Nina mimba na mtoto ana miezi minne, naomba ushauri wenu nifanyeje?

Nina mimba na mtoto ana miezi minne, naomba ushauri wenu nifanyeje?

Do ile theory ya kuwa ukiwa unanyonyesha mimba haiwezi kushika si kwa wote, wengine wakijaribu tu ni kitu na box. Kula vizuri na kufanya mazoezi, jitahidi kutembea hata kwa nusu saa kila siku kama utaweza.

Jitahidi kubalance mapenzi kati ya hawa watoto wote, kwasababu wako karibu huyu aliyetangulia pia atahitaji kupendwa kama mwenzake. Wazazi wengi wanajisahau na attention yote inahamia kwa mtoto mchanga.
Ni kweli unachosema sky Eclat mimi nimeona kwa watoto wangu nijitahidi ku balance mapenzi lkn kuna wakati unajikuta unakuwa makini sana kwa mtoto mchanga.

Huyu niliembebea ujauzito mlalamishi sana huwa anajiona kama simpendi.
 
Do ile theory ya kuwa ukiwa unanyonyesha mimba haiwezi kushika si kwa wote, wengine wakijaribu tu ni kitu na box. Kula vizuri na kufanya mazoezi, jitahidi kutembea hata kwa nusu saa kila siku kama utaweza.

Jitahidi kubalance mapenzi kati ya hawa watoto wote, kwasababu wako karibu huyu aliyetangulia pia atahitaji kupendwa kama mwenzake. Wazazi wengi wanajisahau na attention yote inahamia kwa mtoto mchanga.
It's not a theory my dear, its physiological, scientifically proven. Inaitwa Lactational Amenorrhoea. Tatizo watu wanakosea katika application yake, inatakiwa mtoto awe ananyonya maziwa ya mama pekee (exclusive breast feeding) na mama awe bado hajapata hedhi yake na pia ni miezi sita tu ya mwanzo. Mama akipata hedhi kabla ya miezi sita hii haifanyi kazi na sababu ya wengi kurudia hedhi mapema ni kutokunyonyesha inavyotakiwa.

Baada ya miezi sita hata kama mama bado hajaona hedhi hii method haina tena guarantee. It is a very effective method if applied appropriately.
 
Jitahidi kumtengenezea balanced diet, protein ni muhimu sana katika umri huo kwani ndio anajenga mwili na kinga ya mwili vyakula vya wanga na mboga mboga na matunda, ikiwezekana blend matunda mpe puree au smooth anywe.
Mama anapaswa kujitahidi kula vizuri, pamoja na kuendelea kumnyonyesha mtoto wake mpaka atakapotimiza miezi sita ndio aanze kumpa vyakula mbadala na kuendelea kumnyonyesha huyo mtoto. Kinga bora ni kutoka kwa maziwa ya mama.
 
Ila afya ya mtoto sasa inadhoofika ,
Si umesema mtoto ana miezi 4 jitahidi wewe kula balance diet,mtoto akifika miezi 6 unaanza kumpa chakula za ziada huku ukiendelea kumnyonyesha mpaka mimba ikifika miezi 7 unamuachisha ingawa utakuwa umemkatisha haki yake ya kunyonya miaka 2.
 
Usitake kuleta ubishi hapa, soma uelewe !! Sasa bora kipi? Maziwa ya ng'ombe ambayo hayajachanywa yaliyoondolewa utando wa mafuta mafuta au maziwa fake ya formula ?? Kwa taarifa yako upatikanaji wa mazowa hayo ya kopo ambayo ni original yanachangamoto zake sana unaweza jikuta unampa mtoto maziwa fake, hata hivyo hebu niambie hayo maziwa ya kopo yanatokana na maziwa ya mama wa South Afrika au ulaya yakagandishwa ???
Penda kujifunza unapokoselewa,Nenda kaulize kama kuna dr atakeyekushauri kutumia maziwa ya ng'ombe kwa mtoto mdogo,na kama hujui maziwa ya formula yanatengenezwaje nenda kajifunze kabla ya kubisha.

