Nina mimba na mtoto ana miezi minne, naomba ushauri wenu nifanyeje?

Nina mimba na mtoto ana miezi minne, naomba ushauri wenu nifanyeje?

Do ile theory ya kuwa ukiwa unanyonyesha mimba haiwezi kushika si kwa wote, wengine wakijaribu tu ni kitu na box. Kula vizuri na kufanya mazoezi, jitahidi kutembea hata kwa nusu saa kila siku kama utaweza.

Jitahidi kubalance mapenzi kati ya hawa watoto wote, kwasababu wako karibu huyu aliyetangulia pia atahitaji kupendwa kama mwenzake. Wazazi wengi wanajisahau na attention yote inahamia kwa mtoto mchanga.
Ndo maana wazee wa zamani ukizaa unakwenda kwenu kwa muda mrefu
 
Bado nina maziwa ya kutosha sana, hawezi hata kuyamaliza ... Sasa labda cjui huo utapiamlo unatokana na nini?
Mpe vyakula vya lishe kwa wingi ila uwe makin maana iyo miezi mi nne aliyonayo mfumo wake wa chakula bado mlaini sana hivyo unatakiwa kuhakikisha kama ni chakula au juice juice inakua blended well ili kusiwe na vijinyuzi nyuzi, ondoa hofu atakua tu vyema
 
Kuharisha kwa mtoto huyo wa miezi minne ni effect inayotokana na kunyonya maziwa yasiyo bora na nimachafu hayafai kwa mtoto kunyonya, kwasababu ya ujauzito ulionao.... Yote ni dhambi kutompa mtoto maziwa chakula kisicho mfaa na kudhorotesha afya yake na pia kuwaza kutoa mimba nayo ni dhambi.....mwanzishie mtoto maziwa ya kopo lactogen ambayo hayajachakachuliwa maana fake zipo nyingi, au SMA usiwaze kutoa mimba...
Ampe tu maziwa ya ng'ombe ambayo hayajachanganywa na Maji kuepuka ayo maziwa Fake ya kopo
 
MAZIWA YANAHARIBIKAJE JAMANI!?
hakuna hicho kitu!
AENDELEE KUNYONYESHA MWANAE!
Wataalamu hutuambia hivyo, ila kuepuka hofu ya kuhusisha maziwa anayonyonya mtoto na hali yake ya kiafya namshauri aache tu kumnyonyesha!

Itampa amani na itamjenga zaidi kisaikolojia kumuhudumia mwanae bila kumnyonyesha, mimi pia wanangu wamefungama hivyo hivyo ila niliambiwa niendelee kumnyonyesha mtoto vi homa homa havikwisha kuharisha n.k sasa nilikua namnyonyesha mwanangu saikolojia yangu ikawa inaniambia kama namsababishia mwanangu matatizo, au nampa sumu mwanangu, nikawa najilaumu sana mtoto akimaliza kunyonya na baadae akaharisha mavi yenye mtelezoo yaani ilikua inaniuma sana mama yangu alipokuja aliniambia niache kumnyonyesha akaanza kunipangia na kunielekeza diet ya mtoto na tukaanza kumpa maziwa ya ng'ombe taratiibu mambo yakaanza kubadirika na mpaka sasa yuko vzr kabisa
 
Nenda Hospitali tafuta daktari mwaminifu na mcha Mungu muombe ushauri...atakachokushauri kitekeleze....usiombe ushaur JF kwa watu ambao wengi hatuna utaalam huo.
Usidharau watu Mkuu! Hao ma Daktari unaowaamini wanatumia uzoefu wa vitabu tu, ndo Yale yale unaambiwa usimpe mtoto chochote ndani ya miezi 6 wakati unaishi Dar joto kalii mtu mzima tu huwez kuvumilia kuto kunywa Maji lakini mtoto unaambiwa usimpe hata robo kijiko, ila cha ajabu sasa watoto wao majumban wanawalea nje ya wanavyokushauri
 
Wee unamshaurije MTU aache kunyonyesha? Nani kakwambia MTU akiwa mjamzito kunyonyesha ndo basi? Mafunzo ya wapi hayo? Acha kukurupuka na kutoa mafundisho dhoofu na potofu. Mjamzito anaruhusiwa kunyonyesha mpaka mtoto mwenyewe akatae. Virutubisho vya maziwa viko pale pale na havina madhara yoyote .

