Nina millioni 80 nataka ushauri wa biashara

Nina millioni 80 nataka ushauri wa biashara

Hizi pesa kweli haziji kwenye vichwa vyenye mawazo kibao ya biashara!
Ningekuwa mimi nisingejenga hiyo Guest House, kwa sababu hesabu ya harakaharaka hiyo guest ya 80M ni vyumba kama kumi tu (Guest ya Kawaida sana Mkoani), hapo bado utakuwa unadaiwa pesa ya furniture na mambo mengine! Ukiwa unapangisha 20K kila chumba, say una bahati ya location kila siku vikajaa vyumba saba utakuwa na 140K kwa siku, ondoa 50K ya gharama unabakiza faida ya 90K, mwisho wa mwezi una faida ya 2.7M pekeyake! Itakuchukua miaka kama mitatu kurejesha gharama za ujenzi ndiyo uanze kula faida..hapo nadhani utakuwa unajiandalia mazingira ya kustaafu, obviously baada ya miaka hiyo mitatu guest itakuwa imechoka na kuchuja, Guest nzuri zaidi zitakuwa zimejengwa maeneo hayo na soko lako litashuka!! Sisi wakomaaji wa mjini tukizikamata 50tu basi ntolee, lazima ilale 20M kila mwezi FAIDA! Nina project zangu mbili ziko kwenye vitabu zinahitaji kama 300M na 700M respectively hizo hazina ushindani wowote bongo, ni suala la muda tu, dadeki!

Lakini kwa wewe mkuu ambaye nadhani haujawahi kufanya biashara ya namna yoyote ile ujue unaweza kupoteza kiasi kikubwa cha fedha katika kujifunza biashara, ukija kukomaa mtaji umepungua sana, na kama kazi ndiyo ulishaacha ni lazima ufulie vibaya. NAUNGA MKONO HOJA YAKO YA KUJENGA NYUMBA NA KUREJEA KUAJIRIWA!

Mkuu naitamani kuijua hiyo project yako ya 300
 
Mkuu naitamani kuijua hiyo project yako ya 300

Hahahaa, nisamehe mkuu, hiyo ni siri ya kibiashara mkuu, na hapa ni mjini! Ngoja nikupe mfano mmoja hai kabisa, kuna jamaa yangu alikuja mkoani nikawa napiga naye stori, ni jamaa yangu wa karibu sana, nikaongea naye wazo langu kuhusu kuwasilisha proporsal inayohusu kazi flani ofisini kwao, akalipenda wazo na akasema yeye binafsi atawasilina na Mkurugenzi wao Mkuu na ana uhakika kazi tutaipata. Aliporejea ofisini kwao katika hali ya kuwa over excited akamdokeza ishu IT wao, yule jamaa akaona ile ni pesa iliyo njenje kabisaa akaamua kuzunguka na kuwatafuta jamaa flani wenye kampuni hapo mjini wakaipeleka faster ile proposal kwa mkurugenzi mkuu, ile ishu ikakubalika immediately, Jamaa yangu amekuja kupata muda wa kuongea na Mkurugenzi akashangaa anaambiwa tayari kuna watu wanafanyia kazi kitu kama hicho!!! Hakujua kama amezungukwa, yeye akajua watu wenye wazo kama letu wametuwahi tu, tukapotezea. Miezi kadhaa baadaye yule IT wao akaconfess kwa jamaa kuwa lile wazo aliliiba na kwa bahati mbaya kabisa wale jamaa aliokubaliana nao kutumia kampuni yao walimliza, kazi yenye faida ya 70M wakampa millioni moja na kumwambia kazi ilikuwa ya hasara!!!!!!:doh:
 
Nenda mkuranga, nunua shamba, eka moja 350,000 tshs. Usinunue chini ya 30, kukata na kusafisha visiki lako ishirini kwa eka, chumba kisima kirefu km 13m kila kitu(excl irrigation syst) tupia hapo mihogo au nanasi au pesheni au mahindi, isipokulipa tuamini imani za kiswahili kuwa umerogwa, mihogo unweza kukausha ukasaga unga kingine ukauza mibichi

bonge la wazo hata isipomlipa ardhi ni bonge la asset na inapanda thaman kila siku hivyo miaka kadhaa anaweza kuuza kwa bei kubwa zaid ya aliyonunulia
 