Juzi kati hapa Drs wameelezea jinsi maziwa ya ng'ombe yanavyoleta allergy especially kwa watoto wadogo ambao uwezo wa kinga kupambana na magonjwa bado ni mdogo.
 
Usidharau watu Mkuu! Hao ma Daktari unaowaamini wanatumia uzoefu wa vitabu tu, ndo Yale yale unaambiwa usimpe mtoto chochote ndani ya miezi 6 wakati unaishi Dar joto kalii mtu mzima tu huwez kuvumilia kuto kunywa Maji lakini mtoto unaambiwa usimpe hata robo kijiko, ila cha ajabu sasa watoto wao majumban wanawalea nje ya wanavyokushauri
ahaa mtoto wa kiume anazaliwa na kilo tano halafu mama huna mazia ya kutosha unaambiwa miezi sita anyonye tu eti si atalia mpaka akujazie mtaa?
 
Anza kumpa vyakula vingine na mnyonyeshe ila pata ushauri kwa daktari namna ya kufanya hivyo
 
KUNA WATU HUMU NDANI MNAJIFANYA KAMA KUZAA MMEZAA NYIE TU WENGINE WAMEZAA MATUFE HAYALELEWI, USIDHARAU HATA SIKU MOJA ELIMU YA MTAANI NDIP IMETUKUZA MIMI NA WENGINE NA KUNA WAKATI TUNA i- Apply kwenye maisha ya watoto wetu! Ni Chaguo la mtoa post kuchukua ushauri unaomfaa kutokana na anayoyapitia mwanae na si vinginevyo!
Za kuambiwa changanya na zako,Jitahidi kupenda kusoma tafiti za watu ili upate kitu kipya,wewe ukipata information huchuji unabeba kama ilivyo ,
 
Penda kujifunza unapokoselewa,Nenda kaulize kama kuna dr atakeyekushauri kutumia maziwa ya ng'ombe kwa mtoto mdogo,na kama hujui maziwa ya formula yanatengenezwaje nenda kajifunze kabla ya kubisha,Juzi kati hapa Drs wameelezea jinsi maziwa ya ng'ombe yanavyoleta allergy especially kwa watoto wadogo ambao uwezo wa kinga kupambana na magonjwa bado ni mdogo.
jamani msiwe na hasira tujadili mada kwa amani maziwa ya formular nayo yana changamoto zake ukutane na kifu feki si huwa unasikia yameua watoto huko china ?chochote kinafaa yawe ya ngombe au formular
 
Nanyonyesha, na hadi hivi leo sijawahi kumpa mtoto chochote kile tofauti na maziwa yangu mwenyewe, tatizo saivi naona anaharisha
Ondoa hofu kama mtoto ana harisha mpeleke hospital akapate matibabu labla amepata bacteria infection kwa umri watoto huanza kuweka vidole vyao mdomo au toys.
 
Ninachohitaji ni nifanyeje ili mtoto asidhulike kipindi hiki cha ujauzito? Maana hofu yangu ni juu ya huyu mtoto niliyenaye
Fanya taratibu za kumwachisha huyo wa miezi mine na mtenge bajeti yake ya mlo na maziwa. Mimi rafiki yangu yalimtokea na akafanya hivyo na mtoto alikuwa na afya njema sana na hakupata tatizo lolote.
 
Hakuna kitu Kinachoitwa kubemenda scientifically. Hii ni imani potofu na ilitumika zamani ili kuwafanya wazaz watulie kweny suala la kulea waache kurukaruka.
Kwa hyo kula balanced Diet itakayokidhi mahitaji yako, mahitaj ya aliyeko tumboni na anayenyonya yani ule vzuri haswa.
 
