Nina Milioni 3 ni bora ninunue hisa za CRDB au niende Chalinze nikanunue kiwanja?

Njoo Kibaha nikupe ardhi
 
Nunua sasa cryptocurrencies zinaitwa XRP (moja ni TZS 2,900,) na nyingine inaitwa XLM (moja ni TZS 497.47)then mwezi wa 10/11 mwaka huu uza. Ni uhakika utakuwa umepata hela nyingi kuliko ungenunua hisa za CRDB/ardhi. Na usisahau kumshukuru sana Mungu pindi utakapokuwa umefanikiwa. Kila la kheri.
 
Ukipata kiwanja sehemu sahihi ndani ya miaka 3 unaweza 2× ya pesa uliyonunulia hicho kiwanja + connection ya madeal mengine yanayohusiana na viwanja n.k
Ni kama hisa tu, baada ya miaka mitatu inaweza kuwa ime-double. Shida ya vijana wa leo tunataka faida ya chap na mafanikio ya haraka haraka. Uwekezaji wowote ukiupa muda unazaa matunda.
 
Nunua kiwanja nayo ni zaidi ya Hisa,ukinunua Leo Kwa Hela hiyo muda SI mrefu,unaweza kuuza mara2 ya hiyo uliyonunulia!
 
Upo sahihi mkuu. Na mimi hii ndio namna naifikiria hisa, kwanza inatakiwa uifikirie kwa long term, miaka mitatu, mitano au kumi na kuendelea. Pia, inatakiwa liwe zoezi endelevu. Yaani unanunua hisa kila wiki au kila mwezi. Pia uendelee kukimbizana na vyanzo vingine vya mapato kama biashara, kilimo, uchimbaji madini na ufugaji.
 
Ni kama hisa tu, baada ya miaka mitatu inaweza kuwa ime-double. Shida ya vijana wa leo tunataka faida ya chap na mafanikio ya haraka haraka. Uwekezaji wowote ukiupa muda unazaa matunda.
Hisa niaka mitatu inadouble vip mkuu hebu kokotoa hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…