bibie unafanya hio biashara ya kukopesha?
Yes dear...Ila toka Stone kaingia mpaka anasepa returns imekuwa worsening....

Watu wamechacha, seed capital yangu naona inaelekea kaburini.

Jana mpaka mmoja kaniambia huku akibubujikwa machozi " wity eeh we nipeleke polisi wanifunge, kwanza hapa nilipo nataka kujiua" imagine [emoji134]

Na huyu ndo ana pesa angu ndefuu balaa.
 
Jaribu kuagiza, nguo au viatu kwa idadi ndogo kutoka AliExpress ambavyo sio yeboyebo kwa sehemu ulipo. Then vikifika jilipue mtaani au vyuoni kuvinadisha, game likikubali unaweza ukawa unaongeza bidhaa taratibu.

Note, usianze na mzigo wa pesa nyingi, 200k inatosha kabisa kuanzia.
Laki mbili AliExpress?[emoji15][emoji15]

Na Kodi ya TRA?
 
Mimi ningeku shauri ununue coaster iliyo kwenye hali nzuri, ifanye dalala wewe ukiwa dereva au konda, au ata ukiwakabidhi watu.

Nakumbuka mshua wangu alinunua isuzu journey used ya masaki kariakoo iliweza rudisha mkopo na pesa alipata kidogo zaidi sema ilikua imechoka sana ikaanza kusumbua akaiuza.
Hesabu alikua anapewa 90k kila siku ya kazi.
 
Laki mbili AliExpress?[emoji15][emoji15]

Na Kodi ya TRA?
Vitu vichache huwa ni nadra kupigwa kodi. Kwangu laki mbili naona inatosha kuanzia na sio kwamba unatumia yote kwa mpigo. Mfano ni hizi bidhaa, unaweza agiza vipande 5 ambapo naamini ukiongea na seller anaweza kukupa discount, then ukijumlisha na gharama ya usafiri ambayo utaangalia kama utaimudu. Mzigo ukifika una-fix bei ya mtaani.
Pic_1620540444071.jpg
Pic_1620540402336.jpg
 
Yes dear...Ila toka Stone kaingia mpaka anasepa returns imekuwa worsening....

Watu wamechacha, seed capital yangu naona inaelekea kaburini

Jana mpaka mmoja kaniambia huku akibubujikwa machozi " wity eeh we nipeleke polisi wanifunge, kwanza hapa nilipo nataka kujiua" imagine [emoji134]

Na huyu ndo ana pesa angu ndefuu balaa
Yaani watu walivyowasumbufu kwenye kulipa, sijui wakopeshaji wanatumia mbinu gani kupata faida..mikopo ya kukatwa juu kwa juu ndo atleast aisee.
 
Back
Top Bottom