KingPower
JF-Expert Member
- Jun 8, 2015
- 1,115
- 1,807
Naona huu ni ushauri murua kbsa
Tafuta wataalam wa green house wakufundishe kulima nyanya kwenye huo mjengo, Kwanza kabisa uwaeleze una huo mtaji hivyo wakupe mchanganuo wote wa gharama ya huo mjengo na gharama zingine za kama mbegu, drip pipes, water tanks, na vinginevyo, kwa sababu hela inaweza isitoshe Kuna wataalamu huwa wanauza green house na pia kukufundisha hadi zao likomae ibakie kwako tu kuamua unataka kuuza lini zao lako maana likiwa hata limeiva na lipo kwenye huo mjengo lina uwezo wa kukaa hadi miezi kadhaa bila kuharibika huku ukisubiria bei ya nyanya sokoni ipande madalali waanze kukumezea mate huku udende ukiwatoka
Hiyo biashara itakufanya utulie nyumbani ukiwa bizy na kilimo chako ambacho ni kidogo na cha kisasa na chenye faida kubwa huku ukiwa umekwepa msala wa kukimbizana na Uba ambayo itakufanya urudi na hela ya kula tu ya maendeleo haipo.
Cha msingi poteza mwezi mzima, ukitembelea wenye green house ulizia changamoto za hiyo biashara na faida ukiona inakufaa chukua hatua.