Ww ndo umekurupuku mm nampa ushaur kutokana na niliyoyashahudia akiendelea kumnyonyesha mtt atakua anaharisha mara kwa mara na uwezekano wa kumbemenda mtt ni asilimia kubwa sana anachotakiwa kufanya n kumuanzishia maziwa yale ya kopo na lishe iliyokua imara.

Halaf usipende kujifanya mjuaji sana vingine si lazma usomee au uambiwe na mtu mazingira ninayoishi ni elimu tosha.
 
Nimesema usafi wamatiti, ni kitu cha kuzingatia, usipo zingatia, mtoto anaweza kuunyonya na ndio hapo maziwa yasiwe na lishe ndio hapo utapiamlo unakuja
 
Mtoto hawez haribika mi ilisha nitokea nilibeba ujauzito mtoto akiwa na miez mitano nikashauriwa na daktar kuwa ninyonyeshe hadi mimba ikifika miez saba nimuachishe na wala mtoto hakuharibika nilimnyonyesha mimba ilipofikisha miez saba nikamuachisha

Basi inategemea na ziwa la mtu mm mdogo wangu yalimkuta hayo mambo aliendelea kumnyonyesha mtt na kila cku mtt akawa anaharisha akaambiwa aache kumnyonyesha ikawa n mwendo wa lactogen tu.
 
Ninachohitaji ni nifanyeje ili mtoto asidhulike kipindi hiki cha ujauzito? Maana hofu yangu ni juu ya huyu mtoto niliyenaye
Kuna mila hasa kule Tabora
Mtoto anaogeshwa baadhi ya dawa
Akifikisha miezi 6-7 usi lale nae
Ikibidi unampeleka kwa bibiake au kwa ndugu
 
Ww ndo umekurupuku mm nampa ushaur kutokana na niliyoyashahudia akiendelea kumnyonyesha mtt atakua anaharisha mara kwa mara na uwezekano wa kumbemenda mtt ni asilimia kubwa sana anachotakiwa kufanya n kumuanzishia maziwa yale ya kopo na lishe iliyokua imara. Halaf usipende kujifanya mjuaji sana vingine si lazma usomee au uambiwe na mtu mazingira ninayoishi ni elimu tosha.
Hamna hicho kitu kinachoitwa kubemenda, Anatakiwe aendelee kunyonyesha na azingatie kula lishe kamili na supplement ya vitamin na Zinc,atafute unga wa mbegu za maboga ili kuongeza kiwango cha maziwa ,
 
Aisee maziwa ya ng'ombe yasiyotiwa maji? Content ya maziwa ya ng'ombe aliyoandaliwa ndama ,mtoto ndiyo ayanywe hivyohivyo? Ni bora formula kuliko maziwa ya ng'ombe kwa mtoto mdogo maziwa ya ng'ombe yanasababisha allergy tena ni mtoto mdogo ambaye kinga ya mwili bado ni ndogo.
 
kabemenda mtoto tayari hana swali hapo, miezi mi nne sasa, kama uli nani? na mtumwingine tofauti na mzee mwenyewe ndo madhara hayo cha msingi wanasema acha kumnyonyesha mtoto tena mtafutie maziwa ya kopo na matunda uanze kumpa ila kwa ushauri zaidi muone dokta. maana nakubuka tatizo lako ni kama la mama mdogo wangu lilikuwa hivyo hivyo sema mtoto wa kwanza kawa mbilikimo namaana mfupi
Hakuna kitu kinachoitwa kubemenda elimu ya mtaani inaponza sana.
 
Bado sijaenda hospitali , nimeolewa, nina mtoto mmoja tu, umri wangu ni 29 yr,
Ndgu yangu hiyo ni biingoo....nenda kwa washauri wa afya wakushauri vyema lea mimba hiyo kwa age hiyo fyatua tu ukipumzika umepumzika isitoshe uko kwenye ndoa sio kesi watoto kbao mimba zao zinaongozana...
Be strong eat healthy furahia....
 
