Nina mpango wa kuwapandisha Meridianbet mahakamani, wamenidhulumu pesa nyingi sana. Mmiliki ambaye ni Waziri jiandae

Twende nkusindikize ofisini kwao tukadai M hio wakitupa tunaplace odd 4 yako M3
 
Haaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mtafute muhuni mpya wa sheria Pascal Mayalla atakufanyia hiyo kazi ...tena umesema waziri ndiyo muhusika wa hiyo bet basi lazima Pascal atakuja mbio maana hapo kuna kulamba Asali
Kwangu mimi wanasheria na mahakimu na majaji ni wahuni tu wapo kulamba asali
 
Uh - Oh!

Mkuu 'khadijah Mtalame', au ni 'Khadija mtanzania'?
Utatanishi unaanzia hapo kwenye majina yako. Inawezekana huko kwenye shughuli uliyoleta hapa, pia kukawa ni matatizo tupu!

Lakini hili tuliweke pembeni.

Hii stori yako mbona ni kizungumkuti?

Hii pesa ya kuchezea inapatikana wapi siku hizi? Bila shaka ndiyo sababu hata kukawa na kampuni za kitapeli kama hiyo unayojishughulisha nayo, kwa sababu kuna pesa za kuokota hovyohovyo tu, bila ya kuvuja jasho.

Najaribu kutafuta njia ya kukupa pole, lakini nashindwa, kwa sababu naona hii pesa, Tsh milioni moja, au siyo? Huna uchungu nayo hata kidogo.

Ninachoweza kukutakia ni matokeo mema katika kutafuta hiyo pesa nyingine ya kutupa, utakayopata toka kwa hao matapeli unaonuia kuwapeleka mahakamani. Hawa watakuwa na mahela mengi tu, kwani inaonyesha wanayaokota tu kama mchanga vile toka kwa watu kama wewe.

Hebu Kwanza: Mama anaupiga mwingi kwa kuibadilisha Tanzania kuwa kama Las Vegas hivi. Hadi 2025, nchi yetu hii itakuwa imeendelea sana kutokana na mafanikio ya kazi zake hizi; na za mawaziri wawekezaji kwenye miradi muhimu kama huu wa Meridian'.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Dada Hadija pole sana,hiyo Milioni Moja ilikuwa usuke Mkeka upi(mchezo upi)naamini wewe ni Mkongwe kwenye Betting mpaka una-deposit 1ml si mchezo,binafsi naiamini sana SPORTPESA,hayo makampuni mengine naonaga kama ya kisanii
Mi mwenyewe nina app ya sportpesa tu
 
Nenda ofisini kwao makao makuu,ikishindikana hapo nenda bodi ya michezo ya kubahatisha,huitaji wakili wala kwenda mahakamani,hili suala litaishia ofisini kwao,au kwenye bodi.
 
Meridian wana mambo ya kishamba mnoo, kipindi bado nabet, nilifanya muamala kitu kama laki 3 hivi, nilikosea ile namba yangu ya akaunti, wakadai pesa imeingia kwa mwingine tena ni akaunti ipo kenya hivyo pesa hairudi, niligombana nao mwishowe nikapuuzia, wapeleke mahakamani hao kenge.
 
Unaogopa nini kwenda kwenye ofisi yao?
 
Fungua pm yako mama
 
Wakati huohuo mkurugenzi NI Tarimba Abas mkamaria
 
Pesa yangu fulani niliipata baada ya wiki mbili.
Jamaa wasumbufu sana.
Kuanzia usiku saa 4 huwezi kutoa pesa, hata mchana ukitoa pesa inabidi uwacheki Facebook au uwapigie ndipo waupitishe muamala wako.
Playmaster hata ukikosea kudepose wanakuwekea unakokusudia within a minute ukiwapigia tu.
Ukitoa pesa ina toka ndani ya dk 1 tu.
 
Pole sana dada Khadija. Mimi ni Mwanasheria. Na kwa facts ulizozi-narrate hapa inaonekana una kesi nzuri dhidi ya hiyo Kampuni, unless kama kuna taarifa hujazi-disclose.

Ila nikupe angalizo tu kwamba, kumlipa Wakili baada ya kushinda kesi ni kinyume cha maadili ya Mawakili (unethical conduct); ingawa kitendo hicho kinafanyika kwa siri. Unapaswa ulipe kwanza either partly or in full (kulingana na makubaliano), ndiyo kesi iungurume Mahakamani.

By the way, unapatikana Mkoa gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…