Nina milioni 25, naweza kuwekeza kwenye nini ili nipate pesa nzuri kwa muda mfupi?

Nina milioni 25, naweza kuwekeza kwenye nini ili nipate pesa nzuri kwa muda mfupi?

The best advice

Nimewahi kupoteza 17 Million kwenye kilimo kwa sababu ya kukurupuka - niliambiwa ufuta na mpunga vinalipa sana basi nikasema ngoja nitumie principle of diversification 8.5M niweke kwenye mpunga na 8.5M nyingine niweke kwenye ufuta Kondoa kilichotokea pesa iliyorudi kutoka kwenye mauzo hata milioni tano haikuzidi kwa vyote (mpunga + ufuta) ni mambo ya ajabu sana yanaendelea kama hutafuatilia miradi yako wewe mwenyewe tena kwa ukaribu na unaweza ukawa unafuatilia kwa ukaribu lakini kama huna utaalamu basic wa kitu pia nirahisi sana kupoteza pesa yote - kumbuka ufuta nililima ekari 50 na mpunga ekari 25 na nilienda kukagua mimi mwenyewe lakini matokeo yalikuwa kama hivyo maana najua ntaambiwa kilikuwa ni kilimo cha whatsapp

So kwa mleta mada milioni 25 ni pesa inayoweza kukufanya ukapiga hatua lakini pia kupotea ni dakika mbili tu inabidi uwe makini sana

Ushauri wangu

Katika pita pita zangu nimegundua kama vijana mkiungana especially wenye maono yanayofanana mnaweza kufika mbali kama utakuwa na rafiki mzuri ( wa kibishara maana uwana nao ukizidi hakuna kitakachoendelea) mnaweza kuingia ubia na kufungua microfinance mnaisajili vizuri na kufuata taratibu zote za ki mamlaka mnaweka zenu 10 Milioni na yeye anaweka mnakuwa na 20 Milioni yenu mnaanza kuizungusha kwa riba nafuu bila kuwa na tamaa na kuhujumu au kuonea watu....Milioni 15 nyingine unajiwekea akiba maana hakuna guarantee pia kwamba lazima upate faida kwenye microfinance ila with proper nurturing ni business inayolipa sana ..na wateja mnaweza anza na watu hata watano au kumi mnao waamini (wapo mtaani) japo pia wapigaji ni wengi sana...ila baada ya miaka mitatu kama mnaenda na principle zenu nzuri za kibiashara na kibenki ...utarudi hapa kunipa mrejesho

Ukiweza pia kufanya peke ako Microfinance ni wewe tu ila fuata taratibu na ukubali kukua kidogo kidogo

Uwe na siku njema
Kwa biashara za kibongo ni bora kuwa mchuuzi wa mazao! Hela itakuwa safe sana kama una hustle mwenyewe thru the process usimuachie mtu hela akufanyie kazi maana uaminifu wabongo ni sifuri! Kuna jamaa ni mfanyabiashara mkongwe ila alikusanya 12M kwa vijana 10 kwa kila kijana total of 120M kisha akawapiga kumbe alikopea hela nyumba yake aka default ili wasiuze akapeleka hela za machalii akatokomea kusikojulikana
 
Naona watu wengi mnamshauri hivi..yan ukitaka kufanya biashara ya kukopesha unatakiwa uwe Mchawi au Mcha Mungu sana la sivyo wakopeshaji watakusahaulisha madeni yao.
Hahahah uwe na roho ngumu sana hii biashara au uweke mtu mwenye roho ya kikatili kama mtu wa kudai chako on behalf kwa mtu mwenye roho nyepesi kama mimi ntapigwa ntachakaa mapema tu!
 
Hahahah uwe na roho ngumu sana hii biashara au uweke mtu mwenye roho ya kikatili kama mtu wa kudai chako on behalf kwa mtu mwenye roho nyepesi kama mimi ntapigwa ntachakaa mapema tu!
Shida ni Ulozi,mtu anadiriki akuroge upagawe ili asalimike kuwa Mdeni wako
 
Shida ni Ulozi,mtu anadiriki akuroge upagawe ili asalimike kuwa Mdeni wako
Usimkumbuke kabisa ila shida ni kuiendesha ofisi kijamaa! Ukiiendesha kama taasisi hamna mtu atakuroga! Weka watu wafanye kazi on behalf of you kisha wakupe reports
 
Hahahah uwe na roho ngumu sana hii biashara au uweke mtu mwenye roho ya kikatili kama mtu wa kudai chako on behalf kwa mtu mwenye roho nyepesi kama mimi ntapigwa ntachakaa mapema tu!

na ukiipatia ni kabiashara katamu sana.
 
Tamu kama watu hawakurushi hela zako wanarudisha kwa wakati kama mlivyokubaliana! Hii naona nzuri kufanya na wafanyakazi wenzio maofisini ila sio na watu wa mitaani

basi mimi kwangu tofauti sithubutu kumkopesha wa ofisini kwangu maana ni wasumbufuuuuu so sijawahi thubutu maana waliotangulia wanalalamika.

Wengi ninaowakopesha wanaletwa na watu wangu ndugu, friends nk.

wa mtaani hapana, muda wa kwenda kuchukua masufuria ya mtu kisa hela hapana!!

kwa mtu alie na watu waaminifu afanye hii ni biashara nzuri sana
 
Ooh kwa wanaoletwa na watu wako wa karibu hio inapendeza sana! You can make a good business hata sie tunaowakopaga ni marafiki ambao tuna mahusiano nao mazuri!

Basi mi nikajua wafanyakazi ndio safe kuwakopesha kumbe dah ndio hawafai 😅😅😅
 
Back
Top Bottom