Wakuu hebu nipeni ushauri wa biashara nimepata hizo pesa hapo juu millioni 80 lakini kila nikichekecha biashara ya kufanya ilipe nakua sioni sasa nimeiona niweke hapa ili nipate mawazo nijue pa kuanzia.Mimi naishi mkoa wa Dar-es-salaam

kwa hela hiyo kafungue microfinance yako ya kukopesha mikopo midogo midogo
 
mkuu ningekuwa mimi ndio wewe nisingetafuta kaz nyingine bali ningejiajiri mwenyewe. na biashara nzuri ni ya vijijini haswa za shamba. mfano huku kwetu moro hasa wilaya ya kilombero na ulanga, ardhi yake ina rutuba na pia matrekta ya kulimia yapo machache sana na bei ya kulima kwa heka ni elf 45 had 50 kwa heka na trekta moja ni milioni 25 had 30. so ningekuwa wewe ningeenda tu kijijini kisha nanunua trekta zangu mbili na shamba la eka 5 had 10 kisha nalimisha watu mashamba yao huku na mimi nalima yangu. kwa hii biashara ya trekta kila siku utakuwa unalaza si chini ya laki 5 kwa trekta moja au milion kwa matrekta mawili. ila tu uwe mwenyewe na usimuweke mtu atakuibia. Niishie hapo
 
Anataka kumuibia huyo!!!!

Sijui kama wazo langu limechelewa au lah...lakini kama nimewahi kabla hujaingia katika mpango wowote basi si haba, kwa kusema ukweli mie kwangu nakiona kama hicho ni kiasi kikubwa sana cha pesa na naona kama siku mwenyezi mungu akinijaalia nakunipatia kiasi kama hicho, dua zangu zitakuwa zimejibiwa kwa asilimia 100. hii ni kutoka na mipango na utafiti wangu nilioufanya ktk miaka 3 nilio ktk ujasiriamali.

kwa wewe nakushauri kitu rahisi na kisichokuumiza kichwa kama. ingi katika real estate kama mtu unaeanza na hakika utafika mbali,

Nenda nunua kiwanja kizuri mahali pa zuri (Prime area) kwa bajeti ya 20million, tengeneza nyumba 45 million unabakiwa na chenge 15 million.

jifanye umesahau hiyo 15million ktk bank, na ujitahidi nyumba usimamie mwenyewe kisha itakapokwisha iweke sokoni kwa 80 million, unaweza kukaa nayo bila kuuza kwa masaa 24 mpaka miezi sita, siku ukiuza unaweza kupata faida ya 10million hii ni faida kubwa sana, kwani hakuna operation charges wala running cost yoyote kubwa utalipa baada ya mauzo.


yapo mawazo mengi ila pima na uchague lipi ni zuri. ila kuwa makini sana na biashara inayohitaji rasilimali watu si biashara poa kwa mtu anaeanza, na pia usiingie ktk biashara iliyo rasmi kwani utapaswa kulipa gharama nyingi na licence ni nyingi na malipo yake ni kero sana.

asante
 
Real estate inalipa sana haswa kama inapenda kutengeneza faida na kujiajiri MWENYEWE kwani wachache wanaweza VI7 .JIFUNZE MBINU ZA KUPAMBANA NA WAJASIRIAMALI WENZAKO /VILEILE UNAWEZA KUJIINGIZA KATIKA KILIMO NA UKATOKA NDANI YA MIAKA 2/3 ...KARIBU MAISHA REAL ESTATE ....
 
Wakuu hebu nipeni ushauri wa biashara nimepata hizo pesa hapo juu millioni 80 lakini kila nikichekecha biashara ya kufanya ilipe nakua sioni sasa nimeiona niweke hapa ili nipate mawazo nijue pa kuanzia.Mimi naishi mkoa wa Dar-es-salaam


Chukua mil 30 kawekeze kwa kununua viwanja dsm pembezoni mwa mji,baada ya miaka ukiviuza utapata faida kubwa sana.
 
This year no more drama mainly because my saving accounts show more commas coz I need comma after my comma!!
 
Mkuu huo mtaji ni mkubwa sana,tengeneza rebo yako kisha anza kupaki sembe.Funga 5kgs,10kgs,20kgs,25kgs na 50kgs!

Tafuta site nzuri fungua duka kubwa kwa ajiri ya kusupply.pack na unga wa muhogo na dona,uza jumla na rejareja.

Nimecheka sana hiyo Avatar yako.
 
Back
Top Bottom