Mnyonyeshe akifika miezi sita stop ...anza maziwa yamadukani au ngombe huki ukianza kumzoeza na ujiwarishe .....taratibu mtagika ....ukivika hapo salama weka kitanzi cha miaka 12 kabisa upumzike
 
Pole sana dada yangu. Muachishe mtoto nyonyo na umuanzishie maziwa mbadala na wakati huohuo usilale na huyo mtoto kitanda kimoja ili kumuepusha na hilo joto lako.
Haya yapo na hutokea. Kuwa mwenye Nguvu katika hili.

Uzazi mwema na Mungu akulindie wanao na awape afya njema.
 
Ivi mbona wanasemaja ukiwa wanyonyesha haitungi hovyo hovyo ? kula leki
Wanawake huwa tunatofautiana homoni hata ktk uzazi wa mpango mwanamke mwengine akiacha kutumia mwezi huohuo anapata ujauzito na mwengine anachelewa kupata hata mwaka mzima.
huwa iko hivyo.
 
Hakuna kitu Kinachoitwa kubemenda scientifically. Hii ni imani potofu na ilitumika zamani ili kuwafanya wazaz watulie kweny suala la kulea waache kurukaruka.
Kwa hyo kula balanced Diet itakayokidhi mahitaji yako, mahitaj ya aliyeko tumboni na anayenyonya yani ule vzuri haswa.

Mkuu inaelekea hayajakukuta. Whatever the name is but unamuathiri mtoto.
 
Hivi unathubutuje kuita Mawazo ya mtu ni pumba? Hivi kwanini umekosa adabu kiasi hicho? Hebu heshimuni michango ya watu toa ushauri wako bila kumdharirisha mtu, unayemuita pumba ni mtu mzima kama wewe na ana watoto wanamuheshimu, kumtii na kumsikiliza! Si wewe si wizara ya Afya na wala si Google mwenye uwelewa thabiti wa matatizo amayoyapitia mtu wote wana rashia rashia tu
Soma kwanza comments zake huyo niliyemjibu huko mwanzoni utaona chanzo kwa nini nilijibu hivi. Afu wee unayejiona mwenye adabu na kupitia kila Comments na kuijibu au kutoa mawazo ambayo tayari yalitolewa.

Jaribu kujikakamua angalau ujibu au changia kinachoeleweka.
 
Usidharau watu Mkuu! Hao ma Daktari unaowaamini wanatumia uzoefu wa vitabu tu, ndo Yale yale unaambiwa usimpe mtoto chochote ndani ya miezi 6 wakati unaishi Dar joto kalii mtu mzima tu huwez kuvumilia kuto kunywa Maji lakini mtoto unaambiwa usimpe hata robo kijiko, ila cha ajabu sasa watoto wao majumban wanawalea nje ya wanavyokushauri

ni kweli mkuu ila kwa maelezo yake inaonekana kabisa anataka watu wamwambie atoe hiyo mimba kitu ambacho ni kinyume na mafundisho ya dini zote......Daktari anaweza kuwa na ujuzi wa kwamba kuna madhara gani ktk hali km hiyo. vinginevyo tutatumia hisia tuuu zisizo na hoja za kitaalam hata kidogo
 
Jitahidi Kula vizuri,Na huyo mtoto kuharisha inawezekana kuna stage anataka kuingia,usiwaze negative kwamba labda kwakuwa unanyonyesha Basi ndomana unamdhuru mtoto, Mimi ni mjamzito Na nna mtoto anaenyonya.

Na Ana afya nzuri tuu, makadtari wanashauri unaweza kumnyonyesha mpk mimba itakapokuwa ina miezi Sita,hapo ndo sio salama kuendelea kumnyonyesha huyo mtoto..nna mnyonyesha mwanangu Na ninalala nae..

Kikubwa Kula vizuri,Pumzika vizuri,mazoezi,usijipe stress..Na pia usisahau vidonge vya folic acid
 
Back
Top Bottom