Nina mimba na mtoto ana miezi minne, naomba ushauri wenu nifanyeje?

Nina mimba na mtoto ana miezi minne, naomba ushauri wenu nifanyeje?

If thats the case endelea kumnyinyesha mwanao huku unalea mimba, its a bit tricky but mungu atakusaidia!

Financially mumeo inabidi achakarike vbaya mno, manake after 2.5yrs mtaanza somesha, kama hamkujipanga mpaka hapo itakuwa taabu sana huko mbelen
hata angekuwa baba tofauti hakuna mahusiano na afya ya motto na mahusiano current ya mama!
 
Sijawahi kutoka nje ya ndoa, na wala sitarajii kutoka
weeee wasikupe kichwa kuuma hawa!
I AM A MOTHER OF THREE!
najua ninachokwambia!
ENDELEA KUNYONYESHA MWANAO!
 
Mtu akiwa na mimba ninavyojua hormones zinajitengeneza kwenye maziwa. Sasa huoni akiendelea kunyonyesha itakuwa ni problem
 
Ninachohitaji ni nifanyeje ili mtoto asidhulike kipindi hiki cha ujauzito? Maana hofu yangu ni juu ya huyu mtoto niliyenaye
Kupenda sana nanilii...! Ona sasa imedumbikia kitu nyingine.
 
Uache kumnyonyesha huyo mtoto mdogo umuanzishie chakula mbadala kama maziwa ya ng'ombe, maana kudhoofika kwake kunatokana na kunyonya maziwa yako ambayo tayari yamechanganyika na hormones za ujauzito.

Otherwise waone wataalamu wa uzazi wakupe njia nzuri ya kumlea huyo mtoto bila kumnyonyesha
 
pole!
zingatia diet utilie na uzae, then uanze kutumia njia za uzazi wa mpango ili yasikukute tena kama haya
 
Kubaliana na hiyo hali kwanza.
Tengeneza virutubisho vitakavyokuwa mbadala nyonyo kwa mtoto.
Msilale naye kitanda kimoja
Maisha yaendelee. Jihadhari usisononeke kwa kuwa itamwafect mtoto.
 
hata angekuwa baba tofauti hakuna mahusiano na afya ya motto na mahusiano current ya mama!
hapo ilitumika tafsida, ikimaanisha asiwe anabadilisha wanaume wataathiri afya ya mtoto
 
Habar zenu wana jf!! Samahani sana kwa usumbufu, naombeni msaada wenu nifanyeje mwenzenu yamenikuta nipo njia panda sina cha kufanya.

Mwanangu bado mdogo miezi minne tu sasa na tayari nina ujauzito. Mtoto kashaanza kuhara kila siku na anazidi kunyong'onyea tuu. Hospitali walimpima hana tatizo, je nifanyeje? Nawaombeni sana mnisaidie ili niokoe afya ya mwanangu.

Najua kuna watu watanitukana ila yote sawa nastahili, ushari wako ni muhimu.

Asanteni.
Kuharisha kwa mtoto huyo wa miezi minne ni effect inayotokana na kunyonya maziwa yasiyo bora na nimachafu hayafai kwa mtoto kunyonya, kwasababu ya ujauzito ulionao.

Yote ni dhambi kutompa mtoto maziwa chakula kisicho mfaa na kudhorotesha afya yake na pia kuwaza kutoa mimba nayo ni dhambi, mwanzishie mtoto maziwa ya kopo lactogen ambayo hayajachakachuliwa maana fake zipo nyingi, au SMA usiwaze kutoa mimba...
 
Duh miezi minne toka ujifungue umeanza sex,mbona haraka hivyo!kama hiyo mimba si baba wa huyo unae mnyonyesha hapo lzm aharishe na kwa kifupi umembemenda!
 
kabemenda mtoto tayari hana swali hapo, miezi mi nne sasa, kama uli nani? na mtumwingine tofauti na mzee mwenyewe ndo madhara hayo cha msingi wanasema acha kumnyonyesha mtoto tena mtafutie maziwa ya kopo na matunda uanze kumpa ila kwa ushauri zaidi muone dokta. maana nakubuka tatizo lako ni kama la mama mdogo wangu lilikuwa hivyo hivyo sema mtoto wa kwanza kawa mbilikimo namaana mfupi
 
Hakuna kitu kinachoitwa maziwa machafu, hiyo ni imani ya kimila, mama mjamzito anaweza kumnyonyesha mtoto wake mchanga hadi siku yakujifungua na ikiwezekana na hata baada yakujifungua (kumnyonyesha wote wawili) na yasitokee madhara yoyote na ukioona mtoto akinyonya anaharisha, inawezekana usafi wa matiti ya mama hauja zingwatiwa au tayari mtoto kashapatwa na utapiamlo
Bado nina maziwa ya kutosha sana, hawezi hata kuyamaliza ... Sasa labda cjui huo utapiamlo unatokana na nini?
 
Kulea ni kazi sana, mimi hapa nna mapacha wa nje ila mwenzangu umezidisha miezi mi 4 kha?? Hahahhaa ila usijaliyameshatokea zipo njia za kumlea vyema mwanao atakua vzr tu
 
Kwani bado ananyonya? Kwanza, kitendo cha kupata mimba ndani ya muda mfupi hivyo inamaanisha ulikuwa hunyonyeshi mtoto mara kwa mara maana kunyonyesha ni njia mojawapo ya kuzuia mimba. Na kama hivyo ndivyo huna haja ya kuogopa, shida ni pale mtoto anaponyonya material isiyotakiwa kwenye mwili wake, fyatua tu!
Hiyo sababu ya kutonyonyesha mtoto Mara kwa Mara mi naikataa, wengi tuliaminishwa hivyo hata baada ya kufuata bado tukajikuta tumenasa,
 
Nlisikia mwanamke anaenyonyesha hapati ujauzito kumbe ni porojo tu.

Kupitia wewe nimejifunza kitu.
 
Back
Top Bottom