Ww ndo umekurupuku mm nampa ushaur kutokana na niliyoyashahudia akiendelea kumnyonyesha mtt atakua anaharisha mara kwa mara na uwezekano wa kumbemenda mtt ni asilimia kubwa sana anachotakiwa kufanya n kumuanzishia maziwa yale ya kopo na lishe iliyokua imara. Halaf usipende kujifanya mjuaji sana vingine si lazma usomee au uambiwe na mtu mazingira ninayoishi ni elimu tosha.
Elimu za mitaani hizo mjomba zisikuchanganye. Idara za afya , ustawi wa jamii/watoto na Ma Dr n.k Hakuna MTU atakushauri kuachisha kunyonyesha mtoto mama akiwa mjamzito.

Ukitaka kumshauri MTU hapa shusha nondo kitaalamu na so habari za umbea umbea za mitani za kuomba chumvi au mafuta ya kupikia. Hapa ni kutoa mchango kwa kusaidia jamii . Ukiona huna jibu jitahidi angalau kumwuliza Mr Google atakuelimisha
 
Aisee maziwa ya ng'ombe yasiyotiwa maji? Content ya maziwa ya ng'ombe aliyoandaliwa ndama ,mtoto ndiyo ayanywe hivyohivyo? Ni bora formula kuliko maziwa ya ng'ombe kwa mtoto mdogo maziwa ya ng'ombe yanasababisha allergy tena ni mtoto mdogo ambaye kinga ya mwili bado ni ndogo.
Usitake kuleta ubishi hapa, soma uelewe !! Sasa bora kipi? Maziwa ya ng'ombe ambayo hayajachanywa yaliyoondolewa utando wa mafuta mafuta au maziwa fake ya formula?

Kwa taarifa yako upatikanaji wa mazowa hayo ya kopo ambayo ni original yanachangamoto zake sana unaweza jikuta unampa mtoto maziwa fake, hata hivyo hebu niambie hayo maziwa ya kopo yanatokana na maziwa ya mama wa South Afrika au ulaya yakagandishwa ???
 
Hakuna kitu kinachoitwa kubemenda elimu ya mtaani inaponza sana.
KUNA WATU HUMU NDANI MNAJIFANYA KAMA KUZAA MMEZAA NYIE TU WENGINE WAMEZAA MATUFE HAYALELEWI, USIDHARAU HATA SIKU MOJA ELIMU YA MTAANI NDIYO IMETUKUZA MIMI NA WENGINE NA KUNA WAKATI TUNA i- Apply kwenye maisha ya watoto wetu! Ni Chaguo la mtoa post kuchukua ushauri unaomfaa kutokana na anayoyapitia mwanae na si vinginevyo!
 
Huyo mtoto mpe maziwa, uji mwepesi na mtori kidogo. Usinyonyeshe ova
 
Habar zenu wana jf!! Samahani sana kwa usumbufu, naombeni msaada wenu nifanyeje mwenzenu yamenikuta nipo njia panda sina cha kufanya.

Mwanangu bado mdogo miezi minne tu sasa na tayari nina ujauzito. Mtoto kashaanza kuhara kila siku na anazidi kunyong'onyea tuu. Hospitali walimpima hana tatizo, je nifanyeje? Nawaombeni sana mnisaidie ili niokoe afya ya mwanangu.

Najua kuna watu watanitukana ila yote sawa nastahili, ushari wako ni muhimu.

Asanteni.
Na wasiwasi ulikuwa humsikilizi muuguzi wakati wa somo clinic huwa wanatuelimisha zikifika siku 40 unapoenda kumfulia mtoto kadi la maendeleo ya ukuwaji pia tujiunge na mzazi wa mpango.

Kwa sababu imeshatokea lea tu mtoto na mimba huna jinsi inawezekana kabisa kama utazingatia lishe bora mtoto aliye duniani apate maziwa ya kutosha kwa kipindi hiki cha miezi 6 na watumboni nae apate virutubisho.
 
Sina operation, Ila. Hofu yangu ni juu afya yangu mimi na mtoto, maana kiukweli kupata ujauzito saivi sikupanga kabisa,
Zingatia lishe dada tena hao watakuwa mapacha wa nje wakikuwa utafurahi sana,mie ilishanitokea lakini hakuwa mapema kiasi hicho ilikuwa miezi tisa nililea mimba na mtoto sasa wamekuwa boyz tena najiona mjanja.ila ujiandae kwa miaka miwili si kazi rahisi sana.
 
Back
Top Bottom