Nina millioni 80 nataka ushauri wa biashara

Nina millioni 80 nataka ushauri wa biashara

Umetoa wapi hela yote?

Ok,naona watu wengi humu wanataka kujua hizo hela nimetoa wapi,hizi hela sijaiba ni zangu mwenyewe na nimezipata kihalali.Nilikua nafanya kazi katika kampuni moja ya madini na nimefanya kwa mda wa miaka 6 contract basis imeisha nimelipwa mafao plus nssf nikapata jumla ya shillingi za kitanzania 110 millions nikaamua nitoe 80m kwa ajili ya kuangalia biashara ya kufanya ndio maana umeona hata zile ideal nimechagua biashara ambayo haina mizunguko sana manake nimeshaajiriwa na kampuni ingine na biashara ambayo nimeona itakua ideal in ya kujenga guest house na ninaexpect kuingia contract na mtu kwa ajili ya kuioperate.
 
Nenda mkuranga, nunua shamba, eka moja 350,000 tshs. Usinunue chini ya 30, kukata na kusafisha visiki lako ishirini kwa eka, chumba kisima kirefu km 13m kila kitu(excl irrigation syst) tupia hapo mihogo au nanasi au pesheni au mahindi, isipokulipa tuamini imani za kiswahili kuwa umerogwa, mihogo unweza kukausha ukasaga unga kingine ukauza mibichi
 
Wakuu hebu nipeni ushauri wa biashara nimepata hizo pesa hapo juu millioni 80 lakini kila nikichekecha biashara ya kufanya ilipe nakua sioni sasa nimeiona niweke hapa ili nipate mawazo nijue pa kuanzia.Mimi naishi mkoa wa Dar-es-salaam

Kanunue hisa DSE za CRDB au TBL au TTC. Au nenda S'wanga kanunue ulezi.
 
Nunua zile screen kubwa za matangazo kama zile za palm beach moja unaweza pata kwa usd 14000 ukiwa nazo tatu moja town nyingine mlimani city nyingine stand au airport

Makampuni yote ya simu unakula vichwa
Benki zote wala vichwa
Makampuni ya bia n.k
 
Kanunue hisa DSE za CRDB au TBL au TTC. Au nenda S'wanga kanunue ulezi.

Mkuu kuhusu hisa nasikia faida yake ni ndogo sana sijui kuna ukweli wowote?Nikinunua ulezi S'wanga soko lake liko wapi na nitanunua kwa bei gani na kuuza bei gani?
 
Nunua zile screen kubwa za matangazo kama zile za palm beach moja unaweza pata kwa usd 14000 ukiwa nazo tatu moja town nyingine mlimani city nyingine stand au airport

Makampuni yote ya simu unakula vichwa
Benki zote wala vichwa
Makampuni ya bia n.k

Kuweka matangazo hizo kampuni zitanilipa kiasi gani kwa kila tangazo na nafikiri kuna gharama ambayo inabidi kuilipa manispa ni kiasi gani?
 
kunA tanker linauzwa 70 mil. njoo tufanye biashara.
 
Hizi pesa kweli haziji kwenye vichwa vyenye mawazo kibao ya biashara!
Ningekuwa mimi nisingejenga hiyo Guest House, kwa sababu hesabu ya harakaharaka hiyo guest ya 80M ni vyumba kama kumi tu (Guest ya Kawaida sana Mkoani), hapo bado utakuwa unadaiwa pesa ya furniture na mambo mengine! Ukiwa unapangisha 20K kila chumba, say una bahati ya location kila siku vikajaa vyumba saba utakuwa na 140K kwa siku, ondoa 50K ya gharama unabakiza faida ya 90K, mwisho wa mwezi una faida ya 2.7M pekeyake! Itakuchukua miaka kama mitatu kurejesha gharama za ujenzi ndiyo uanze kula faida..hapo nadhani utakuwa unajiandalia mazingira ya kustaafu, obviously baada ya miaka hiyo mitatu guest itakuwa imechoka na kuchuja, Guest nzuri zaidi zitakuwa zimejengwa maeneo hayo na soko lako litashuka!! Sisi wakomaaji wa mjini tukizikamata 50tu basi ntolee, lazima ilale 20M kila mwezi FAIDA! Nina project zangu mbili ziko kwenye vitabu zinahitaji kama 300M na 700M respectively hizo hazina ushindani wowote bongo, ni suala la muda tu, dadeki!

Lakini kwa wewe mkuu ambaye nadhani haujawahi kufanya biashara ya namna yoyote ile ujue unaweza kupoteza kiasi kikubwa cha fedha katika kujifunza biashara, ukija kukomaa mtaji umepungua sana, na kama kazi ndiyo ulishaacha ni lazima ufulie vibaya. NAUNGA MKONO HOJA YAKO YA KUJENGA NYUMBA NA KUREJEA KUAJIRIWA!
 
Back
Top Bottom