Kwa milioni tano ni ngumu kupata IST ya maana ili ufanye uber, pia biashara ya uber ni ngumu kwa sasa.
Ushauri wangu tu, chukua nusu ya hiyo pesa (2.5m) nunua pikipiki (boxer?) halafu fanyia biashara wewe wenyewe, hiyo hela nyingine weka akiba tu, wakati unapiga miche miche za bodaboda kuna deal za biashara zingine unaweza ukazijua then ukaitumia hiyo pesa iliyobakia kama mtaji. Kwa boda upo uhakika wa kulaza sio chini ya elfu 10 kwa siku.
Ushauri mwingine unaweza ukanunua bajaj used kwa hiyo milioni tano halafu ukapiga mwenyewe hiyo biashara, na kuwa na uhakika wa kulaza sio chini ya elfu 25 kila siku.