Nina Milioni 3 ni bora ninunue hisa za CRDB au niende Chalinze nikanunue kiwanja?

Njoo nazo huku tunduru tutafuta jiwe moja tu unauga umaskini
 
Shida ya Kiwanja hakina gawio mkuu. Yaani ukiweka umeweka

Ila nimeambiwa kule kwenye hisa kila mwaka kuna magawio
Fanya calculation ya Gawilo lako kwa miaka jumla itakuwa kiasi gani miaka 5-10 ijayo. Then fikiria juu ya appreciation ya ardhi baada ya miaka hiyohiyo. Utagundua ardhi itakupa gawio hata mara 10 au 100 ya gawio la CRDB. Jambo la msingi hakikisha unanua ardhi salama.
 
Kwa shilingi milioni tatu ikiamua kununua hisa ina maana utapata hisa 1093 kwa bei ya leo 2680 kwa hisa moja.

CRDB mwaka huu wametoa gawio la shilingi 90 kwa hisa moja na makadirio ya gawio la 110 kwa mwakani....

Kupata faida kwenye hisa kuna mambo mawili.
1. Kupata gawio
2. Kukua kwa thamani ya hisa/capital gain...

Kwa kwa hisa 1100 ina maana utapata gawio la 121,000/= ukisubiri mwaka mzima.

Na kama hisa itajikongoja ikapanda thamani tuseme kwa kiasi cha 3500 mpaka mwakani ina maana faida yako itakua ni 900 kwa kila hisa ukiamua kuja kuziuza zikipanda thamani hvyo utapata 900,000/= kama faida

Ishu je hisa ni uhakika kupanda. Jibu ni HAPANA. So ni kama betting kutegemea kupanda.

Pia milioni 3 ni ndogo sana kwa biashara ya hisa...

Kwa ushauri wangu nunua SHAMBA utulie usubiri hiyo miaka 5 uje uuze viwanja.

Ardhi haiozi.
 
Inategemea kiwanja Kipo sehemu gani, malengo ni nini kwenye hicho kiwanja kama ni kujenga au kuuza au shamba...Vyote ni muhimu kulingana na malengo yako ya muda mrefu...
Mkuu haijalishi kiwanja kipo wapi ili mradi hakina mgogoro. Kila miji hadi vijiji vinaendelea. Ndani ya mwaka tu kiwanja kinakuwa na thamani mara 2 ya bei aliyonunulia.
 
Kata nusu nunua mashamba nusu nyingine nunua kiwanja hutajuta 5yeras to come. Chalinze ya moto sana.
 
niliwahi kuwa na same amount, nikasema niifanyaje nikaamua kuanza kibiashara cha wakala wa mitandao ya fedha, kuacha gharama za kutengeneza kibanda na kupata leseni za niashara nilianza na mtaji wa 2.5m hivyo hivyo kwa kubangaiza ndani ya mwaka kamtaji kakawa 5m na hapo ilikuwa ni mitandao ya simu tu. currently nimepata nmb na nbc nasongesha mdogo mdogo. Mwisho wa yote nunua ardhi au anzisha biashara achana na hayo magawio hayo yanawafaa wazee au mtu mwenye ela ambayo anadunduliza ili afikie kiwango flani.
 
Mkuu haijalishi kiwanja kipo wapi ili mradi hakina mgogoro. Kila miji hadi vijiji vinaendelea. Ndani ya mwaka tu kiwanja kinakuwa na thamani mara 2 ya bei aliyonunulia.
Uwezo wa kunusa Potential ya eneo ni muhimu Sana, lazima ujue unanunua kwaajili gani...Yapo maeneo licha ya Kutokuwa na migogoro bado pako vile vile, appreciation mwendo wa Kobe, limenitokea Hilo....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…